wiseboy.
JF-Expert Member
- Aug 11, 2014
- 2,931
- 4,549
Tanzania ni nchi ambayo serikali yake haina dini,ila wananchi wake wana dini,na sote tunaongozwa na katiba ambayo ndio mama wa heri taifa zima,inakuwaje kunafanyika mipango mizito bungeni kuhakikisha kuwa mahakama ya kadhi inakuwepo Tanzania?
Kwanini mambo ya dini yasiamuliwe na mabaraza ya dini husika?
Waislam waende Bakwata na wakristo nao kwao,kupitisha mahakama ya kadhi ni kutulazimisha watanzania wote tuwe waislam.
Sheria haiwezi kuwa kwenye katiba halafu useme inatumika kwa kundi moja katika jamii,kivipi?
Iwapo mahakama ya kadhi itapita basi taifa hili litapasuka,kesho wakristo watakuja na madai yao wakitaka yawemo kwenye katiba,kesho kutwa watakuja wapagani nao na madai yao yawemo kwenye katiba,mwisho wake nini kama siyo mpasuko mkubwa kwa taifa?
Watanzania hatuwezi kukubali kuona mtu anapigwa mawe hadi kuuawa eti kwa kuwa kazini,mahakama ya kadhi haitakuwepo,Tanzania hatuna dini,kila mmoja na aabudu kwa imani yake,imani yako isiwe kero kwa wengine.
Nakupenda Tanzania,MUNGU ILINDE NCHI YANGU ULIYONIPA.