Mahakama ya ICC yatakiwa kuingilia kati mauaji ya raia yanayoendelea DRC

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,502
9,282
759392c4762e4a305f0e84a287b64586

Kiongozi wa mashtaka katika Mahakama ya ICC Fatou Bansouda
KINSHASA,CONGO

MASHIRIKA ya kiraia nchini Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo ( DRC) na sehemu nyengine duniani, yanataka Ofisi ya mwendesha Mashtaka katika Mahakama ya Kimataifa ya ICC, kuchunguza mauaji yanayoendelea Wilayani Beni Mashariki mwa nchi hiyo na wahusika wote kufunguliwa mashtaka.

Wito huu umetolewa wakati mkutano wa nchi wanachama wa Mahakama ya ICC uliofanyika mjini Hague nchini Uholanzi.

Mashirika ya kiraia nchini DRC yakiongozwa na Joseph Dunia Ruyenzi yanataka ofisi ya kiongozi wa mashtaka kuanza mara moja uchunguzi huko Beni.

Tangu mwezi Novemba watu zaiid ya 100 wamepoteza maisha Wilayani Beni, baada ya kushambuliwa na watu wenye silaha wanaoaminiwa kuwa waasi wa ADF Nalu.

Kutokana na utovu wa usalama, jeshi la serikali na lile la kulinda amani MONUSCO limetangaza operesheni ya pamoja dhidi ya makundi ya waasi Mashariki mwa nchi hiyo.

Licha ya operesheni hii, mauaji yameendelea kuripotiwa kila wiki wilayani Beni, huku watu wakiishi kwa hofu na hata kushindwa kwenda kazini.
 
makosa mengi yanayotokea Congo na nchi nyingi tu yapo kwenye kitabu hiki, download bore
 

Attachments

  • MAHAKAMA YA ICC - THE HAGUE.pdf
    1,019.2 KB · Views: 1
Back
Top Bottom