Mahakama ya Afrika Mashariki Arusha: Muendelezo wa kesi ya kuhoji uhalali wa muungano

kupumua ndio mpango
 
Jama
jamani inamaana mkiungana au mkichangia mtaji kibiashara hakuna kugawana kilamtu abaki nachake nikosa?mbona Sudan ilikuwa nchi moja sio muungano lakini zimekuwa nchi mbili je sisi ambao tokazamani zilikuwa nchi 2 zikirudi kama zamani kosa nini?
 
Tanganyika inafaidi nini kutoka zanzibar
SI NDO LAKUSHANGAZA HILO!
NADHANI UKUBWA TUU (PRESTIGIOUS) NDIO FAIDA WANAYOPATA.
MIMIMUBWA LAZIMA NIKUKANDANIZE NA UNIHESHIMU KWA SHIKAMOO KILA SIKU,HUTAKI KONZI .
 
Write your reply...KESI YA KUHOJI UHALALI WA MUUNGANO
Suala la Muungano wa Tanganyika na Zanzibar kuhojiwa kisheria katika Mahakama laendelea kuchukuwa kasi maradufu, licha ya Wazanzibari 40,000 wanaoendelea na kesi dhidi ya Muungano huu, itakayoendelea kusikilizwa katika mahakama ya Haki ya Afrika Mashariki huko Arusha Tanzania bara hivi karibuni, Kwa kusikilizwa ombi no. 7 la mwaka 2018 kuhusiana na waombaji kuiomba Mahakama hiyo kuweka Maskani yake Kwa muda huko Zanzibar Kwa kuisikiliza kesi hiyo ya Muungano ili Wazanzibari waliowengi waweze kuhudhuria Mahakamani Kwa kusikiliza mwenendo mzima wa kesi hiyo.
Waombaji wameiomba Mahakama hiyo Kwa mujibu wa sheria kifungu no. 21 (4) 116 Kwa mujibu wa sheri ya mwaka 2013 za Mahakama hiyo jambo ambalo linakubalika kwa misingi ya hoja, Kwa mujibu wa utaratibu wa kufikia lengo la kuitowa Zanzibar katika Muungano huu Wazanzibari hawa wamejipanga katika mpango wakupata hatua ya mwenendo wa Mahakama na pia kuwasilisha ombi maalumu Kwa Katibu Mkuu wa Umoja wa mataifa kutaka kurejeshewa kwa kiti chake halali katika umoja huo.
Ili Zanzibar iendelee kukitumia kiti chake hicho cha uwanachama wa kudumumu katika umoja huo wa nchi za dunia nzima, ambapo bado Zanzibar ni mwanachama. hivyo, iendelee kuutumia uwanachama wake peke yake kwa manufaa ya Zanzibar na watu wake. katika hatua nyengineyo yenye kuleta sura yenye nguvu ya kuendelea kukataliwa Kwa Muungano huu wa Tanganyika na Zanzibar jopo la wanasheria wa huko Tanganyika wapatao 17 wamejichomoza kushirikiana na wananchi wa Tanganyika kutoka mikoa ya Dar es Salaam, Mtwara, Lindi, Mkoa wa pwani, Tanga, Morogoro, Arusha, Moshi, kigoma na singida Kwa hivi sasa.
lengo kuu ni kuifungulia kesi serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, uhalali wa kisheria wa kuanzishwa kwa Muungano kupitia jamhuri ya Tanganyika dhidi ya Jamhuri ya watu wa Zanzibar. kimsingi hadi hivi sasa utaratibu wa upatikanaji wa majina ya wananchi Kwa kila mkoa majina laki Tatu (300,000) unaendelea, kesi hiyo pia inategemewa kufunguliya katika Mahakama ya Haki ya Afrika Mashariki Arusha, hatua hiyo inategemewa kutekelezwa ndani ya mwezi huu Kwa manufaa ya watu wa Tanganyika pamoja na kuwa viongozi wakuu wa mpango huu hawajawa tayari kutajwa majina yao hadharani Kwa kulinda dhamira yao hiyo ili isije kuvurugwa na wapinga demokrasia na haki za binaadamu nchini.
# AjendaYaZanzibar
 


Mrejesho baada ya usikilizwaji???
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…