Mahakama ni muhimili wa nchi hii au muhimili wa CCM?

kiLimIlire

JF-Expert Member
Apr 8, 2012
311
639
A bell has rang to my brain... Hasa baada ya wana CCM Mwanza kukata rufaa mahakamani dhidi ya mbunge wa Ilemela, Highness Kiwia (CDM), wakipinga ushindi wake wa 2010. Hata baada ya mahakama kuu kanda ya Mwanza kuhamua kuwa Mh. Kiwia alishinda kihalali, na kuwaamulu wana ccm hao kulipa gharama za kesi iliyokuwa imefunguliwa hapo awari dhidi ya Mh. Kiwia,bado wana CCM wanasonga mbele kwa kukata rufaa dhidi ya maamuzi hayo ya Mahakama Kuu kanda ya Mwanza. Kwa mujibu wa rufaa hiyo, walalamikaji wa kesi hiyo ni Yusuph Masengeja Lupilya, Nuru Ramadhan Nsubuga pamoja naBeatus Martin Madege.Wana CCM hao ambao ndiyo walalamikaji wa kesi hiyo ya madai namba 12/2010, wamekata rufaa kwa kile kinachoonekana hukumu ya awali iliyotolewa na Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza, haikuwatendea haki.Nayatazama maamuzi ya mahakama dhidi ya Godbless Lema (CDM) aliyekuwa mbunge wa jimbo la Arusha Mjini kama kiini macho dhidi ya harakati za M4C.Alikadharika Tundu Lisu, mbunge wa Singida Mashariki (CDM) nae aliwekewa pingamizi mahakamani dhidi ya ushindi wake wa ubunge 2010. Pamoja na kushinda ktk kesi hiyo tusishangae wana CCM wakikata rufaa dhidi maamuzi yalompa Mh. Lisu ushindi.Pengine kuna kesi nyingine nyingi dhidi ya wabunge wa CDM.Nachokiona mimi ni mahakama kutumiwa na magamba kuzolotesha harakati za CDM dhidi ya serikali ya magamba hao, kwani itawapasa CDM kuelekeza baadhi ya nguvu zao mahakamani kupambana na nguvu ya sheria ambayo usipokuwa makini unapigwa chini.Iwapo CCM wanaujua umuhimu wa mahakama, mbona hawawapeleki watuhumiwa (mafisadi) wa kashfa mbalimbali zilizopelekea chama hicho kutoaminika miongoni mwa watanzania wengi wa mijini na sasa wa vijijini.Je mahakama imekuwa muhimili wa CCM badala ya Taifa?
 
Bado mihimili ya dola bado haipohuru .mhimili mmoja ndiyo una nguvu dhidi ya mingine yaani serikali .tusubiri mabadiliko ya katiba ndiyo utakuwa huru.
 
Back
Top Bottom