GE2025 Mahakama Kuu yatupilia mbali pingamizi la Tundu Lissu dhidi ya Hati ya Mashtaka

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

DuaZaMama

JF-Expert Member
Joined
Jun 2, 2025
Posts
1,882
Reaction score
4,129
Mahakama Kuu jijini Dar es Salaam imetupilia mbali pingamizi lililowasilishwa na Tundu Lissu kuhusu uhalali wa hati ya mashtaka pamoja na maelezo ya mashahidi ambayo yanadaiwa kuandikwa kinyume cha sheria.
Lissu alidai hati hiyo pamoja na viambatanisho vyake, ikiwemo maelezo ya mashahidi, vimeandikwa kinyume cha sheria na havikidhi matakwa ya kisheria.

1758528718678.png
Katika uamuzi wake, Jaji Nduguru amesema hati ya mashtaka iliyopo Mahakama Kuu ni ileile iliyowasilishwa awali Mahakama ya Kisutu na haijafanyiwa marekebisho yoyote.

Ameeleza kuwa kifungu cha 135 na 138 cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai (CPA) vinaweka wazi matakwa ya kisheria kuhusu muundo na maelezo ya hati ya mashtaka, na kwamba hati iliyowasilishwa inajitosheleza kisheria.

Kuhusu hoja ya maelezo ya mashahidi kuandikwa kinyume cha sheria, Mahakama imekataa pingamizi hilo kwa maelezo kuwa halikuwasilishwa kwa wakati sahihi, na hivyo halina msingi wa kisheria.
Kwa uamuzi huu, shauri la msingi linaendelea kusikilizwa kwa ushahidi.
Endelea kutufatilia kwa taarifa zaidi​
1758528578759.png
 
Lissu aache kjjitetea wafanye wanavyotaka.

Inawezekana vipi mawakili wanaovurunda kwenye kila hatua wawe wako sahihi kila siku mbele ya Mahakama?

Mahakama iliyoshindwa kukemea raia kupigwa katika viunga vya Mahakama mpaka Jaji Mstaafu anajitokeza na kuhoji, ndio itawezza kumtendea Lissu haki?
 
Majaji ni wapumbavu tu pamoja na mawakili wao wa serikali,yote yanafuata maelekezo tu
 
I mnaangaika bure kabisa. Lissu awezi kuachiwa kabla ya uchaguzi. Kinachofanyika hapo ni danadana kuvuta muda, kwa maana ya kesi hapo hakuna kesi
 
Mahakama Kuu jijini Dar es Salaam imetupilia mbali pingamizi lililowasilishwa na Tundu Lissu kuhusu uhalali wa hati ya mashtaka pamoja na maelezo ya mashahidi ambayo yanadaiwa kuandikwa kinyume cha sheria.
Lissu alidai hati hiyo pamoja na viambatanisho vyake, ikiwemo maelezo ya mashahidi, vimeandikwa kinyume cha sheria na havikidhi matakwa ya kisheria.

Katika uamuzi wake, Jaji Nduguru amesema hati ya mashtaka iliyopo Mahakama Kuu ni ileile iliyowasilishwa awali Mahakama ya Kisutu na haijafanyiwa marekebisho yoyote.

Ameeleza kuwa kifungu cha 135 na 138 cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai (CPA) vinaweka wazi matakwa ya kisheria kuhusu muundo na maelezo ya hati ya mashtaka, na kwamba hati iliyowasilishwa inajitosheleza kisheria.

Kuhusu hoja ya maelezo ya mashahidi kuandikwa kinyume cha sheria, Mahakama imekataa pingamizi hilo kwa maelezo kuwa halikuwasilishwa kwa wakati sahihi, na hivyo halina msingi wa kisheria.
Kwa uamuzi huu, shauri la msingi linaendelea kusikilizwa kwa ushahidi.
Endelea kutufatilia kwa taarifa zaidi​
Nyie mbwa wa ccm muachieni lisu mara moja laasivyo tz itawaka moto 29/10/2025
 
Watoe hukumu yao basi ya mchongo. Wasitupotezee muda na wakati tayari wanafahamu wanachokifanya
 
Hawa viongozi wanatuletea matatizo... hivi wana taarifa sahihi kweli?....Anyway muda utaongea
 
Mahakama hii ambayo "Mpiga maadili" Rostam AZIZI alisema zinapigiwa cm? Mimi hata mwenendo nimechoka hata kuufuatilia mana napata kizunguzungu tu. Mashtaka yenyewe ni USENGE MTUPU kutupotezea muda tu.
 
Back
Top Bottom