Mahakama Kuu yatengua Hukumu ya Mbunge wa Kilombero, Peter Lijualikali

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,243
34,903
13882551_1772776119626635_5361149175275392023_n.jpg

Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam imetengua Hukumu iliyotolewa na Mahakama ya wilaya Kilombero dhidi ya Mbunge Peter Lijualikali hivyo katika kesi ya msingi Lijualikali amekutwa hana Hatia.

Mbunge Lijualikali alihukumiwa kwenda Jela Miezi Sita(6) bila faini na Mahakama ya Kilombero. Alikuwa akikabiliwa na Kesi ya kufanya vurugu wakati wa Uchaguzi 2015.

========


Mahakama Kuu kanda ya Dar ES Salaam imetengua hukumu iliyotolewa na Mahakama ya Wilaya Kilombero dhidi ya Mbunge Peter Lijualikali baada ya kukubaliana na warufani kwamba hati ya mashtaka iliyomtia hatiani ilikuwa na upungufu.

Uamuzi huo umetolewa leo mbele ya Jaji Ama- Isaria Munisi baada ya kupitia sababu za kupinga mbunge huyo kutiwa hatiani na kuhukumiwa kifungo cha miezi sita jela.

Peter aliwakilishwa mahakamani na Wakili Tundu Lissu na Fred Kiwelo wakati Jamhuri ilikuwa ikiwakikishwa na Wakili wa Serikali, Faraja Nchimbi.

Mshtakiwa mwingine aliyehukumiwa kifungo cha nje, Stephani Mgatta adhabu yake pia imetenguliwa.

Rejea;

=> Tundu Lissu amesema kuwa CHADEMA itakata rufaa dhidi ya hukumu ya Mbunge kwenda jela miezi sita

=> Mbunge wa Kilombero(CHADEMA) Mh. Lijualikali, afungwa jela miezi sita
 
SASA KESHO MJE MNALIALIA hapa........oooooh tumeshindwa kesi fulani kwasababu ni MAAGIZO toka JUU....ili hali MAHAKAMA kupitia hili la LIJUAKALI inathibitisha kabsa MAHAKAMA ni muhimili unaojitegemea...
Na hiki ni kithibitisho KINGNE wimbo wenu wa kipuuzi JUU YA MAGUFULI ya kuwa anaingilia mihimili MINGNE SI KWELI KABSA......
 
Back
Top Bottom