Mahakama kuamua kesi ya Kinana leo

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,869
1,225
Na Tausi Ally, Mwananchi | Jumatano, Januari 15 2014

Mahakama Kuu Tanzania, Kanda ya Dar es Salaam, leo inatarajiwa kutoa uamuzi, dhidi pingamizi zilizowasilishwa na upande wa mlalamikiwa kwa njia ya maandishi dhidi ya Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana.

Kinana anamtaka Mbunge wa Iringa Mjini (Chadema), Mchungaji Peter Msigwa, kufuta matamshi ya kumkashifu, kumfedhehesha na kumhusisha na ujangili wa meno ya tembo.

Uamuzi huo, unatarajiwa kutolewa na Jaji Zainabu Muruke, baada ya Mchungaji Msigwa kupitia wakili wake, Peter Kibatala kuwasilisha kwa njia ya maandishi, pingamizi lake dhidi ya mlalamikaji ambapo anaiomba mahakama hiyo kuifuta kesi hiyo kwa madai kuwa ina upungufu kisheria.

Kwa mujibu wa Msigwa kupitia wakili wake Kibatala wanadai kuwa kesi hiyo iliyofunguliwa na Kinana dhidi yake, haina mashiko kwa sababu ilikosewa jinsi ya kufunguliwa.

Walidai kuwa kesi hiyo ilikosewa namna ilivyofunguliwa Ilipaswa kufunguliwa mkoani Mwanza ambapo tukio linadaiwa kutokea ama mkoani Iringa kwenye makazi ya kudumu ya Mchungaji Msigwa. Hivyo wanaiomba mahakama kuifuta kwa sababu ina upungufu wa kisheria.

Kinana anaiomba mahakama iamuru Mchugaji Msigwa amlipe kiasi cha Sh 350 milioni kutokana na matamshi ya Aprili 21, 2013, yaliyotolewa katika mkutano wa hadhara.
 
Tuko

JF-Expert Member
Jul 29, 2010
11,184
1,500
Tembo 40 waliuawa mara tu baada ya kusitishwa operesheni tokomeza...
Tujiunge na Msingwa na wadau wengine kupiga vita uharamia huu kwa viumbe hawa wasio na watetezi...
 
nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,869
1,225
Katiba lazima igawe kuwe na NGUVU pekee za MAHAKAMA na POLICE; SHERIA na BUNGE; RAIS... NGUZO TATU... SIO RAIS awe na superpower na ku-manage wote hao...

Sababu Unaona hii kesi nani atashinda pamoja hata na kuwa na ukweli fulani...
 
FOR 2015

JF-Expert Member
Sep 4, 2012
538
0
Duh, Kinana is so Cheap!!!! 350 million? ndio maana ufisadi hauwezi kuisha chini ya CCM.
 
Masulupwete

JF-Expert Member
Feb 15, 2012
1,551
2,000
Huyu msigwa kumbaff kabisa. Sokomoko kalianzisha mwenyewe sasa kimenuka anakimbilia kwenye technicality issues badala ya kupambana kwa hoja alizoanzisha mwenyewe. Huyu ndio tutegemee ajenge hoja ya maana bungeni kweli?? Ama kweli tuna safari ndefu kama nchi.
 
MwanaDiwani

JF-Expert Member
Mar 22, 2013
5,536
1,195
Sasa huyu Msigwa kama kweli anao ushahidi kwa nini anajificha kwenye case technicality ili kesi ifutwe?.

Haoni kuwa hii ndiyo ilikuwa nafasi ya yeye kuyasema machafu yote mbele ya mahakama na wananchi wakauona na kuusikia ushahidi wake.

Huyu Msigwa hana ushahidi wowote na kama angekuwa nao basi asingeliweka pingamizi ili kesi yake ifutwe kabla ya kusikilizwa kwa sababu eti haikufunguliwa Mwanza au Iringa.

Tunachotaka sisi wananchi ni kusikia ushahidi wa tuhuma zake mahakamani na siyo kutaka kujificha kwenye ujanja wa kisheria ambao utatufanya tusisikie ushahidi wowote.
 
Malafyale

JF-Expert Member
Aug 11, 2008
12,978

Msigwa MB haijaikwepa kesi hii!

Kesi ikifutwa Kinana atafungua upya ama Iringa nyumbani kwa Msigwa au Mwanza sehemu aliyo yasema haya maneno!

Sheria za defemation ndiyo zinavyosema!
 
Mkirindi

JF-Expert Member
Mar 2, 2011
5,901
2,000
Ukitaka Kujua Muongo wa siasa ni kama Msigwa, Huyu Bw anatafuta Umaarufu kwa njia za kipoumbavu na zisizo na manufaa yeyote, ni mjinga wa hali ya juu sana, kwani ametumika na Dr Slaa katika hili na akaahidiwa ya kuwa aseme hivyo na atapewa ushahidi, Mpaka leo hajapewa ushahidi. Kinana anasingiziwa na yote haya ni ya uongo, mahakama hiyo hiyo ambayo mnaipenda inapo waachia huru wana CDM wanapopandikizwa mijikesi na polisi na kuishaingilia inapotoa uamuzi wa haki wakati wenu na leo itatoa hukumu ya haki kwenye kesi hii.

Basi Msigwa akishundwa au kuonekana na hatia msije na papara za kesi imechakachuliwa, kaonewa, kuna mkono wa ccm, Rais kaingilia, Kinana kamhonga jaji na kamuahidi Ubunge nk...............

Kueni wapenda haki
 
mcubic

JF-Expert Member
Mar 3, 2011
10,251
2,000
Hivi haya maneno hakuyasemea bungeni....ili awe na kinga? Mleta uzi hebu nisaidie Saa 24:0 AM ni saa ngapi?
 
Baba V

JF-Expert Member
Dec 29, 2010
19,501
1,500
Ukitaka Kujua Muongo wa siasa ni kama Msigwa, Huyu Bw anatafuta Umaarufu kwa njia za kipoumbavu na zisizo na manufaa yeyote, ni mjinga wa hali ya juu sana, kwani ametumika na Dr Slaa katika hili na akaahidiwa ya kuwa aseme hivyo na atapewa ushahidi, Mpaka leo hajapewa ushahidi. Kinana anasingiziwa na yote haya ni ya uongo, mahakama hiyo hiyo ambayo mnaipenda inapo waachia huru wana CDM wanapopandikizwa mijikesi na polisi na kuishaingilia inapotoa uamuzi wa haki wakati wenu na leo itatoa hukumu ya haki kwenye kesi hii.

Basi Msigwa akishundwa au kuonekana na hatia msije na papara za kesi imechakachuliwa, kaonewa, kuna mkono wa ccm, Rais kaingilia, Kinana kamhonga jaji na kamuahidi Ubunge nk...............

Kueni wapenda haki
Is this your price...!? you're so cheap dude..!
 
iPad ya Apple

JF-Expert Member
Jul 21, 2013
322
0
21.04.2012 Ni katika viwanja vya Mbugani jijini mwanza.

Rev. Hon.Peter Msigwa (Mb) Iringa Urban. Aliutangazia umma wa Tanzania kuwa Kinanaaa,,,,,, kinanaaaaa Kinanaaa ni

huyu Katibu mkuu wa CCM Anafanya biashara ya Pembe za Ndovu, anamiliki meli zinazo safirisha pembe za ndovu.

Kinanaaa anakosa na Hana HAKI ya kikatiba ya kuwa nje ya Gereza hadi sasa, lakini kwa sababu serikali ya maccm

ni legerege kinanaaaa adadunda tu majukwaani tu na Balozi wa china nchini Tanzania.

Wenje naye aka panda jukwaani na kusema Kinana adadunda sababu serikali ya CCM ni Importent kutoka juu hadi chini.

Oxford Dictionary Tenth edition inaeleza neno Importent kuwa kitu dhaifu, isiyoweza lolote, Ha.ni.si.

NB:
Tukumbuke pia Leo ni kesi ya Amatus Liyumba ya kukutwa na cm gerezani, intellijensia inasema moja ya Dialled Numbers kwenye cm ya Liyumba baada ya kukamatwa ilikuwa anaongea na Mkulu. Hapa Ngoma inogile.
 
mcubic

JF-Expert Member
Mar 3, 2011
10,251
2,000
Bila shaka Yeriko atawahi mahakamani kutujuza.....Kinana kwa nini hajadai Tsh 1 kama manji alivyomdai fidia kama hiyo Mh mengi?
 
Top Bottom