Magwanda: Ishara ya Udikteta wa wanasiasa!

Magwanda: Ishara ya Udikteta wa wanasiasa!

Kuna msemo unasema "Ukikosea kufunga kishikizo cha mwanzo cha Koti, basi yanayofuata ni matokeo tu ya kosa hilo". Tusimlaumu MS kwa uwezo wake mdogo wa kufikiri, haya ni matokeo ya Elimu ya shule za kata, tunategemea fikira gani toka kwa MS ambaye ni form four leaver (uki penda sema graduate) wa sekondari ya kata!

CHUKUA TANO....Huyu mtu ana mtindio wa akili
 
malaria sugu yani sijui nikuweke kundi gani anyway inaonekana unampenda sana slaa na utampa kura yako ila unaogopa kuisaliti ccm hadharani coz umechakachuliwa,em kata shauri leo chagua slaa kwa mabadiliko
 
kwani mgombea mwenza wa chadema darasa la ngapi?
ok. lkn jee kwnini dk slaa havai suti kama vile akina zito kabwe

JK+na+Mzee+Songambele+na+wana+CCM+wa+Songea+wakisakata+rhumba+baada+ya+JK+kumaliza+kuhutubia+uwanja+wa+Majimaji+leo.jpg
 
images
images
images
images


kila nikiangalia. dk slaa sijawahi kumuona akivaa suti na tai kama tulivyozoea kuona viongozi wetu wakuu. jee dk slaa akiwa rais kama inavyonyesha kwenye jf jee tutegemee aina nyegine ya kivazi
dk slaa akialikwa kimatifa, tutegemee aina nyengine ya mavazi kwa rias wetu?

Mavazi!!!!
 
Magwanda ni ishara ya vita na ukomonisti. CHADEMA wakiingia madarakani watakuwa madikteta kama Hugo Chaves au Fidel Castro.

MnyikaJJ.jpg


Hata Zitto Kabwe naye anavaa. Mpaka sasa asiyevaa haya ni Dr Slaa mnyenyekevu mtumishi wa Mungu

PM

mawazo ya wanafunzi waliosomea huku wanakaa kwenye matofali yana shida sana...hasa ukaja ukajua kompyuta ukubwani ndo tabu kabisa kila ukiona kompyuta basi unataka ku post kitu JF
 
Do not judge book basing on its cover!hayo ni mavazi tu kama mavazi mengine.Ni kama mavazi kama yale wanayofaa makada wa CCM,tofauti ni rangi na aina ya mishono!huu ni ufinyo wa kufikiri wa hali ya juu!
 
Nona CCM wameamua kupenyeza makanjanja kwenye JF ili ku-neutralize upepo mbaya wa kisiasa unaowavumia kila kona. Chakushangaza na kuchekesha ni kuwa hao makanjanja wao hana hoja zenye nguvu na mvuto. Hivi kweli mtu unaweza kupima ubora wa Rais kwa mavazi? Common guys, lets be serious! hivi kwa nini tusirudi kwenye hoja za msingi kama vile:

1. Nani anaweza kupambana na ufisadi na nani hawezi?

2. Nani atasimamia rasilimali zetu kwa makini na nani hataweza?

3. Nani anakerwa na umaskini wa watanzania na nani anachekelea umaskini wa watanzani?

4. Nani anajua sababu ya umaskini wa watanzania na yuko tayari kupambana nao nani hajui sababu ya umaskini wa watanzania na hivyo hawezi kupambana nao?

5. Nani hajali maslahi ya wafanyakazi na hahitaji kura zao na nani anajali maslahi ya wafanyakazi na anahitaji kura zetu ili atatue matatizo yetu? N.K

Taifa hili lina matatizo mengi kiasi kwamba mtu anayepoteza muda kuhoji mavazi ya mgombea ananipa shaka kama kweli ni mtanzania mwenye uchungu na anakerwa na umaskini wetu.


My take: Ni bora tuwe na rais anayevaa magome ya miti lakini mwenye uwezo na utayari wa kushughulikia kero za watanzania hasa, UFISADI Kuliko kuwa na Rais kichwa upepo ambaye hajui hata sababu ya umaskini wetu.
 
Do not judge book basing on its cover!hayo ni mavazi tu kama mavazi mengine.Ni kama mavazi kama yale wanayofaa makada wa CCM,tofauti ni rangi na aina ya mishono!huu ni ufinyo wa kufikiri wa hali ya juu!
Kweli kabisa huyu jamaa badala ya kujadili sera anajadili mavazi, kwani yale ya kijani yana maana gani?
 
kamusi ya kiswahili kwa kiingereza inasema hivi kuhusu gwanda= a worthless cloth or a smock. Ukiangalia kamusi ya kiingereza inasema nini kuhusu "smock" inasema=loose overall worn to protect one's clothes na inaongeza zaidi kwa kusema historically a smock is a linen overgarment worn by an agricultural worker! So MS na wenzio Chadema kuvaa gwanda wanakumbusha kuwa hilo ni vazi la wakulima ambao ndio wazalishaji wa nchi hii, lakini CCM bila kujali wanafuja jasho lao!
 
Magwanda ni ishara ya vita na ukomonisti. CHADEMA wakiingia madarakani watakuwa madikteta kama Hugo Chaves au Fidel Castro.

MnyikaJJ.jpg


Hata Zitto Kabwe naye anavaa. Mpaka sasa asiyevaa haya ni Dr Slaa mnyenyekevu mtumishi wa Mungu

PM

naomba mwenye picha za Mwalimu Nyerere akiwa na magwnda yake maarufu ya mgambo atusaidie. Labda kama unataka kutuambia kuwa Mwalimu Nyerere na CCM ni madikteta ndio maana wanakataa mabadiliko ya Katiba na kungania Katiba ya yenye viraka lukuki.

Hamna hoja zozote zenye maslahi kwa taifa kazi yenu ushabiki wa kivyama tu.
 
Magwanda ni ishara ya vita na ukomonisti. CHADEMA wakiingia madarakani watakuwa madikteta kama Hugo Chaves au Fidel Castro.

MnyikaJJ.jpg


Hata Zitto Kabwe naye anavaa. Mpaka sasa asiyevaa haya ni Dr Slaa mnyenyekevu mtumishi wa Mungu

PM

BILA KAUDIKTETA KIDOGO HALI KAMA HII HAITAKWISHA SOMA HAPA CHINI
Machozi ndani ya daladala

Nikiwa kati ya WATU waliohudhuria mikutano ya kampeni hasa ya urais,nimeona mengi,nimesikia mengi,ahadi kemkem,tam,nzuri na zenye kuvutia na kama JK,SLAA au LIPUMBA mmoja wo akishinda na kutekeleza ahadi zake basi TANZANIA itakuwa kama Boswana au kama sio kuifikia Afica kusini. Sina sababu ya kuzitaja ahadi kwani wengi wenu mwazijua.

Ni saa 12:30 za jioni siku ya ijumaa,natoka ofisini kwangu JMOO nakwenda posta ili kupanda gari la kuelekea mbezi nyumbani kwangu(mbezi ya kimara).Abiria ni wengi kama kawaida,wezi wamo,ila kuna magari ya kwenda mbezi ya buku(elfu moja) naingia na muda si mrefu gari inajaa na kuondoka,wote tumekaa,foleni ni kama kawaida kwani inaanzia faya na uku gari ikiwa imewekwa radio moja ya chama tawala.Watu tupo kimya na aliyesimama ni konda tu.

Mara hiyo radio ikaanza kutangaza sera za mgombea uras wa chama tawala,ahadi nyingi,kile mara iki najua mwazijua sina shida ya kuzitaja ila ni moja tu ambayo nitaitaja ambayo imenipelekea kuandika UJUMBE huu kwenu,ni ile ya KUNUNUA BAJAJI 40 KWA WAMAMA WAJAWAZITO,hapo ni saa 1:30 za jioni na hatujavuka magomeni.

Mara baada ya huyo mgombea kutaja iyo ahadi,nikasikia sauti kuoka nyuma ya gari ikisema “ZIMA RADIO YAKO AU BADILISHA STESHENI”ni sauti ya kike tena mwanamama mjamzito.Dereva alizima radio,tukawa kimya kila mtu nahisi alikuwa anajiuliza kwanini huyu mama kasema radio izimwe au ibadilishe stesheni,ukimya ulitawala kama dk 15.Tukiwa tunaanza foleni ya ubungo pale mahakama ya ndizi au bigbrother, na ikiwa ni saa 2:07 za usiku,nikasikia sauti ya mwanamama mwingine(sio mjamzito) ikisema “KAMA MIMBA ZINGEKUWA ZINABEBWA KWA ZAM HUYU KIKWETE ASINGETAMKA MANENO HAYO”nikashtuka nikageuka nyuma nikakutana uso kwa uso na yule mama mwenye mimba,mimba yake ilikuwa ni kama ya miezi nane tena ilikuwa kubwa(namaanisha tumbo ni kubwa sana).

Tukiwa tupo stand ya mkoa na gari likiwa limesimama na ni saa 2:45 usiku kumbuka nimetoka posta saa 12:30 za jioni.Yule mama mjamzito akasimama akaanza kusema “MIMI SITOMPA KURA KIKWETE KWA JAMBO ILI,NILIKUWA NIMPE ILA KWA JAMBO KAMA ILI SIWEZI KUMPA”uku akilia na kutokwa na machozi,yule mama mwingine aliyesema “kama mimba zingekuwa zinabebwa kwa zam huyu kikwete asingetamka maneno hayo” akaanza kumbembeleza yule mama mjamzito akimsii akae.Nilimtazama kila mtu ndani ya gari sura zilibadilika zikawa sura za majonzi.

Nikatoka kwenye daladala(kimawazo) nikaleta taswila ya BAJAJI nikamuweka yule mama nyuma na mimi nikawa dereva,nikafikiria umbali wa kilometa 50 toka kijijini kwetu kule kanyigo kuja hospital,barabara imejaa mashimo,nikawaza tumbo la yule mama akiwa yuma na uchungu na babaji ikiwa inayumba kwenye mabonde ya barabara,”NILILIA” nilishutushwa na honi nyingi za magari ambazo zilikuwa zikilipigia daladal letu kwa kutotembea, kwani kila mtu alikuwa kwenye mawazo ya yule mama(naisi) na dereva alijisahau kwa kumuonea huruma yule mama.Nilikuwa karibu na dereva nikamuuliza vp?,akajibu “WE ACHA TU”uku akitoa leso na kufuta machozi na kuanza kuendesha gari.

Ni saa 3:07 usiku tupo kimara tunaanza foleni ya kimara stopover,watu wote wapo kimya akuna aliyeshuka mpaka sasa na konda kaka kwenye mlango ameinama,kila mtu kainama,uku wengine wakivuta mafua,na yule mama mjamzito akionekana ana asira na uku machozi yakimtoka yenyewe.Nikajiuliza ina maana watu wote tunakwenda mbezi?,pia huyu mama vp mbona kabadilisha kila mtu ndani ya daladala? Katumwa nini?.Nikasikia sauti ya baba mmoja kutoka katikakti ya gari akisema shusha konda hapo,konda akasema wapi?,baba akajibu hapo hapo,Mmmmmmmmm?,”Samahani konda nilikuwa nashuka bucha nimejisahau” alisikika yule baba akisema,Mmmmmmmmm?.Ndipo nilipoona kila mtu karudi katika hari yake ya kawaida na wengine wakashuka hapo kama watu sita hivi.Nikajiuliza je walikuwa wanawaza nini? Mpaka wapitishwe kituoni?.Je walikuwa katika taswila kama yangu?,au uchovu wa kazi?

Kati ya wale walioshuka pale njiani(sio kituoni) baba mmoja akasema akimwambia yule mama mjamzito “POLE SANA MAMA NA MIMI NAKUHAIDI SITOMPA KURA KIKWETE”akatelemaka.Tunavuka stopover na ni saa 3:30 usiku,kila mtu kaanza kusema lake”KIKWETE HANA AKILI”alisikika baba mmoja,”KIKWETE NI MGONJWA” alisikika dada mmoja,”WANAIGEIZA NCHI YA FAMILIA KWANI HAPA TUNATAWALIWA KIFALME” alisikika kaka mmoja.Ni saa 3:45 nashuka kibanda cha mkaa na niliposimama nikwaambia abilia “HUYO NDIO RAIS WENU HATA KIWA CHIZI SI MLIMCHAGU WENYEWE” nikajibiwa na konda “SHUKA UKO NA NENDA ZAKO”,Mmmmmmmm ata konda?

Nikiwa njiani nakwenda kwangu nikawa natafakari “JE YALE MACHOZI YA MAJI YALIYONDONDOKA NDANI YA DALADALA LEO”je ni ya bure tu?,na je “IPO SIKU YATALIPWA”?,na je “IPO SIKU YATAGEUKA KUWA NI MACHOZI YA DAM”? nisingependa ilo tafakari langu la mwisho litokee.

Je wewe unatoa machozi gani au maneno agani?,je machozi ya furaha? Au ya uzuni kama yule mama mjamzito?au maneno ya kumtukana rais wako kama wale watu kwenye daladala.Kazi kwako. Nikipata nauli kabla ya UCHAGUZI nitakwenda kanyigo nimuulize babu “JE BABU UMESHAWAI KUONA KICHUGUU CHA SENENE”?.​
 
Tumeshuhudia viongozi wa juu wa chadema aikiwemo mgombea wa uraisi Dr. Slaa wakivaa mavazi ya askari wa mgambo kwa miaka isiyopungua mitano sasa. Ilianza kama utani, lakini nadhani ujumbe wa chama wa mabadiliko na matokeo ya uchaguzi vimeonesha wazi significance ya ujumbe wa mavazi hayo.

Mimi nadhani ujumbe mkubwa ni kwamba, wanachadema tuko kwenye kazi ya uaskari kuongoza mapambano ya kidemokrasia hadi mapambazuko ya mabadiliko yaonekane. Matokeo ya uchaguzi huu yanaonesha kuwa bado kazi ni kubwa ya kuelimisha umma, na kuziba mianya yote ya kuhujumu matokeo ya chaguzi zijazo. Inahitaji kila mwanachadema awe askari shupavu, mwenye nidhamu ya hali ya juu kwa viongozi wetu ili tufikie azma hii.

Natoa wito kwa wanachadema na watz wapenda mabadiliko kote, kuvaa sara hizi. Sio kuvaa mwilini tu, bali kwanzi moyoni na katika fikra zetu, kisha mwilini katika shughuli za siasa ili kupeleka ujumbe wa umakini wetu. Let us be as serious and tenecious as a buffalo.
 
Back
Top Bottom