Magufuli: Watanzania wamekata tamaa | Page 2 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Magufuli: Watanzania wamekata tamaa

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Field Marshall ES, Sep 29, 2015.

 1. Field Marshall ES

  Field Marshall ES JF-Expert Member

  #1
  Sep 29, 2015
  Joined: Apr 27, 2006
  Messages: 12,659
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 0
  John Magufuli, amesema amejipanga kulipa deni kwa Watanzania kwa kuleta mabadiliko ya kweli. Amesema pamoja na hali hiyo, anatambua namna wananchi walivyokata tamaa ikiwamo kushindwa kubadili maisha yao, kutokana na ubinafsi wa watu wachache ambao wameamua kujimilikisha rasilimali za nchi.


  "Ninajua Watanzania wanataka mabadiliko ambayo ni M4C yaani ‘Magufuli for Change' na kwa lugha ya kawaida ni Magufuli kwa mabadiliko tena ya kweli," alisema Dk. Magufuli.

  Akizungumza namna atakavyoubadili mji wa Iringa, alisema anajua changamoto zilizopo katika mkoa huo, ikiwamo kero ya barabara hasa za ndani.
  "Ninawashangaa watu wanasema eti CCM haijafanya kitu na wengine ni hapa hapa Iringa mjini tena mchungaji wa kondoo wa Mungu ambaye anazijua amri kumi za Mungu ikiwemo ya kutosema uongo.

  "Tena amekuwa akitukana ovyo ndani na nje ya Bunge nataka kuwaambia mawaziri nao ni binadamu wana nyongo…nataka kuwauliza ikiwa kila siku unamtukana waziri hivi kweli anaweza kukupa fedha za maendeleo, nichagueni mimi na wabunge wa CCM," alisema.

  Alisema anahitaji ushindi wa asilimia 99 ili wapinzani waisome namba kupitia masanduku ya kura.

  Mchagueni Magufuli haya yote ana weza
   
 2. HoodRich

  HoodRich JF-Expert Member

  #21
  Sep 29, 2015
  Joined: Sep 13, 2015
  Messages: 208
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Amekosea kuchagua basi la kupanda, anasifia basi la mabadiliko wkt yeye amepanda basi la hujuma, ufisadi, rushwa, unyanyasaji
   
 3. Borakufa

  Borakufa JF-Expert Member

  #22
  Sep 29, 2015
  Joined: May 26, 2011
  Messages: 1,503
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Viva Jose Viva Jose
   
 4. Ngaramu

  Ngaramu JF-Expert Member

  #23
  Sep 29, 2015
  Joined: May 7, 2009
  Messages: 383
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Chama gani kimetufikisha hapa???????

  CCM out out out!
   
 5. M

  MCHUMIPESA JF-Expert Member

  #24
  Sep 29, 2015
  Joined: Mar 11, 2012
  Messages: 2,095
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  ndani ya xxm kumejaa wezi na wapga dili hakuna mwenye uchungu na watanxania hata mmoja.

  lowasaa atosha wapga dili wa nini???
   
 6. R

  Rafikikabisa JF-Expert Member

  #25
  Sep 29, 2015
  Joined: Nov 6, 2009
  Messages: 252
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 45
  sasa hivi kwa hali ilivyo ground kama tunatemea kura kuna kazi kwa CCM ni ngumu huwezi hamini hata mikoa iliyokuwa haina upinzan imeisha kwenda. Kila aina ya mbinu itatumika hila CCM imechelewa. Meli ya change/mabadiliko inakwenda kwa speed sana.
   
 7. JACKSON WAMBURA

  JACKSON WAMBURA Senior Member

  #26
  Sep 29, 2015
  Joined: Dec 11, 2012
  Messages: 164
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  kwani yule Wa upande Wa pili ye ametokea serikali IPI na kwa miaka mingapi?
   
 8. Obama wa Bongo

  Obama wa Bongo JF-Expert Member

  #27
  Sep 29, 2015
  Joined: May 10, 2012
  Messages: 4,998
  Likes Received: 3,168
  Trophy Points: 280
  babu ES habari za kampeni? nasikia umekuwa kampeni meneja wa yule rafikio billionea..........
  Ila lowassa ameshakuwa rais tayari.
   
 9. s

  simanyane JF-Expert Member

  #28
  Sep 29, 2015
  Joined: Apr 10, 2015
  Messages: 2,256
  Likes Received: 443
  Trophy Points: 180
  Kumbe upo?nilikuwa najiuliza mbona hawa jamaa hawaonekani kutetea mfumo wao waambie na wenzako waje hapa kujibu hoja sio kuchungulia dirishani
   
 10. Mtumishi Wetu

  Mtumishi Wetu JF-Expert Member

  #29
  Sep 29, 2015
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 5,105
  Likes Received: 463
  Trophy Points: 180
  Mr.Zero gharama za maisha ziko juu, bei za vitu muhimu juu k.m. sukari, mafuta, umeme juu yeye anazungumzia mabarabara??
  Namabengo na Nkasi wanakula lami??
  Mabadiliko ni pamoja na kushusha gharama ya maisha ili fedha zetu ziwe na thamani!!
  Sio kutubebesha madeni watu wanakufa kwa maisha duni!!
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 11. N

  Ninaweza JF-Expert Member

  #30
  Sep 29, 2015
  Joined: Dec 14, 2010
  Messages: 7,654
  Likes Received: 1,465
  Trophy Points: 280
  Mkuu alihaidi kufufua nini Iringa, kilicho haribiwa na selekali ya chama tawala?
   
 12. Evelyn Salt

  Evelyn Salt JF-Expert Member

  #31
  Sep 29, 2015
  Joined: Jan 5, 2012
  Messages: 46,227
  Likes Received: 34,419
  Trophy Points: 280
  magufuli anavoongea utadhani sio mwana ccm, utadhani hayupo ndani ya serikali ya jk na ccm kwa ujumla
   
 13. Super Handsome

  Super Handsome JF-Expert Member

  #32
  Sep 29, 2015
  Joined: Jul 16, 2013
  Messages: 3,224
  Likes Received: 3,440
  Trophy Points: 280

  Ha ha ha Le super mogul..haha hii ID si aliikataa?
   
 14. Emmadogo

  Emmadogo JF-Expert Member

  #33
  Sep 29, 2015
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 4,159
  Likes Received: 3,427
  Trophy Points: 280
  Huyu babu nadhani kidonge kimeisha nguvu sasa kichwa chake kinajipeleka tu kama gari la taka

  "eti anashangaa watu wakisema kuwa ccm haijafanya kitu....eti ccm imefanya mengi"

  halafu huyohuyo anasema " wananchi wamekata tamaa" sasa inamaana; kama wamefanya mazuri watu wangekata vipi tamaa. Mwambieni ajitoe tu kwenye mbio za urais maana hata hajui anagombea uwaziri au urasi.

  Eti nina dawa ya wakuu wa shule wanaokula michango...hapohapo kaahidi elimu bure.
   
 15. nkondo

  nkondo Member

  #34
  Sep 29, 2015
  Joined: Jun 28, 2013
  Messages: 64
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 15
  MAGUFULI uko sawa hatuna shida na wewe shida yetu ni CCM haki ya MUNGU ungegombea chama kingine ningekupa kura yangu ila kwa ccm nisamehe bure tumechoka kama unavyosema na wewe umechoka toka huko uje tusaidiane mabadiliko maana hamna namna nyingine sasa waondoke tu
   
 16. SMU

  SMU JF-Expert Member

  #35
  Sep 29, 2015
  Joined: Feb 14, 2008
  Messages: 8,112
  Likes Received: 2,411
  Trophy Points: 280
  Nadhani ukweli ni "tumekatishwa tamaa na CCM"! Tutawaonesha kupitia sanduku la kura ni kwa kiasi gani CCM is such a big disappointment.
   
 17. James7

  James7 Senior Member

  #36
  Sep 29, 2015
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 105
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 45
  Hatuhitaji Rais asiyeweza kudhibiti chuki yake dhidi ya mwananchi. Kama ameweza kuwabagua wana-Iringa akiwa waziri, je akiwa Rais hawezi kuwaua kabisa watu hao?
   
 18. Ng'wale

  Ng'wale JF-Expert Member

  #37
  Sep 29, 2015
  Joined: Nov 24, 2011
  Messages: 1,928
  Likes Received: 731
  Trophy Points: 280
  Ndiyo maana ametoka kule baada ya kuona gari haliendi akabadili na kupanda gari la uhakika. Angekua anaongea akiwa kule ungeungwa mkono, lakini kauona udhaifu ulioko huko akaondoka. Sasahivi wimbo uliopo nchi nzima ni mabadiliko tu, hata Magufuli umempendeza anauimba. Waliambiwa watanyooka wakabisha, sasa kila mtu anaona hata M4C inaigwa!!! kweli huu ni mwaka wa mabadiliko.
   
 19. mwanamby

  mwanamby JF-Expert Member

  #38
  Sep 29, 2015
  Joined: Apr 6, 2015
  Messages: 826
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 33
  Kwahiyo akipita atalipa kisasi kwa wanambeya kisa walimpa makavu live? Mtu yeyote mwenye visasi hafai hata mjumbe wa nyumba kumi.
   
 20. Ryaro wa Ryaro

  Ryaro wa Ryaro JF-Expert Member

  #39
  Sep 29, 2015
  Joined: Oct 4, 2010
  Messages: 2,663
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  Mbona Anawapigia Campaign Wapinzani.Kweli Magufuli si mwanasiasa.

  Waziri miaka 18 Hadi sasa then leo unasema Watz wamekata tamaa.

  Hatudanganyiki jibu LA yote haya ni UKAWA tu.
   
 21. s

  sansiro12 JF-Expert Member

  #40
  Sep 29, 2015
  Joined: Oct 17, 2012
  Messages: 252
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 35
  Nani kawafanya watanzania kukata tamaa????? Let be objective. Serikali ilikuwa wapi?
   
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
Loading...