Magufuli utatoa wapi pesa kutekeleza hii miradi?

Magufuli utatoa wapi pesa kutekeleza hii miradi?

uliza kwanza alitoa wapi hela za kulipia mamia ya km za lami alizofungua kagera,kigoma,tabora na Singida ndio utajua,wakati bado tunakomaa na madini kwwanza tunalala na wawekezaji wa ndani(efds lazima kila mfanyabiashara awe nayo),miradi uliyoitaja hapo sio kwamba yote haijaanza,mfano namba 9(terminal 3),halafu umejifunga kusema hatupati mikopo ya maana wakati Marekani na Gates wameleta neema juzijuzi tu hapa


hehehe eti neema!
 
tulieni mkunwe upele hapa KAZI TUU

Mimi nimeandika kwa hoja, ww inaniqoute badala ya kueleza hoja zako kunipinga unaandika upuuzi halafu unajinasibisha na ccm. Acha utoto dogo kwenye hoja nzito. Acha tujadiliane na kaka zako, ww weka madaftari kwenye bag muda wa shule umefika.
 
Mnarusha rusha miguu tu, kama mnazo tuleteeni pangaboi yetu, kutoka mwezi wa 7 mpaka sasa tunaingia wa 10
 
Nyie endelea kukariri 2019 mwishoni mtashangaa sana,kuna project kibao zipo hewani lakini kwasababu mmejitwisha chuki za kisiasa,mnakuwa blind.Ila nakuhakikishia miaka 2 tu ijayo,hamtaamini macho yenu na uchaguzi 2020 upinzani utapoteza viti vingi sana.Ndo maana wajanja wa upinzani wameshtuka wapo kimya tu.
Haya yalisemwa tangu upinzani ukaingia mpaka leo haujapotea licha ya kuwa mnasaidiwa na vyombo vya ulinzi vyote. Sisi tunaishi humu nchini hiyo miradi ingekuwa inaendelea kujengwa tungeiona. Unayosema kuwa tumejawa na chuki za kisiasa. Nadhani huelewi maana ya chuki wewe. Watu wa upande wenu ndio wamejawa na chuki wanapandikiza chuki kuanzia kwa viongozi wa dini mpaka kwa watoto! Kwa akili zako za kibashite unadhania zile kura mil. 6 walizopata wapinzani ukitoa za kina January makamba hazikuwa lolote wala chochote.
Huku kijijini watu wanaulizia zile mil. 50 kwa kila kijiji vipi? Wanasema miaka inakatika mbona hamleti
 
Mkuu kwanza nikupongeze kwa kujibu kwa hoja na kuweka propaganda pembeni. Sasa najiuliza kwanini mnakimbilia kwenye smg kumbe mngeweza kutoa maelezo mazuri hata kama sio ya mafanikio lakini yanaingia akilini.

Hilo la mradi wa stiegler gorge nasubiri utekekezaji wake zaidi kuliko jitihada ninazoziona sasa. Kuna hii tabia ya kuanza jambo kwa kulitangaza kupata kick kisha linaishia hewani. Mfano ule wa 50m@kijiji mpaka bajeti iliyoisha lakini hakikutekelezwa hata kijiji kimoja na kwenye bajetu ya sasa wala halipo. Utekekezaji wa hili la umeme ni muhimu.

Kwenye viwanda naona nadharia na matarajio yalikuwa juu kuliko uhakilisia ndio maana umeona kuna post inayomuonyesha PM kwenye kiwanda cha twyford, wamesahau hata JPM alionyeshwa akitembelea kiwanda hichohicho. Tumeambiwa Pwani kuna viwanda 300+ lakini hatujawahi hata kuonyeshwa ujenzi wa hivyo viwanda. Hapa ni propaganda kuwapagawisha wananchi ili waimbishwe uchapa kazi.

Ajira, kwa kweli eneo hili awamu hii imeshindwa kabisa na ndio hapo kwa hofu inapowaingia wapiga debe wa awamu hii mpaka kufukia kutaka kuchezea katiba kws kupanua goli kufikia miaka 7. Ukienda kwenye kilimo japo ndio chenye kutoa ajira kubwa ni kama kumemshinda jamaa kabisa na sioni akipaweza. Ajira serekalini napo bado hana jipya kama watangulizi wake.

Kwa hiyo unapoona sisi wapingaji na wakosoaji tunafanya upande wetu msikimbilie kusema tuna chuki bali tuna hoja. Kwa hiyo tunasema ubora wa jamaa tunaupins kwenye maenei hayo na sio kwenye kukunja ndita na kuongea kwa jazba. Tujadilianeni kwa hoja na sio mambo ya smg kwani kwetu tunaona smg zinatumika sio kwa sababu za uzalendo bali nkuficha udhaifu.
Mkuu nakuelewa sana., naamini humu ndani wengi wanakuwaga na nia ya kueleweshana ila kuna wachangiaji wengi ambao tayari wameshajikita katika ushabiki wa kisiasa ambao kuna level mtu akishafika hata thread haisomi hadi mwisho ila akishaona mleta mada ni fulani anaanza kejeli moja kwa moja,namna hiyo hatufiki.

Umewahi kuwa na nia fulani nzuri tu,mfano kwenye dala dala jirani yako umemuona mtu ana mzigo au begi kasimama na abiria waliosimama ni wengi,ila wewe ukiwa kwenye siti ukamwambia akupe begi umshikie ili umpunguzie mzigo,akakupatia na kukushukuru kwa shingo upande huku kila sekunde kumi anakugeukia geukia kama vile usifungue begi kuiba chochote,huwa ukishtuikia hiyo hali unajisikiaje?,.. waweza kutamani umrudishie begi na umtukane,ila kibinadamu unamuweka kwenye nafasi yake,pengine kuna ka laptop kake au ka tecno kake kapya,unakuwa mpole tu.

Sasa ndo kitu kinachosababisha tunaoamini JPM ana nia nzuri,toka akiwa waziri wa ujenzi akipewa bilioni kibao za barabara kilometa nyingi lakini mpaka leo watu wame google akaunti zenye pesa zake wamekosa,huwa tunapatwa na hasira tukiona mtu analazimisha kumtukana na kumkejeli bila ushahidi wakati mwingine hadharani.Amini kitu kimoja,kero za wananchi walio wengi hasa hasa wa chini na wa kati,sio kero ambazo wapinzani wanadhani wanawapigania wananchi wao hasa wa majimboni.

Nipe mfano mmoja wa kero za wananchi wa Singida Mashariki alizokuwa anazipigia kelele Lissu siku za karibuni?
 
first thing first sasa hivi makusanyo yako kwenye 1.3tr na jamaa anataka tufunge huu mwaka na 1.4tr so tunakuwa na hela za miradi kama bilioni 450 kila mwezi,kwa haraka haraka anaweza kukamilisha miradi karibia 10 kwa makusanyo ya miezi 10 pekee,anaposema "Makame tangaza tenda ndani ya wiki tatu mimi najua hela ipo" ni kweli jamaa hatanii


hahaha
 
Nyie endelea kukariri 2019 mwishoni mtashangaa sana,kuna project kibao zipo hewani lakini kwasababu mmejitwisha chuki za kisiasa,mnakuwa blind.Ila nakuhakikishia miaka 2 tu ijayo,hamtaamini macho yenu na uchaguzi 2020 upinzani utapoteza viti vingi sana.Ndo maana wajanja wa upinzani wameshtuka wapo kimya tu.
OP kwa lugha ya Malkia
 
Hebu anaglieni miradi mikubwa inayoanza na itakayoanza mda si mrefu..je hizi peas Magu anatoa wapi??
1.Strogersgorge:2100MW rufiji..
see Wazabuni 66 wajitokeza mradi wa umeme wa Stiegler’s Gorge — Ministry of Energy and Minerals
2. Kupanua Barabara ya Mwenge---Moroko to be 8 lane na fly over ya Moroko na Mwenge
3.Ujenzi wa barabara kutoka Kimara had Chalinxe--8 lane super highway
4.Kuchimba maji kigambon..Kuzalisha lita 50 million per day.
5.Kuleta maji za ziwa Victoria Tabora, Nzega, Igunga
6.Kuunganisha Barabara ya Nyakanazi to Kigoma kwa Rami.
7.Ujenzi wa majengo ya Wizara na Taasis zake Dodoma
8.Kupanua Bandari za Dar na Mtwara na Tanga
9.Kupanua Viwanja vya ndege
10.Kununua ndege zote
11.Kuongeza Mwendo kasi Moroko--Tegeta, Kariakoo Mbagala, Kariakoo tabata
13.Standard Gaurge..14 tirrions costs

Hizi pesa Magu unazitoa wapi wakati makusanyo yanarange tillion 1 kwa mwez, hapo utoe mishahara ya wafanyakazi (550 Billion),Madeni 400 Billion hivyo unabakiza 50 Billion kwa mwezi kwa ajili ya OCs na Miradi ya Maendeleo. Swahi je Magu anatoa wapi hizi pesa za miradi mikubwa hivi wakati mapato nikidogo??? Au anaprint hera. Nasema hvyo kwani serikali haijapata mikopo ya maana tangia iingie madarakani.
Jiulize Watanzania tuyapata wapi hela hii kwa sababu ni miradi yetu wote si ya Magufuli. Kinachokuuma hakuna barabara ya lami kwenda Marangu kama enzi za amani.
 
Hiyo miradi/ ujenzi unaendelea sasa hivi tunapochangia hii mada?

shida sio kuendelea, shida inaendeleaje? maana wewe yawezekana unaishi kwa shemeji yako na watoto kama house boy, issue sio unaishi, issue ni JE UNAISHIJE?
 
shida sio kuendelea, shida inaendeleaje? maana wewe yawezekana unaishi kwa shemeji yako na watoto kama house boy, issue sio unaishi, issue ni JE UNAISHIJE?
Miradi inaendelea aje? Nipatie jibu, bahati mbaya au ni nzuri, sina shemeji wa kumtegemea.
 
Mkuu pitia hiyo link ya mleta mada 1... inaanza na Wazabuni 66 wajitokeza mradi wa umeme wa....,utaona mahali kuna maelezo kama haya ...."
Sambamba na hilo, Dkt. Kalemani aliweka wazi kuwa mkandarasi atakayepewa kazi ya kujenga mradi huo ni yule tu atakayeridhia kujenga mradi kwa gharama nafuu na kwa muda mfupi ndani ya kipindi cha miezi 36.

Alisema kuwa tayari Serikali imetenga fedha za kutekeleza mradi huo ambao unatarajiwa kukamilika ndani ya miaka mitatu baada ya kumpata mzabuni na kuanza ujenzi wake."

Amini maneno yangu serikali sasa hivi ina pesa za kutosha tu,na hii miradi itakamilika kama ilivyopangwa.Swali la mleta mada ni zuri sana na fikirishi.Ukusanyaji wa mapato wa serikali upo juu miaka yote ila pesa zilikuwa zinaishia mikononi mwa wajanja.Nakubaliana na wewe viwanda havijawa vingi kila mkoa kama tulivyotarajia,ila bado ni mapema kuhukumu.Tatizo linaanzia sehemu moja,watanzania wenye uwezo walio wengi hawajazoea pesa za ku hustle,nikupe mfano mmoja wakati fulani 2011 Mh.Ole Sendeka aliwahi kusema bungeni kuwa tungekuwa na watu kama Mengi angalau wawili kila mkoa tungekuwa mbali sana.Watanzania wenye uwezo wa kuanzisha viwanda wapo wengi sana,lakini kutokana na pesa zao zimepatikana kifisadi hawataki kuwekeza pesa katika namna ya ku hustle.Kuendesha kiwanda kunahitaji dedication ya pesa na muda pia.Wengi wanaishia kununua hisa,au kujenga apartments au hotel ambazo mwishowe ajira zinapatikana kwa uchache.Hapo utaona nia ya JPM ni nzuri ila tatizo ni sisi wenyewe.
Tatizo la ajira nakubaliana na wewe kuongezeka,lakini kuna kitu watu wanakisahau.. Tangu miaka kati ya 8 hadi 15 iliyopita intake ya form five.,college, vyuoni pamoja na vyuo vyenyewe vinaongezeka kwa % kubwa kila mwaka,wakati nafasi za serikalini ambayo ndo muajiri mkubwa karibu ni zilezile.Ili ajira ziwe za kutosha ilibidi angalau watu waanzishe viwanda katika sekta binafsi ili angalau sekta binafsi ipunguze pengo la wanaoishia street baada ya kutoka vyuoni.Na kingine watu wanaotoka vyuoni wengi wana mentality ya lazima waajiriwe,hili swala nchi jirani kama Kenya au Nigeria wameshalisahau siku nyingi,ni rahisi kukuta mtu yupo first year ana banda la chips mtaani,wakati akiwa free kidogo jioni waweza mkuta kasimama mwenyewe kwenye goli akimenya viazi au kukaanga chips,na mtaji ni pesa aliyobana kwenye Boom,ila hapa wanashindana kununua galaxy S6 na S7,yule wa Kenya akimaliza chuo tayari ana mtaji wa kuanzisha restaurant wakati huyu wa hapa anakaa kwa shemeji Sinza anayefanya kazi Tigo au Voda huku akiwa amejaa jeuri ya degree aliyoipata na ndoto za mshahara mkubwa na kuendesha IST miezi michache baadae.Mkuu matatizo na changamoto ni nyingi sana,nyingine zinatokana na mifumo aliyoikuta raisi wetu nyingine ni sisi wenyewe,naweza kutoa maelezo page hata 10.
[emoji111][emoji111][emoji111][emoji111] nimekuelewa sana
 
Miradi inaendelea aje? Nipatie jibu, bahati mbaya au ni nzuri, sina shemeji wa kumtegemea.

Ubongo wako mzito sana, nikupe mfano, inawezekana umeachiwa nyumba ya urithi, sawa, ila kila siku twakuona Bar unakunywa, bila kazi, kumbe mwenzetu umeenda CRDB umeacha hati ya nyumba umechukua mkopo, Hauna pesa ila maisha ya bar yanaendelea, sasa swali lako ni sawa na, UNAENDELEAJE KWENDA BAR HUKU HUNA HELA WALA KAZI? SIKU WATAKUJA KUUZA NYUMBA NDO TUTAJUA KWAMBA ULIKUWA UNA MATATIZO.
 
Ubongo wako mzito sana, nikupe mfano, inawezekana umeachiwa nyumba ya urithi, sawa, ila kila siku twakuona Bar unakunywa, bila kazi, kumbe mwenzetu umeenda CRDB umeacha hati ya nyumba umechukua mkopo, Hauna pesa ila maisha ya bar yanaendelea, sasa swali lako ni sawa na, UNAENDELEAJE KWENDA BAR HUKU HUNA HELA WALA KAZI? SIKU WATAKUJA KUUZA NYUMBA NDO TUTAJUA KWAMBA ULIKUWA UNA MATATIZO.
Ndugu, tupunguze siasa, Miradi inaendelea aje?
 
Uchumi wa gesi unatosha kugharimia kila kitu, ila miaka 10 haitoshi kukamilisha hii miradi yote, ndio maana for continuity, tunapendekeza Magufuli andelee kwa miaka 20, tukiona bado anahitajika, then tumpatie indefinite extension kama Kagame, Museveni na Mugabe!.

Kwa Kasi hii ya Magufuli, kuna haja Kufanya Uchaguzi wa Rais 2020?
Paskali
Umeenda mbali zaidi ya Juma Nkamia, hivyo unastahili 'sifa' zaidi yake, kama ni pongezi we uko juu, kama ni kejeli kwa wazo lake we uko juu zaidi
 
Vyanzo viko vingi tu..


Tutakopa+Ongeza kodi zisizo na msingi+Filisi tajiri yoyote atakayekosana na mtakatifu yohana nk
 
Ndugu, tupunguze siasa, Miradi inaendelea aje?

KAMA HUJAELEWA BASI LEVEL YA UELEWA YAKO NI NDOGO SANA, KWA HIYO SINA MDA TENA WA KUENDELEA KUKUELEWESHA, FICHA UJINGA WAKO.
 
Back
Top Bottom