Magufuli ulimtembelea Sumaye. Ina maana na wewe msaliti?

Azim Sokoine

JF-Expert Member
Aug 20, 2014
1,431
2,627
habar wakuu,

Rais Maguful amesikika akisema kuwa wabunge wa ccm waliokuwa wamepanga kwenda kumsalimia Godbless Lema ni wasaliti..kauli ambayo kusema sio nzuri hususani ikiwa imetolewa na mkuu wa nchi kwan yy kama rais anapaswa kuwaunganisha watz kuwa kitu kimoja na sio kutoa kauli za kuligawa taifa.

Wazir mkuu mstaafu ambaye yupo CHADEMA mh Sumaye alikuwa amelazwa hospital na mh Magufuli akaenda kumtembelea..inamaana wanaccm na ww wakuite msaliti kwa ulivyokwenda kumsalimia Sumaye?

Rais Magufuli omba radhi kwa kauli hii.
 
Yaani huoni tofauti ya hivyo vitu viwili na mazingira ya kila tukio? Hospitali na mahabusu ni sawa? Unaweza ukaishi na ukafa hujawahi hata kuuchungulia mlango wa mahabusu lakini hayupo hata mmoja aliyeishi na akafa asihitaji huduma ya utabibu, tena yeye mwenyewe. Haya mambo mawili ni tofauti sana na usirudie tena kuyalinganisha maisha na kwenda mahabusu. Ugonjwa ni maisha.
 
habar wakuu,

Rais Maguful amesikika akisema kuwa wabunge wa ccm waliokuwa wamepanga kwenda kumsalimia Godbless Lema ni wasaliti..kauli ambayo kusema sio nzuri hususani ikiwa imetolewa na mkuu wa nchi kwan yy kama rais anapaswa kuwaunganisha watz kuwa kitu kimoja na sio kutoa kauli za kuligawa taifa.

Wazir mkuu mstaafu ambaye yupo CHADEMA mh Sumaye alikuwa amelazwa hospital na mh Magufuli akaenda kumtembelea..inamaana wanaccm na ww wakuite msaliti kwa ulivyokwenda kumsalimia Sumaye?

Rais Magul omba radhi kwa kauli hii.
Hakuna hiyo , mwache hivyohivyo .
 
Amani iwe nanyi wanajamvi
wameoneshwa adui yao, wanapangiwa namna ya kutumia akili zao , wanatakiwa wawe wabaguzi! hatari kubwa inakinyemelea chama chao.Ambao walikuwa hawaamini, sasa ukweli kauweka wazi kabisa.Kusema kwamba kupanga kwenda kumuona Mheshimiwa Lema gerezani ilikuwa ni usaliti, maana yake ni kwamba Lema alifungwa kwa maelekezo ya mtu! kesho wataambiwa kwenda kumzika Mwana CHADEMA ni usaliti kwa chama chao! wataacha hatafika kumzika Mwana chadema au mpinzani yeyote kisa sisi ni wapinzani wao ni ccm!! UKABURU.

Dhambi ya ubaguzi haiishi vikao vya ndani. Hutoka nje ya mipaka ya vikao.Kuna CCM wengi tu wameolewa na watu wa vyama vya upinzani. kesho wataambiwa ndio wanao toa siri za vikao vyao. Dawa ni kuwatenga! Mnako tupeleka siko !

Mkitubagua hatuta wabagua maana tunajua ubaya dhambi ya ubaguzi. Dhambi ya ubaguzi ni kama kula nyama ya binadamu.ukitubagua kwasababu ya kuwa wapinzani, kesho utabagua watu kwa makabila yao, ukanda wao au kwa Uzanzibar wao.Ubaguzi ukikukolea utawabagua watu hata katik kutoa ajira serikalini.
 
... Kuoa nje ya kabila lako ni usaliti
... Mwalimu kumuoa daktari ni usaliti
... Mkiristo kumwoa mwislamu ni usaliti
... Kupokea msaada wa wazungu ni usaliti
... Serikali kutoa huduma maeneo ya wapinzani ni usaliti
... Kuoa nje ya familia ni usaliti (kaka na dada waoane)

Mkuu wa Kaya asipojaribiwa, Kaya hujaribiwa
 
Tunapoolekea tutakuwa kama Burundi au Rwanda japo tunaoomba yasitimie.

Maaana mkuu ndio Anataka awe Raisi wa maisha wa TZ
 
Back
Top Bottom