kkarumekenge
JF-Expert Member
- Aug 14, 2013
- 1,708
- 1,026
Uongozi ni kutumia hekima na busara. Sheria peke yake siyo uongozi. Awe Mkapa, Pinda na hata Kikwete wamekuwa wakiokoa wananchi mara kadha kutokana na kadhia ya Magufuli. Inadaiwa ati anapendwa, na nani??? Hapendwi, bali anautumia mfumo uliokufa kujikweza na kuonekana yeye ni mchapa kazi. Ni sawa na Mrema. Mrema alikuta mfumo wa utawala uliokufa, kwa hiyo hali kama hiyo huwafanya baadhi yetu kufikiria kuwapa madaraka watu kama kina Magufuli. Kiongozi huongozwa na mambo mengi, maana hata kauli lazima itolewe kwa hekima. Pamoja na kile kilichoonekana ubabe lakini mara nyingi Mkapa alikuwa makini sana katika kuwasilisha ujumbe wake, vivyo hivyo kwa Kikwete na Pinda. Unaposikia kiongozi anatamka haogopi kufa ujue hilo ni janga. Kama haogopi anamtangazia nani. Hao viongozi na mawaziri wa kulialia, nakufa, natishiwa, siogopi nk, hawafai kabisa. Ni majanga!!!
Wewe unabusara gani kama mhuni tu,sheria lazima zifuatwe unajiganya kwa kuvunja sheria halafu unataka eti busara ni akili za kinalisu hizi za unafiki na umbea.