Magufuli,Ubabe katika shughuli za Serikali umepitwa na wakati!

pepopunda

Member
Joined
Sep 16, 2013
Posts
13
Reaction score
7
Mh.Magufuli anatakiwa kujua kwamba Watanzania wa sasa sio wale wa zamani ambao mtu angeweza kuwaburuza atakavyo.Sasa hivi Serikali inaendeshwa kwa misingi ya Utawala Bora.Inashangaza kuona Mh. huyu akitoa majigambo na kumdharau Waziri aliyekuwa ametoa waraka kuruhusu magari yatumiayo barabara zetu kupewa msamaha wa uzito unaofikia asilimia tano ya uzito uliowekwa kisheria.Jambo la kujiuliza ni je,Mh Magufuli kauona lini Waraka huo?Mbona upo tangu mwaka 2006 na yeye amekuwa Waziri wa Wizara hiyo tangu lini?Unafiki wa namna hii ni hatari kwa maendeleo ya nchi hasa pale Serikali inapokuwa na viongozi wa aina ya Mh. Magufuli.Kama kulikuwa na nia nzuri ya kuchukua hatua ya kuufuta huo Waraka Mh. Magufuli alishindwa nini kutoa muda kwa wasafirishaji ili wajue kuwa kuanzia tarehe fulani unafuu uliokuwepo utaondolewa.Viongozi wapenda sifa na wenye majigambo wanawaumiza wananchi kwa maamuzi yao ya kipuuzi na yasiyozingatia busara.Kwamba msafirishaji ambaye gari lake tayari liko njiani atarekebisha vipi mzigo alioubeba kabla ya kufika mizani?Hapo kuna utawala bora?Sasa hivi tayari wananchi wameanza kupata adha ya usafiri kutokana na ubabe wa kiongozi asiye na msimamizi!Mtu huyu anasemekana kuwa anautaka uraisi akiupata nchi hii si itaangamia?
 
Nchi hii ukisimamia sheria zilizotungwa na Bunge unaonekana una kiburi na majivuno. Ukivunja Katiba na Sheria unapigiwa makofi! Bure kabisa. Kama sheria ipo, ni wajibu wa Magufuli kuisimamia. Kama ni mbaya, mwenye fursa na uwezo wa kuiondoa ni Bunge, na si Magufuli. Aliapa kulinda au kuvunja sheria? Kaza buti Magufuli. Watanzania wamezoea kila kitu kiende wanavyotaka. Hatuwezi kufika. Magufuli nasema songa mbele. Bunge lijalo wabadili sheria. Full stop!!!!
 
Tatizo la magufuli liko wapi kama huna matatizo kwa nini mnapenda kushabikia hata maswala ya kihuni unataka watu wafanye ujinga na kusumbua wengine ili iweje wewe kama ulikuwa kwenye mgomo pole sana imekula kwako.
 
Viongozi wa aina ya magufuli ndiyo tunaowataka kwa sasa viongozi wasioweza kusimamia sheria zilizotungwa na bunge hatuwataki wewe na hao wenye maroli wenzako kama mnataka kugoma kagomeni nyumbani kwenu.
 
Tatizo la Mswahili, amezoea WIZI, Akibanwa anatafuta sababu...
 
Ukishajua chanzo cha neno "bongoland", wala hutapata shida juu ya hawa wanaomwandama Magufuli. Nchi hii kila kitu watu wanataka kifanywe kisanii-sanii tu. Ukisikia watu wanamchukia polisi, basi ujue ni yule asiyehongeka! Madereva wakimsifu trafiki, ujue huyo trafiki hatoi adhabu kwa wanaovunja sheria za barabarani. Shuleni ukisikia mwalimu anapewa jina la "mnoko", ujue ni yule anayetaka wanafunzi wawe darasani wakati wa vipindi. Tukiendelea na upuuzi huu nchi hii itakuwa tambara bovu! Najua kwa hili Magufuli atashindwa, maana Pinda hatachelewa kumtaka awaache! Kila kitu nchi hii ni uvunjifu wa sheria tu. Hata hiyo katiba mpya inayokuja, kwa mwenendo huu, bure tu!
 
Viongozi wa aina ya magufuli ndiyo tunaowataka kwa sasa viongozi wasioweza kusimamia sheria zilizotungwa na bunge hatuwataki wewe na hao wenye maroli wenzako kama mnataka kugoma kagomeni nyumbani kwenu.

Sheria gani inayo sema kama unataka kugoma ukae nyumbani?
 
Barabara zinatumiwa na wengi. Si wote wana malori au wanatumia mabasi. Wengine wana Escudo zao. hao wakikwazwa na malori na mabasi yaliyogoma na kuwekwa barabarani, ni kuwaonea. Unapogoma usiibue kero kwa wengine. Goma huko huko nyumbani kwako.
 
Viongozi wa aina ya magufuli ndiyo tunaowataka kwa sasa viongozi wasioweza kusimamia sheria zilizotungwa na bunge hatuwataki wewe na hao wenye maroli wenzako kama mnataka kugoma kagomeni nyumbani kwenu.
Mi nadhani ni kufuata taratibu tu! Huwezi kuzidisha uzito, halafu ukiambiwa hilo ni kosa unagoma, hapana. Kila jambo lina sheria na taratibu zake, ambazo yatupasa tuzifuate.
 
Tatizo la magufuli liko wapi kama huna matatizo kwa nini mnapenda kushabikia hata maswala ya kihuni unataka watu wafanye ujinga na kusumbua wengine ili iweje wewe kama ulikuwa kwenye mgomo pole sana imekula kwako.

hivi wewe unapata wasaa wa kupumzika????
 
Ukishajua chanzo cha neno "bongoland", wala hutapata shida juu ya hawa wanaomwandama Magufuli. Nchi hii kila kitu watu wanataka kifanywe kisanii-sanii tu. Ukisikia watu wanamchukia polisi, basi ujue ni yule asiyehongeka! Madereva wakimsifu trafiki, ujue huyo trafiki hatoi adhabu kwa wanaovunja sheria za barabarani. Shuleni ukisikia mwalimu anapewa jina la "mnoko", ujue ni yule anayetaka wanafunzi wawe darasani wakati wa vipindi. Tukiendelea na upuuzi huu nchi hii itakuwa tambara bovu! Najua kwa hili Magufuli atashindwa, maana Pinda hatachelewa kumtaka awaache! Kila kitu nchi hii ni uvunjifu wa sheria tu. Hata hiyo katiba mpya inayokuja, kwa mwenendo huu, bure tu!

nawachukia sana polisi,tena sana,sana sana,chuki yangu dhidi yao siwez kuielezea,na si kwamba nshawai lala polisi,wala kufanya kosa lolote,,,,na humu nshakula sana ban kisa polisi,,,,
 
Barabara zinatumiwa na wengi. Si wote wana malori au wanatumia mabasi. Wengine wana Escudo zao. hao wakikwazwa na malori na mabasi yaliyogoma na kuwekwa barabarani, ni kuwaonea. Unapogoma usiibue kero kwa wengine. Goma huko huko nyumbani kwako.

Akigoma nyumbani utajuaje kama amegoma au huko likizo?
 
Nchi hii ukisimamia sheria zilizotungwa na Bunge unaonekana una kiburi na majivuno. Ukivunja Katiba na Sheria unapigiwa makofi! Bure kabisa. Kama sheria ipo, ni wajibu wa Magufuli kuisimamia. Kama ni mbaya, mwenye fursa na uwezo wa kuiondoa ni Bunge, na si Magufuli. Aliapa kulinda au kuvunja sheria? Kaza buti Magufuli. Watanzania wamezoea kila kitu kiende wanavyotaka. Hatuwezi kufika. Magufuli nasema songa mbele. Bunge lijalo wabadili sheria. Full stop!!!!

Acha ushabiki wa kijinga. katika swala la kusimamia sheria huwa sharti hekima na busara zitangulie alafu sheria ifuate. Tatizo la Mh. Makufuli busara na hekima o% sifa za kijinga ndio kaweka mbele na ndio maana utaona anatoa kauli za kejeli na dharau uku ajijificha kwemye kivuli cha sheria.
 
Wewe unabusara gani kama mhuni tu,sheria lazima zifuatwe unajiganya kwa kuvunja sheria halafu unataka eti busara ni akili za kinalisu hizi za unafiki na umbea.
 
Back
Top Bottom