Magufuli: Tunakwepa Kodi na Tutazidi Kukwepa Kodi

Magufuli: Tunakwepa Kodi na Tutazidi Kukwepa Kodi

Umeongea point. Mimi watanikamata kwenye PAYE yao tu, kwingine nakuunga mkono.
 
Nakubaliana na mtoa mada, viwango vyetu vya kodi ni vya juu sana kupita nchi nyingi duniani hasa pale unapoleta mizigo kutoka nje ya nchi. Tax code yetu isipofanyiwa marekebisho wengi wataendelea kutumia rushwa ili wapitishe mizigo yao.
 
1.heti=eti

Sidhani na sitaki kuamin kama waliokumbwa na sakata la TRA ni mbuz wa kafara tu lkn wenyew wapo tu wameachwa....

Nakumbuka jukum kubwa walilopewa jopo la maguful kabla ya uchaguz mkuu,lilikua ni kutafuta mianya yote ya mapato na njia za kuongeza mapato kwa kuhakikisha watu hawakimbii kodi (tax evasion & avoidance) ...asa wewe unaanzaje kusema hutalipa na utakwepa kodi?? Unaanzaje kukwepa kodi kwa Magu??

Pia kumbuka kua "TAX IS A NON-QUID PRO QUO PAYMENT"
Heti Magufuli kaja na mtindo wa kutumbua majipu, kawatoa watu wasiokuwa na hatia kafara. Bade kuwa mshabiki wa Lowassa katolewa mbuzi wa kafara naye. Fisadi dagaa Masamaki kwa ulafi wake kanasa kama kambare na wengine wengi. Kikwete aliwaambia kwamba watu wataendelea kukwepa kodi. Ni kweli tutaendelea kukwepa kodi

Nasema kwamba hatutalipa kodi na tutaendelea kukwepa kodi kutokana na sheria kandamizi zilizopo. Kwa nini niagize bidhaa za dola $5,000 alafu ushuru nilipe $5,000, in maana kwamba, sitapata faida, au bidhaa zangu zitakuwa ghali kiasi kwamba sitapata wateja, zaidi, .mfanya kazi wa TRA anayelazimishwa kufikisha target anaamua nilipe kiasi gani. Ninapotafuta fedha za kulipia, penalty za demurrage zinajilimbikiza ili tu nishindwe kulipa zipigwe mnada na wajanja.

Kwa nini nilipe kodi wakati naona kabisa TRA inaniibia. Naagiza gari dogo aina ya Toyota Avensis ya mwaka 2007 kwa dola $2,100 ikiwemo usafirishaji, tena kigari chenye kilomtea zaidi ya laki moja, alafu naambiwa nilipe ushuru $4,225. Wanatumia formula

Dr. Mpango na Magufuli, kwa mwendo huu ili mfanikiwe, rekebiheni sheria za kodi , siyo kutumbua majipu hewa. Tatizo ni sheria na mfumo mzima. Hapa mnajisumbua, tena tutakuja na mbinu mpya za kukwepa kodi. Mimi pamoja na watanzania wengi wataendelea kukwepa kodi hadi sheria kandamizi zitakapoondolewa. Ntaendelea kukwepa kodi hadi watu wenye vipato vya juu nao waanze kulipa kodi. Wabunge na watumishi wengi hawalipi kodi, huku muuza dagaa, au mimi muuza bucha nabanwa. Mtakuwa mbuzi wa kafara nyie wenyewe, na mtatumbuliwa majipu yenu msipokimbia kubadilisha hizi sheria hovyo.
Kumbuka kua = Kumbuka kuwa
Kodi isipokuwa halisi hailipiki na hivyo kufanya watu kujitahidi kukwepa lakini pia kodi isiyolipika ni mtaji wa rushwa kwa watoza kodi.
 
Mtalipa tu.....maana hakuna namna mtakwepa.......mtafuatwa huko huko bila kujali wewe ni mwana ccm......ni mwana cdm.....ni mwana cuf......wote lazima mlipe kodi.......
 
Kodi ilikuwa juu sana kwa sababu TRA walikuwa wanashindwa kufikia target zao sababu moja wapo ilikuwa wanafabiashara wakubwa walikuwa hawalipi kodi. Sasa hivi kodi itashuka kwani kila mtu akilipa kodi TRA wataweza kukusanya zaidi ya target. Lakini kama kawaida kuna wengine wagumu kuelewa watajaribu kukwepa kodi wakikamatwa ni kifungo na fine kubwa. (Sheria lazima iwekali sana kwa wakwepa kodi)
 
Mkuu, TRA imekuwa scheme ya kukomoana.
 
Nimesikia mshahara wa mtu mwenye cheo cha Raisi haukatwi kodi, wa mbunge haukatwi kodi, Vipi wanataka sisi wananchi tulipe kodi wakati wao wenyewe hawalipi kodi?, hii ni double standard
 
Nimesikia mshahara wa mtu mwenye cheo cha Raisi haukatwi kodi, wa mbunge haukatwi kodi, Vipi wanataka sisi wananchi tulipe kodi wakati wao wenyewe hawalipi kodi?, hii ni double standard
Hawa watu wanatuchezea akili kwa sababu akili zetu zimeisha za kuchezewa siku zote
 
Heti Magufuli kaja na mtindo wa kutumbua majipu, kawatoa watu wasiokuwa na hatia kafara. Bade kuwa mshabiki wa Lowassa katolewa mbuzi wa kafara naye. Fisadi dagaa Masamaki kwa ulafi wake kanasa kama kambare na wengine wengi. Kikwete aliwaambia kwamba watu wataendelea kukwepa kodi. Ni kweli tutaendelea kukwepa kodi

Nasema kwamba hatutalipa kodi na tutaendelea kukwepa kodi kutokana na sheria kandamizi zilizopo. Kwa nini niagize bidhaa za dola $5,000 alafu ushuru nilipe $5,000, in maana kwamba, sitapata faida, au bidhaa zangu zitakuwa ghali kiasi kwamba sitapata wateja, zaidi, .mfanya kazi wa TRA anayelazimishwa kufikisha target anaamua nilipe kiasi gani. Ninapotafuta fedha za kulipia, penalty za demurrage zinajilimbikiza ili tu nishindwe kulipa zipigwe mnada na wajanja.

Kwa nini nilipe kodi wakati naona kabisa TRA inaniibia. Naagiza gari dogo aina ya Toyota Avensis ya mwaka 2007 kwa dola $2,100 ikiwemo usafirishaji, tena kigari chenye kilomtea zaidi ya laki moja, alafu naambiwa nilipe ushuru $4,225. Wanatumia formula gani?

Dr. Mpango na Magufuli, kwa mwendo huu ili mfanikiwe, rekebiheni sheria za kodi , siyo kutumbua majipu hewa. Tatizo ni sheria na mfumo mzima. Hapa mnajisumbua, tena tutakuja na mbinu mpya za kukwepa kodi. Mimi pamoja na watanzania wengi wataendelea kukwepa kodi hadi sheria kandamizi zitakapoondolewa. Ntaendelea kukwepa kodi hadi watu wenye vipato vya juu nao waanze kulipa kodi. Wabunge na watumishi wengi hawalipi kodi, huku muuza dagaa, au mimi muuza bucha nabanwa. TRA imekuwa sehemu ya kukomoana. Watu wachini tunanyanyasika huku makampuni makubwa kama Vodacom wanadunda.

Magufuli na kundi lako mtakuwa mbuzi wa kafara nyie wenyewe, na mtatumbuliwa majipu yenu msipokimbia kubadilisha hizi sheria hovyo na kandamizi.
Magufuli anasema: LIPA KODI,
Mfumo unasema: KWEPA KODI. Kweli hii ni DOUBLE STANDARD!
 
Magufuli asipoangalia atajikuta anaua tabaka zima la Wajasiriamali ( Enterpreneurs) wazalendo lililoibuka katika awamu ya nne.
Katika awamu ya nne, wazawa nao waliziona fursa wakachangamka, wakaenda china, wakaleta mzigo, wakafungua fremu na kuuza bidhaa kedekede, Kimsingi Kazi walizokuwa wakifanya Wahindi, Waswahili nao wakaanza kuzifanya.
Ile Kampuni ya Silent Ocean ambayo ni kampuni tanzu ya Home Shopping Center ilifanya kazi kubwa ya kuwasafirishia wananchi mizigo yao kutoka China.
Tatizo lililokuwepo ni kukwepa kodi, Kweli katika hili serikali inafanya vizuri sana kulithibiti.
Hata hivyo Serikali itambue kuwa KODI zake za bidhaa kutoka nje siyo Rafiki wa Wajasiriamali, Zinakwamisha hawa watu kunyanyuka, Ni lazima ifanyike Restructuring ya Mfumo wa Kodi ili kujenga solid base ya Wajasiriamali ambao ndiyo matajiri wa Kesho.
Pili Urasimu na mizunguuko ya Kutoa mizigo bandarini ni usumbufu mtupu, mtu umatumia masiku kibao kuto mizigo, hii siyo nzuri kwa wajasiriamali na watumiaji.
 
Maskini wee mkwepa kodi, usifanye hivyo bwana kama wafanyavyo tigo, na vodacom na njia ya wizi ya nipige tafu, ama kweli una hasira kama za kwangu kwani niliuziwa vitz yangu niliyonunua dola u$450 wao walitaka US$ 1500 iko wapi haki hapa, jamaa wameamua kutupiga eti tusitembee tukiwa tumekaa, watembee wao tu kwenda dodoma, tatizo ni wabunge wetu tuliowatuma, wao wanaona kodi zitoke kwenye magari tu badala wangezitoa kwenye petroli baada ya watu kununua gari, kila siku kukatisha watu tamaa wasinunue mikoko wakati mitumba yenye vilaka, nguo za nylon , midoli wanaachia tu, vichokonoleo pia, hivi tunatumia akili gani , tunazicharge kama betri zikiisha tunarudia mchezo huo. Ifike hatua Magu mwenyewe aishauri bunge iache mambo ya ndiyo mzee wapeleke mswada wa kurekebisha kodi bila kutegemea sana magari na pombe na sigara, tena nisije kusikia mtu anatoza kodi kitimoto maana ndiyo sitarehe iliyobakia .
 
niliwai kupendekeza kodi ya gari ndogo iwe 1,000,000/= na kodi ya magari makubwa iwe 2,000,000/=
 
Back
Top Bottom