Magufuli: Tunakwepa Kodi na Tutazidi Kukwepa Kodi

Mwingereza

JF-Expert Member
Jan 21, 2014
1,115
2,771
Eti Magufuli kaja na mtindo wa kutumbua majipu, kawatoa watu wasiokuwa na hatia kafara. Bade kuwa mshabiki wa Lowassa katolewa mbuzi wa kafara naye. Fisadi dagaa Masamaki kwa ulafi wake kanasa kama kambare na wengine wengi. Kikwete aliwaambia kwamba watu wataendelea kukwepa kodi. Ni kweli tutaendelea kukwepa kodi

Nasema kwamba hatutalipa kodi na tutaendelea kukwepa kodi kutokana na sheria kandamizi zilizopo. Kwa nini niagize bidhaa za dola $5,000 alafu ushuru nilipe $5,000, in maana kwamba, sitapata faida, au bidhaa zangu zitakuwa ghali kiasi kwamba sitapata wateja, zaidi, .mfanya kazi wa TRA anayelazimishwa kufikisha target anaamua nilipe kiasi gani. Ninapotafuta fedha za kulipia, penalty za demurrage zinajilimbikiza ili tu nishindwe kulipa zipigwe mnada na wajanja.

Kwa nini nilipe kodi wakati naona kabisa TRA inaniibia. Naagiza gari dogo aina ya Toyota Avensis ya mwaka 2007 kwa dola $2,100 ikiwemo usafirishaji, tena kigari chenye kilomtea zaidi ya laki moja, alafu naambiwa nilipe ushuru $4,225. Wanatumia formula gani?

Dr. Mpango na Magufuli, kwa mwendo huu ili mfanikiwe, rekebiheni sheria za kodi , siyo kutumbua majipu hewa. Tatizo ni sheria na mfumo mzima. Hapa mnajisumbua, tena tutakuja na mbinu mpya za kukwepa kodi. Mimi pamoja na watanzania wengi wataendelea kukwepa kodi hadi sheria kandamizi zitakapoondolewa. Ntaendelea kukwepa kodi hadi watu wenye vipato vya juu nao waanze kulipa kodi. Wabunge na watumishi wengi hawalipi kodi, huku muuza dagaa, au mimi muuza bucha nabanwa. TRA imekuwa sehemu ya kukomoana. Watu wachini tunanyanyasika huku makampuni makubwa kama Vodacom wanadunda.

Magufuli na kundi lako mtakuwa mbuzi wa kafara nyie wenyewe, na mtatumbuliwa majipu yenu msipokimbia kubadilisha hizi sheria hovyo na kandamizi.
 
Last edited by a moderator:
Kodi zinakwepwa duniani pote,tatizo tu usikamatwe.
Thou shall not get caught, The eleveth commandment
 
mtaishia jela this time, ni lazima serikali makini ikusanye kodi na iwashughulikie kikamilifu wakwepakodi wote

Kodi halali italipwa na sio ya kubambikiwa, kodi gani wanaijua TRA tu? Kila siku kuna kodi mpya, unalipa kodi baada ya miaka miwili unaletewa tena deni lilelile

Mfano hata PAYE yenyewe ni kubwa mno unalipwa laki 7 unakatwa laki 1 nzima kama kodi.

Tatizo TRA sio wabunifu wao wanang'ang'ania watu wachache walipe kodi kubwa badala ya kupanua wigo wa walipa kodi ili kushusha kodi. Kuna watu wengi sana wasio kwenye sekta rasmi hawalipi kodi mfano madalali, mafundi ujenzi au mafundi bomba na wanatukamua sana pesa. Mfano leo mimi nimemwita fundi bomba aje anifanyie kazi kwangu gharama ya vifaa sh 20,000 kazi yenyewe ni ya kama nusu saa ananiambia labour charge sh laki moja nikamtoa mbio sasa wapo wengi wa aina hiyo wanakamata hela ndefu lakini hawalipi kodi
 
Last edited:
Kodi halali italipwa na sio ya kubambikiwa, kodi gani wanaijua TRA tu? Kila siku kuna kodi mpya, unalipa kodi baada ya miaka miwili unaletewa tena deni lilelile

Mfano hata PAYE yenyewe ni kubwa mno unalipwa laki 7 unakatwa laki 1 nzima kama kodi.

Tatizo TRA sio wabunifu wao wanang'ang'ania watu wachache walipe kodi kubwa badala ya kupanua wino wa walipa kodi ili kushusha kodi. Kuna watu wengi sana wasio kwenye sekta rasmi hawalipi kodi mfano madalali, mafundi ujenzi au mafundi bomba na wanatukamua sana pesa. Mfano leo mimi nimemwita fundi bomba aje anifanyie kazi kwangu gharama ya vifaa sh 20,000 kazi yenyewe ni ya kama nusu saa ananiambia labour charge sh laki moja nikamtoa mbio sasa wapo wengi wa jamii hiyo wanakamata hela ndefu lakini hawalipi kodi
Well said @Ndalama Sikafunje
 
1.heti=eti

Sidhani na sitaki kuamin kama waliokumbwa na sakata la TRA ni mbuz wa kafara tu lkn wenyew wapo tu wameachwa....

Nakumbuka jukum kubwa walilopewa jopo la maguful kabla ya uchaguz mkuu,lilikua ni kutafuta mianya yote ya mapato na njia za kuongeza mapato kwa kuhakikisha watu hawakimbii kodi (tax evasion & avoidance) ...asa wewe unaanzaje kusema hutalipa na utakwepa kodi?? Unaanzaje kukwepa kodi kwa Magu??

Pia kumbuka kua "TAX IS A NON-QUID PRO QUO PAYMENT"
 
Kama umemwelewa mleta mada anamaanisha kodi ni kubwa sana na ndo chanzo cha kukwepa kodi. So anachoona hizo rates zirekebishwe ili mambo yawe sana. Halafu kwa maelezo yake anaonesha kuwa atakuwa willing kulipa kodi endapo rates zitakuwa fair.
 
Hata mim naomba unielewe hapo mwisho
 
Hata mim naomba unielewe hapo mwisho
Ofcoz mimekuelewa. Ni kweli hatoweza kukwepa kodi nirahisi nadhani ilikuwa ni demonstration tu kwamba rates are so high.
Lakini pia unaposea quid pro quio what does it mean? Nnavyoelewa kuhusu iyo ni kwamba unapotoa kodi usitegemee kupata return sawa na amount ya kodi uliyotoa, inaweza ikazid au kuwa chini ya hiyo amount so hiyo quid pro quio ulikuwa unamaanisha nn?
 
Back
Top Bottom