Magufuli: Tujadili uwezo wake

Magufuli: Tujadili uwezo wake

Wale wa ccm mukubali tu this election mmepata mgombea by accident lakini hana vigezo stahiki kuongoza taifa hili lenye challanges nyingi . Taifa linahitaji kiongozi mjuaji na mbunifu pia tunahitaji kiongozi mwenye vision na uoni wa tuendako.nina mashaka mara hii tutachagua kwa sababu inabidi kuchagua tu hakuna cha kufanya.
Kikwete juu ya madhaifu yake lakini ni mwanasisa makini na mahiri.mpangaji mikakati na mbunifu pia na yote ni kweli he is a super diplomat...
This time haya tu.....tutafika
 
Mnamjadili mtu ambaye ameshashindwa! nani mwenye akili timamu akamchague Magufuli asiyejua kufikiria au kuwaza?
 
ameshiriki kukataa katiba ya wananchi kwa maneno yake. mtu anayekataa maoni ya wananchi hafai.kuwaambi watu wanaopata chini ya dola moja kwa siku wapige mbizi ni ukatili.
 
"Kulikua na nchi moja inaitwa Libya ilikua imetulia na imeendelea sasa wakapigana wenyewe kwa wenyewe wakamua Sadam...aaah no ni Ghadafi..Sadam ni wa kuwait!"
Huyo ni magufuli...poor foreign policy...ndio nilitaka tujadili uwezo wake ...kwenye haya ni zero....
 
Magufuli nje ya matinga tunga.

Ccm wamemlitisha Magufuli waziri wa barabara kwa miaka mingi tokea ssrikali ya Mkapa.

Amedumu zaidi katika wizara ya bara bara kuliko wiza nyengine alofanyia kazi.

Sifa yake kuu inayotumiwa ma Ccm ni ujenzi wa bara bara. Wizara nyengine alizokaa hakuonekani chochote kile kinacho ashiria ufanisi wake.

Alikuwa waziri wa nyumba na kubwa alofanikisha ni kuuza nyumba za serikalili zenye thamani kubwa kwa bei ya kutupa. Pia akiwajengea mawaziri na senior staff wa serikali nyumba za cimmunity na wengi walikataa kuishi huko.

Utakavokuwa vovote Tanzania itapata Rais au Lowassa ...hili ni kutokana na harakati za siasa zinavo Onekana.

Hivyo kwa vile tunatarajia Labda Magufuli atashinda hivyo tumjadili uwezo wake.

1. Kuna suala mambo ya nje na mahusiano ya nje..jee ana msimamo gani na uwezo wake kifiplomasia uko vipi. Masuala ya EAC . AU UN SADCC Na kuna masuala ya kimataifa.

Masuala ya kushiriki kijeshi nje ya nchi...mfano somali . Kikwete ali kataa kuingilia Somali kijeshi..na haya ni masuala ya Urais.

Tanzania hatuna utaratibu wa bunge kuridhia jeshi letu kushiriki masuala ya nje. Ni rais tu ndio mwamuzi jee magufuli anao uzoefu huu na mamuzi yake bila kuathiri usalama na mahusiano ?

2. Kuna suala la Muungano. Hili suala linahitaji siasa na diplomasia ya hali ya juu.ubabe au kutofahamu siasa yake inaweza kuleta mfarakano. Pale jangwani alisema yeye anachojua ni utanzania tu...watu wengi hawaku notice lakini huo ni udhaifu.

3. Je, magufuli atakubalika na mataifa makubwa wafadhili wetu?

4 Suala la mafuta jee lipi jipya analo litaloifanya Tanzania kufaidi. Dubai na wengine sio miujiza ila ni matumizi mazuri na faida nuu ya mafuta yao.Je, vipi nasi miaka kumi ijayo tutakuwa Dubai ?

5. Suala la ajira na kujaa kwa machunga wa kichina ...hili ni tatizo..hawa wachina wanaingia kwa wastani mmubwa kila siku na chama chake its seems hawana sera ya kueleweka.

Wengi hawa ni chingas tu sio wawekezeja. Pia suala la m TX wa kizungu na Asia ..ni wengi mno.

In fact nusu ya nyumba za Upanga wanaishi ma TX wa nje na kazi zao sio proffesionalns.kule Masaki 90% wanakaa wazungu kama waajiriwa.

Ni wazi nafasi nyingi zimeshikwa wageni...jee magufuli anao ubavu wa kuwaliga stop wageni hawa?

Tumuangalie Magufuli.

Atakua rafiki wa taifa rafiki la Kuwait
 
Back
Top Bottom