Magufuli, Trump, Bolsonaro na Duterte

Magufuli, Trump, Bolsonaro na Duterte

Toosweet

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2012
Posts
2,140
Reaction score
1,983
JF Kwenu,

Katika kipindi cha kuanzia mwaka 2015 mpaka sasa, dunia imejipatia marais wenye msimamo mkali katika kuongoza nchi zao.
Kuna John Magufuli, Donald Trump,Jair Bolsonaro, Rodrigo Duterte.Wengine ambao sitawajadili ni Recep Tayyip Erdogan na Vladimir Putin.
John Magufuli, wakati was kampeni aliahidi kujenga Tanzania yenye kutegemea uchumi wa viwanda. Alipoingia madarakani aliagiza mawaziri na wakuu wa mikoa kwamba klia mkoa uwe na viwanda mia.
Ili kutia msisitizo, wiwanda vilivyobinafsishwa na ambavyo haviendelezwi wala kuzalisha virudishwe kwa Umma(Serikalini).
Likafuata zoezi la kujenga miundombinu ili kukidhi uwepo wa viwanda.
Reli ya SGR imeanza kujengwa kwa kasi kwa 'fedha za ndani'. Fedha zimeelekezwa kwenye baadhi ya maeneo kwa ajili ya Mradi wa Umeme Vijijini(REA).
Kuna mpango umeanza wa ku-invest kwarnye mradi mkubwa wa umeme kwenye bonde la mto Rufiji, yaani Stiegler's Gorge. Mradi huh no wa toka enzi ya uhuru. Kwa sasa efficiency yake au uwezo wa kuzalisha umeme imeshuka mpaka 40%.
Fedha zimetolewa na kununulia ndege ili kuwa na shirika la ndege imara pasipo kupangiwa bajeti. Makao makuu ya nchi yanahamia Dodoma pasipo kupangiwa bajeti.
Taasisi za Serikali na vikundi wanapokea fedha cash 'kutoka kwa rais'.
Vyama vya siasa, asasi za kiraia na taasisi za haki za binadamu wamepigwa stop. Ukikosoa Seriikali utauona moto wake. Uhuru wa maoni uhuru wa kukusanyika, uhuru wa kupata habari, demokrasia nk, kwaheri.
Shughuli nyingi za uchumi zimedorora kwa kuwa serikali inataka kuhodhi kila kitu. Hoteli, Inland Container Terminals, Bureau de Change,Commercial Banks, Community Banks nk, viko hoi.
Waandishi wa habari, wanasiasa, watu wa haki za binadamu, wasomi na wakosoaji wengine wanaisoma namba. Ukileta ujuaji utapotezwa. Wamekomeshwa.

Donald Trump, Rais wa 45 wa Marekani aliyeingia ulingoni mwaka 2016 ni mhafidhina na amechaguliwa toka Republican, chama cha wahafidhina.
Trump hapendi kukosolewa. Ametamka hadharani kuwa mpango wa bima ya afya wa aliyemtangulia, Raise Barack Obama toka Democrat ni wa hovyo. Alijaribu kuufuta ila hajafanikiwa.
Ameponda makubaliano ya Nchi za Ulaya na Marekani juu ya mpango wa nyuklia wa Iran. Mpango huu ulilenga kuifanya Iran isitishe mpango wake wa nyuklia, kwa makubaliano ya kusaidiwa kiuchumi au kupata faida za kiuchimi kama kuuza mafuta kwa uhuru na kufutiwa vikwazo ilivyowekewa awali.
Trump amefuta mpango huo na amerudisha vikwazo kwa Iran. Nchi za Ulaya zimepania kuendelea kufanya biashara na Iran.

Hata wakati wa kampeni, Trump alimsifia sana Putin na kudai yuko imara kuliko Obama. Urusi imeonekana iliingilia uchaguzi wa Marekani wa mwaka 2016,uliomweka Trump madarakani. Vyombo vya usalama vya Marekani vilianzisha uchunguzi ili kubaini ni kina nani walihusika. Maofisa wa Urusi waliobainika kushiriki kudukua taarifa na kuingilia uchaguzi wamewekewa vikwazo na Marekani. Wenzao wa Marekani wametetewa na Trump na wamefanya Marekani igawike kisiasa. Wahusika wengi walikuwa wasaidizi na washauri wa Trump kwenye kampeni.
Wajumbe wa Democrat wametoa shinikizo ili wahusikwa wait we kwenye Seneti(Grand Senate) ili kuhojiwa. Trump amepoteza wateule wake kadhaa kutokana na kukwepa hoja ya Urusi kuingilia uchaguzi wa Marekani. Mwanasheria Mkuu aliyemtetea sana wakati wauteuzi na ambaye alipingwa sana, Jeff Sessions, ameandika barua ya kujiuzulu.Trump amevuruga mtizamo wa Wamarekani kuhusu dunia na mfumo wa demokrasia yao usio wa kibaguzi.
Trump ni mtu asiyeeleweka. Amepata kutamka kuwa NATO ni mzigo kwa Marekani.
Amepanga kuweka uzio kuzuia 'vibaka na wala unga' wa Mexico wasiingie Marekani kwa kuwa wanazuia ajira na kuongeza uhalifu nchini kwake. Ameitaka Mexico ichangie ujenzi wa ukuta.Mexico Imegoma.
Kuna msafara wa wahamiaji toka Honduras na Venezuela wanasafiri maelfu ya kilometa kuja Marekani kupitia Mexico. Trump ametoa onyo kuwa hao ni wahalifu. Hawataingia Marekani. Ameandaa kikosi cha askari zaidi ya 5,000 kuwazuia, wakirusha mawe, watapigwa risasi.

Wako wahamiaji ambao wametengwa na familiar zao. Mtoto anapewa hifadhi, mzazi anarudishwa alikotoka.
Trump anawachukia waandishi wa habari, hasa wa CNN. Katika kikao na waandishi wa habari jana, ameamuru mwandishi wa habari akae chini. Amegoma kujibu swali, amemwambia, "You are a rude, horrible person. You shouldn't be working with the CNN".

Mwishoni mwa mwezi Oktoba Jair Bolsonaro alishinda uchaguzi wa Brazil na kuwa rais. Bado makeke yake hayajaonekana ila msimamo wake uko wazi. Ameshinda kwa zaidi ya 55% ya kura toka chama chake cha PSL, Social Liberal Party.
Chama chake cha sasa ni cha 9 kuwahi kujiunga nacho. Ametokea Christian Democratic Party akiwa Meya.
Bolsonaro ni Conservative. Aliunga mkono utawala wa kidikteta wa kijeshi wa Brazil miaka iliyopita. Wengi wanahofia demokrasia kuminywa.
Bolsonaro ana msimamo mkali juu ya wahalifu na juu ya maadili ndani ya familia. Haya yamemfanya awe na wafuasi wengi hasa vijana kati ya miaka 16 na 24 kwenye nchi ambayo uhalifu na rushwa viko kwa kiwango cha juu.
Kauli zake zimemfanya atuhumiwe mara tatu na kufikishwa mahakamani.
Tarehe 6 mwezi Septemba, alichomwa kisu kwenye kampeni lakini aliendelea na kampeni kwa ku-post video kwa wafuasi wake kutokea hospitali.

Ametoa ahadi kuwa ataruhusu silaha kwa wananchi kwa ajili ya kujilinda. Vilevile atapunguza umri wa mtu kushitakiwa akiwa mtu mzima toka miaka 18 hadi miaka 16.
Ameapa kufuta sheria ya wafungwa kupata ruhusa na kurudi nyumbani wakiwa kifungoni ikiwa wana mambo la dharura(prisoner furloughs).

Bolsonaro ni muumini wa sera za uchumi wa kiliberali. Kuruhusu ubinafsishaji na uhuru wa soko.

Rodrigo Duterte ni Rais mzee zaidi kuwahi kutawala Ufilipino. Ameingia madarakani akiwa na miaka 71,Juni 2016 baada ya kushinda uchaguzi kwa kupata 39.01% ya kura zote. Jina jingine huitwa Digong.
Kabla ya hapo, amekuwa Meya kwa vipindi 7 kwa muda wa miaka22 katika mji wa Davao, ulio kwenye kisiwa cha kusini zaidi cha Mindanao.

Akiwa Meya wa Mindanao, alihusika na mauaji ya watu 1,400 kwa mtindo wa extra judicial killings dhidi ya wahalifu, hasa wala unga.

Aliposhinda uchaguzi, akiwa mwenyeji wa kwanza kwa nafasi hiyo toka kisiwa cha Mindanao, kama populist/nationalist, rais wa 16 wa Ufilipino, aliapa kuanzisha vita na wala unga na wahalifu wengine.

Kwa kutumia Philippine Drug War Squad, mpaka mwaka 2017 Januari,
alishafyeka wala unga 7,000.Polisi wameshaacha hata kutunza takwimu.Ukijulikana unalamba unga, utatembelewa na vijana wa Death Squad na kuuawa, hakuna kesi.
Wala unga, vibaka na watoto wa mtaani ni miongoni kwa waathirika.

Kelele zilipopazwa na mashirika ya utetezi wa haki za binadamu na nchi za Ulaya, Marekani na UN kuhusu mauaji hayo, alitishia kujitoa UN na kuanzisha umoja na nchi za China, Urusi na nchi za Afrika.

Msingi wa watawala hawa ni kufikia malengo bila kujali gharama na jinsi ya kuyafikia malengo.
The ends justify the means.

TS.
 
Kila Rais Duniani Ana Misimamo Yake Binafsi. Kinachotofautiana Ni Umakini Na Ubora Wa Misimamo Hiyo.

Mara Nyingi Misimamo Mibovu Ndio Hufanya Maraisi Wawe Maarufu Zaidi Katika Dunia Hii Iliyochafuka!
 
Wise
 
Umekosea sana kumuweka Trump na hao vichaa mkuu, yaani Trump angekuwa kama huyo Duterte, au Bolsonaro au hata Magufuli, asingemaliza hata mwaka pale Ikulu
Sio fair
 
Nitakushangaa kumponda Magufuli alafu unampongeza Trump! Bora ata umpongeze Magu aiseeeee
 
Huyu Diving nasikia anawachukia sana Mapadri,Nasikia pia anadai Mungu hayupo kwani angekuwepo angemuepusha Mapadri kumvuta masikio.
 
Back
Top Bottom