Shark
JF-Expert Member
- Jan 25, 2010
- 29,986
- 30,179
Wadau,
Style ya Maghufuli ya Kupunguza gharama kwa kuhamisha kusudio la awali la michango au gharama husika limemtokea puani Bwana Harusi mmoja mkazi wa Sinza baada ya Wanakamati kutokubaliana na wazo lake la kuhamishia michango iliyochangwa kwa ajili ya harusi yake kwenye shughuli ingine.
Issue ilianza kwa Bwana Harusi mtarajiwa huyo ambae ndie mweka hazina kuwaambia wanakamati kua nae ameamua kufuata style ya maghufuli hivyo anafuta sherehe zote zilizokua ziendane na shughuli hiyo ya harusi na ameamua kua kiasi kilichochangwa cha Tshs 26Million anaamua kukielekeza kwenye kununua Gari na Kiwanja kwa ajili ya Familia yake tarajiwa. Kikao hicho kilifanyika Urafiki makutini ambako ni maarufu kwa shughuli kama hizo.
Wanakamati hawakukubaliana nae kwani lengo la michango hiyo halikua hilo lililotajwa na Bwana harusi mtarajiwa huyo hivyo hawatoeleweka kwa wachangiaji. Bwana harusi alijitetea kwa kutoa mifano kadhaa ya jinsi Rais Magufuli alivyofuta sherehe mbalimbali na kufanya reallocation ya funds kwa mafanikio.
Mwishowe kikao kilivunjika, Wanakamati kumshambulia Bwana Harusi kwa maneno na nusura wampige kama sio uwezo wa Mbio aliekua na Bwana Harusi. Mi nlikua napita tu maeneo hayo ghafla nikashuhudia mtu akitimua mbio, baada ya kuuliza ndo nikapewa huu mkasa