Magufuli siyo mnafiki, Magufuli sio mjinga. Ana uhakika wa kurudi madarakani 2020

herzegovina

JF-Expert Member
Oct 28, 2015
3,141
4,721
Kichwani kwa JPM kuna viwili ambavyo kati ya hivyo viwili, ana uhakika Wa 100% na kimoja wapo.

1. JPM ana uhakika Wa asilimia 100 kuwa ni lazima atarudi tena madarakani mwaka 2020. Inaweza kuwa "at any cost" au kwa ile imani yake kuwa wanaompinga ni kikundi "kidogo tu" cha mitandaoni na sio watanzania walio wengi. Inawezekana JPM ameomba takwimu za watu wanaotumia mitandao katika nchi hii na kugundua kuwa ni asilimia ndogo sana ukilinganisha na wasiotumia mitandao ya kijamii.

Hili linamfanya JPM kusema/kufanya lolote lile analojisikia bila kujali anamuumiza nani....bila kujali inaleta tafsiri gani....bila kujali chochote kile kwa sababu ana uhakika Wa 100% kuwa atarudi tu madarakani.

2. JPM ana uhakika kuwa hawezi kurudi madarakani hata iweje kwani nchi imeshamshinda hivyo anashindana na wananchi wake kwa kuwa yeye ndiye Mwenye mamlaka kuu ya maamuzi.

Hili linamfanya aende kinyume na kila kitu ambacho wananchi wanataka ili awakomoe. Mkitaka katiba mpya anawaambia bado ananyoosha nchi, mkitaka mpande madaraja anawaambia bado anahakiki watumishi (same applies to madai ya walimu), mkitaka awatembelee wahanga Wa majanga, haendi na akienda hawapi faraja Bali anawakejeli....mkitaka awaondoe viongozi wasio na sifa, hawaondoi.....MWISHO KABISA ANAWAAMBIA, YEYE HUWA HAPANGIWI.

NINA UHAKIKA, ANA UHAKIKA NA KIMOJA WAPO KATI YA HIVYO.
 
Nadhani kwenye uongo ulimaanisha sio mwongo hodari.,kila uongo wake unashtukiwa mapema.
Anakuwa frustrated,anapanick na kuanza kutisha watu.

Kuhusu Unafki. That ship has sailed the moment aliposema yeye ni maema kweli daima same time tunashuhudia kila siku akidanganya.

Soundbite ya kusema ya moyoni nayo imechuja kwa sababu huko moyoni sio lazima kuwe na facts na ukweli, kunaweza kuwa kumejaa hila, ufedhuli na kila aina ya ubaya.

Kama mnabisha tazameni double standard za issue ya BASHITE
 
Haya ngoja tuangalie mpira utakuwaje hiyo 2020, wananchi sio watu wa kihivyo anavyowahic yeye.
 
  • Thanks
Reactions: SDG
Kichwani kwa JPM kuna viwili ambavyo kati ya hivyo viwili, ana uhakika Wa 100% na kimoja wapo.

1. JPM ana uhakika Wa asilimia 100 kuwa ni lazima atarudi tena madarakani mwaka 2020. Inaweza kuwa "at any cost" au kwa ile imani yake kuwa wanaompinga ni kikundi "kidogo tu" cha mitandaoni na sio watanzania walio wengi. Inawezekana JPM ameomba takwimu za watu wanaotumia mitandao katika nchi hii na kugundua kuwa ni asilimia ndogo sana ukilinganisha na wasiotumia mitandao ya kijamii.

Hili linamfanya JPM kusema/kufanya lolote lile analojisikia bila kujali anamuumiza nani....bila kujali inaleta tafsiri gani....bila kujali chochote kile kwa sababu ana uhakika Wa 100% kuwa atarudi tu madarakani.

2. JPM ana uhakika kuwa hawezi kurudi madarakani hata iweje kwani nchi imeshamshinda hivyo anashindana na wananchi wake kwa kuwa yeye ndiye Mwenye mamlaka kuu ya maamuzi.

Hili linamfanya aende kinyume na kila kitu ambacho wananchi wanataka ili awakomoe. Mkitaka katiba mpya anawaambia bado ananyoosha nchi, mkitaka mpande madaraja anawaambia bado anahakiki watumishi (same applies to madai ya walimu), mkitaka awatembelee wahanga Wa majanga, haendi na akienda hawapi faraja Bali anawakejeli....mkitaka awaondoe viongozi wasio na sifa, hawaondoi.....MWISHO KABISA ANAWAAMBIA, YEYE HUWA HAPANGIWI.

NINA UHAKIKA, ANA UHAKIKA NA KIMOJA WAPO KATI YA HIVYO.
Swali dogo..nini maana ya kuwa kiongozi halafu bado wanaoongozwa wanataka wasimame mbele waelekeze..
 
NAIJIBU HEADING YAKO.
Magufuli anajua fika kuwa yeye ni mnafiki aliyebobea.

Magufuli anajua kuwa anazo qualifications zoote za kuitwa mjinga (kwa mujibu wa katiba)

Magufuli anajua kabisa hatakiwi kuendelea kuwepo ikulu achilia mbali kurudi tena 2020 (reason:- hayuko tayari kupangiwa cha kufanya kama katiba inavyoelekeza)
 
Back
Top Bottom