Magufuli: Nimeigawa MV Dsm kwa JWTZ, wale wanaoiandika andika, wajue wanaandika "mzinga wa JWTZ"

barafu

JF-Expert Member
Apr 28, 2013
6,739
32,866
image.jpeg

Picha hii ni ufunguzi wa Kivuko cha Mv Dar Es Salaam

Rais Magufuli ametamka tena.Kauli ambayo inaweza kuzua tena mjadala japo yeye ameaasa kuwa wanaojadili wajue wanajadili "kifaa cha jeshi"

Leo katika hotuba fupi baada ya kuapisha wateule wake katika jeshi,polisi na mashauriano ya kigeni, Rais Magufuli amesema ile meli/kivuko cha "Mv Dar es Salaam" ambacho watu wamekuwa wakiisemasema, sasa ameamua kukigawa kwa JWTZ kikosi cha Wanamaji.

Lengo la kugawa Kivuko hicho ni kurahisisha ulinzi na patrol katika eneo la bahari ya Hindi ili kuweza kudhibiti magendo na uingizaji wa bidhaa haramu pamoja na wahamiaji haramu wanaotumia pwani na fukwe za bahari ya Hindi kuingia ndani ya nchi.

Rais anasema Kivuko hicho kwa sasa ni mali ya JWTZ na sio tena kwa ajili ya safari za Dsm-Bagamoyo.

Rais anasema Kivuko ambacho kilitambulika kama MV DAR ES SALAAM kwa sasa kina Namba za Jeshi na kimesajiliwa kama kifaa cha Jeshi.

Kwa hiyo wale waliokuwa wanakisemasema na kukiandika, waache mara moja maana kwa sasa Kivuko hicho ni mali ya JWTZ na ni sawa na "Mzinga wa Jeshi" ambao habari zake hazipaswi kuandikwa hovyohovyo.

Rais JPM anasema "Kwa hiyo wale wanao-andikaandika, wajue Kivuko hicho kwa sasa ni mali ya jeshi, ni kama Mzinga au kifaru cha jeshi"

Kwa kauli hiyo, Rais anatahadhalisha kuwa waandishi waache kuhoji na kuandika juu ya Kivuko hicho,kwani kwa sasa ni kama "Mzinga au Kifaru cha Jeshi" ambapo katazo lake lilishakatoka, kwamba kuandika juu ya vifaa vya JWTZ toka kipindi kile gazeti la "Dira ya Mtanzania" lilipoandika "Wanakijiji Waiba kifaru cha JWTZ"

Habari ile ilizua taharuki, waandishi kukamatwa na msemaji wa JWTZ wakati huo, ambae kwa sasa ndio Katibu wa Mashauriano ya Kigeni wa CCM Kanali Ngeleba Lubinga alipiga mkwara. Ikiwa ni zuio kuwa waandishi wasiandike habari za jeshi bila taarifa rasmi.

Kanali Lubinga(kada na kiongozi wa CCM) alisema "Sadism is inevitable when the situation is Alarming". Na baadae Kanali Lubinga alisema "Aliyeandika juu ya kifaru cha jeshi kuibiwa, atawasimulia tumemshughulikiaje"

Kauli hii ilikuwa ni onyo kwa watu na waandishi wa habari kuandika habari zinazohusu JWTZ na vifaa vyake.Kwa kauli ya leo ya Mh.Rais kuwa "Mv Dsm" ameigawa kwa jeshi,na hivyo kwa sasa ni kama "kifaru au mzinga" wa jeshi,na hapo hapo kusisitiza kuwa waliokuwa wanaandika juu ya Kivuko hiki wajue sasa wanaandika "mzinga" wa Jeshi ambao Kanali Lubinga alishaonya kuwa "sadism" haizuiliki.

Tukijikumbusha, hii Mv Dsm ilizua mjadala sana juu ya ghalama zake na ukweli wa kasi yake.Ilionekana kiasi kilichotumika kununua kwanza hakikufuata sheria za manunuzi ya umma,na ubora wake ulikuwa katika mashaka makubwa.

Mimi nazungumzia MV Dsm hii kwenye picha,siyo huo "mzinga wa JWTZ" aliousema Rais.

Kwa zaidi tujikumbushe hapa juu ya MV DAR ES SALAAM
MV Dar es Salaam kufa kabla ya kuanza kazi?
 
Ingekua busara angetumia hiyo nafasi kujibu tuhuma za ufisadi kuhusu hicho kivuko, sio kuja na kauli za vitisho......

Tujitahidi kutenganisha Jeshi na kashfa za kisiasa, Jeshi lisiwe dampo la wanasiasa kufichia maovu yao.....Naona ya Meremeta yanajirudia.
 
Haaaah sometimes inabidi kucheka tu ......

Kuna muda Rais namwelewa sana lakini kuna muda nashindwa kumwelewa kabisa kwa kauli zake............

Hivi JWTZ ndio watumie vitu vibovu na wananchi wasiseme kisa kuogopa?...................

Siku kikiwamwaga kwenye maji na wakafa itakuwa ni faida ya nani?...........
 
View attachment 467730 Picha hii ni ufunguzi wa Kivuko cha Mv Dar Es Salaam

Rais Magufuli ametamka tena.Kauli ambayo inaweza kuzua tena mjadala japo yeye ameaasa kuwa wanaojadili wajue wanajadili "kifaa cha jeshi"

Leo katika hotuba fupi baada ya kuapisha wateule wake katika jeshi,polisi na mashauriano ya kigeni,Rais Magufuli amesema ile meli/kivuko cha "Mv Dar es Salaam" ambacho watu wamekuwa wakiisemasema,sasa ameamua kukigawa kwa JWTZ kikosi cha wanamaji.

Lengo la kugawa Kivuko hicho ni kurahisisha ulinzi na patrol katika eneo la bahari ya Hindi ili kuweza kudhibiti magendo na uingizaji wa bidhaa haramu pamoja na wahamiaji haramu wanaotumia pwani na fukwe za bahari ya Hindi kuingia ndani ya nchi.

Rais anasema Kivuko hicho kwa sasa ni mali ya JWTZ na sio tena kwa ajili ya safari za Dsm-Bagamoyo.Rais anasema Kivuko ambacho kilitambulika kama MV DAR ES SALAAM kwa sasa kina namba za jeshi na kimesajiliwa kama kifaa cha jeshi.

Kwa hiyo wale waliokuwa wanakisemasema na kukiandika,waache mara moja maana kwa sasa,Kivuko hicho ni mali ya JWTZ na ni sawa na "Mzinga wa Jeshi" ambao habari zake hazipaswi kuandikwa hovyohovyo.

Rais JPM anasema "Kwa hiyo wale wanao andikaandika,wajue Kivuko hicho kwa sasa ni mali ya jeshi,ni kama Mzinga au kifaru cha jeshi"

Kwa kauli hiyo,Rais anatahadhalisha kuwa waandishi waache kuhoji na kuandika juu ya Kivuko hicho,kwani kwa sasa ni kama "Mzinga au Kifaru cha Jeshi" ,ambapo katazo lake lilishakatoka ,kwamba kuandika juu ya vifaa vya JWTZ toka kipindi kile gazeti la "Dira ya Mtanzania" lilipoandika "Wanakijiji Waiba kifaru cha JWTZ"

Habari ile ilizua taharuki,waandishi kukamatwa,na msemaji wa JWTZ wakati huo,ambae kwa sasa ndio Katibu wa Mashauriano ya Kigeni wa CCM Kanali Ngeleba Lubinga alipiga mkwara.Ikawa ni zuio kuwa waandishi wasiandike habari za jeshi bila taarifa rasmi.

Kanali Lubinga(kada na kiongozi wa CCM) alisema "Sadism is inevitable when the situation is Alarming.Na baadae Kanali Lubinga alisema "Aliyeandika juu ya kifaru cha jeshi kuibiwa,atawasimulia tumemshughulikiaje"

Kauli hii ilikuwa ni onyo kwa watu na waandishi wa habari kuandika habari zinazohusu JWTZ na vifaa vyake.Kwa kauli ya leo ya Mh.Rais kuwa "Mv Dsm" ameigawa kwa jeshi,na hivyo kwa sasa ni kama "kifaru au mzinga" wa jeshi,na hapo hapo kusisitiza kuwa waliokuwa wanaandika juu ya Kivuko hiki wajue sasa wanaandika "mzinga" wa Jeshi ambao Kanali Lubinga alishaonya kuwa "sadism" haizuiliki.

Tukijikumbusha,hii Mv Dsm ilizua mjadala sana juu ya ghalama zake na ukweli wa kasi yake.Ilionekana kiasi kilichotumika kununua kwanza hakikufuata sheria za manunuzi ya umma,na ubora wake ulikuwa katika mashaka makubwa.

Mimi nazungumzia MV Dsm hii kwenye picha,siyo huo "mzinga wa JWTZ" aliousema Rais.

Kwa zaidi tujikumbushe hapa juu ya MV DAR ES SALAAM
Why MV Dar project could fail before its official launch
Aiseee naita miujiza
 
Haaaah sometimes inabidi kucheka tu ......

Kuna muda Rais namwelewa sana lakini kuna muda nashindwa kumwelewa kabisa kwa kauli zake............

Hivi JWTZ ndio watumie vitu vibovu na wananchi wasiseme kisa kuogopa?...................

Siku kikiwamwaga kwenye maji na wakafa itakuwa ni faida ya nani?...........

Wanajeshi wanajua kupiga mbizi hawatazama!
 
Haaaah sometimes inabidi kucheka tu ......

Kuna muda Rais namwelewa sana lakini kuna muda nashindwa kumwelewa kabisa kwa kauli zake............

Hivi JWTZ ndio watumie vitu vibovu na wananchi wasiseme kisa kuogopa?...................

Siku kikiwamwaga kwenye maji na wakafa itakuwa ni faida ya nani?...........
Kakimbia scandal yake kiaina ila records hazifutiki milele.

Yeye ndiyo muhusika mkuu wa hii MV Mbovu asijidai kuwarushia jeshi vitu vilivyooza
 
Back
Top Bottom