Magufuli ni Tingatinga? Hebu someni hapa!

Magufuli ni Tingatinga? Hebu someni hapa!

mcfm40

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2010
Posts
4,452
Reaction score
3,152
Wakati wa kupitishwa kugombea kwa tiketi ya CCM, Kikwete alimpa Magufuli a.k.a ya Tingatinga. Na tangu hapo katika mikutano yake huyo Tingatinga ya kujitambulisha amekuwa akiitwa tingatinga na mgombea mwenza wake. Na naona pia baadhi ya vyombo vya habari vimelidaka hilo.

Hebu tulichambue hili neno tingatinga. Tingatinga ama buldozer kwa kimombo ni mtambo ambao mara nyingi unatumika kuchimba barabara. Lina uwezo wa kuzoa na kubomoa iwe nyumba au miti na kusafisha njia kwa muda mfupi. Lakini Tingatinga halijiendeshi lenyewe, linaendeshwa na mtaalamu anayejua namna ya kulitumia kwa kazi kusudiwa. Na hii ndio point yangu.

Hii ni kusema kuwa waliomwita Magufuli Tingatinga hawakukosea. Ni mtu anayehitaji kuendeshwa na kufungwa spidi gavana. Ni mtu anayefuata sheria bila kutumia busara. Kama vile ukiliacha tinga tinga bila kuliongoza linaweza kubomoa na kuharibu hata kile ambacho hakikusudiwa. Hili lijionesha mara kadhaa kwa Magufi. Kikwete alishawahi kumwambia awe na huruma kwa wananchi. Pia Pinda alishawahi kumpiga stop kuzuia malori yenye uzito mkubwa kupita barabarani. Magufuli ni mchapa kazi lakini ni mtu anayehitaji kufungwa gavana.

Je ni nani atakuwa dereva wa hili tingatinga? Je hili Tingatinga litaachwa bila dereva? Ni wazi aliyemwita tingatinga anajua wazi yeye ni mmoja wa madereva wa hili Tingatinga akipokezana Mkapa. Magufuli akibahatika kuwa rais watakao kuwa wanaongoza ni hawahawa kina Kikwete na Mkapa.

Kumteua Maguli kugombea urais ilikuwa kosa la kiufundi. Magufuli sio kiongozi, bali ni mtendaji. Kiongozi ni mtu wa maono na kutoa dira, mtu wa ideas. Rais ni nembo, ni alama, ni mtu 'abstract'. Haingii kwenye mawizara kufuatilia utekelezaji. Rais hawezi kupambana na wazembe kwa sababu hana nafasi hiyo. Rais anakaa ikulu. Analetewa taarifa na tu wasaidizi wake. Magufuli hakluandaliwa kuwa rais hata ukimsikliza hotuba zake, kwanza Hana personal vision. Anasema tu atatekeleza ilani ya CCM. aNASEMA ATAPAMBANA NA WATENDAJI WWAZEMBE. Anazungumza km vile ni waziri. Rais hawezi kuapmbana na watendaji wabovu,. ndio maana Kikwte alishindwa. Hiyo ni kazi ya waziri mkuu akisaidiana na mawaziri wake. WAZIRI MKUU AKIWA LEGELEGE BASI HAKUNA KITACHOENDELEA.

Waziri Mkuu ndiye mtendaji ndiye anayeweza kwenda popote bila kuhitaji presidential motarcade na mbwembwe nyingi. Ndiye anayesimamia wizara ili zitekeleze majukumu yake. Hii sio kazi ya rais. Kwa maana hiyo basi kumteua Magufuli kugombea urais CCM imeangalia tu ushindi bila kuangalia personality ya mtu huyo na maana halisi ya cheo hicho. MAGUFULI ALIPASWA AWE WAZIRI MKUU, NDIO NATURE YAKE. NDIO KIPAJI CHAKE, UFUATILIAJI WA MAMBO. KUMFANYA RAIS NI KUMFUNGA MIKONO NA HAPA TUMEMISUSE RESOURCE MUHIMU SANA. KATIKA NGAZI YA URASI MAGUFULI ATAKUWA MWINGINE KABISA kama akibahatika KWA SABABU YA MIIKO YA NAFaSI YENYEWE.

Udhaifu mwingine wa Magufuli. Hana uzoefu wowote wa kimataifa. hana ABCs za elimu ya siasa, hana ABCs za uchumi. Ni mwanasyansi mkemia. Kwa maneno mengine, Magufuli is very mechanical. Labda itabidi kama akichaguliwa miaka miwili ya kwanza katika hiyo nafasi akapate kozi za uongozi, siasa na uchumi. MAGUFULI HAKUANDALIWA KUWA RAIS. HIVYO KM ATACHAGULIWA TUTAENDELEA KUONGOZWA NA HAWA MARAIS WASTAAFU WALAU KWA MIAKA MITANO YA KWANZA NA KUNA UWEZEKANO MKUBWA MAGUFULI KM ATACHAGULIWA SASA ASIRUDI TENA KWA AWAMU YA PILI.

TINGATINGA LAZIMA LIONGOZWE LISIPOONGOZWA VIZURI LITALETA MAAFA!
Watanzania tuchague mtu atakayekuwa na maamuzi ya kwake asiyehitaji kuwa na hofu na alifanyalo. na mtuhuyo ni LOWASA pekee! Magufuli hatoshi kabisa kwenye nafasi ya urais!
 
mcfm40

Umesema kweli tupu mkuu.Hapo kwenye kumwongezea elimu ya kimataifa, inatakiwa
pia apewe dozi kali ya diplomasia na miiko yake. Mechanicality aliyo nayo ni hatari
kwa mahusiano ya kimataifa.Ni rahisi sana kwa Magufuli kusema, kwa mfano:
Tanzania is a sovereign state.We will use military option to deal with any country
that interferes with our country!
 
Last edited by a moderator:
Makala yako ni nzuri lakini umeiandika kana kwamba Magufuli anasubiri kuapishwa tu
Yani kama vile hakuna mchakato mwingine mbele yake ambao haiyumkini ndio ukawa mwisho wake na chama chake kuliongoza taifa hili
Msijisahau rais wa nchi hii hachaguliwi na NEC ya ccm anachaguliwa na watanzania wote.
 
Umenena vema mkuu. Ila ni bora kama dereva wake atakuwa mkapa, lakin akiwa Kikwete tumekwisha. Uswahiba hautaisha.
 
Sizani kama Nyerere alikuwa na uzoefu wa mambo ya kitaifa wakati anakuwa raisi wetu pia Nyerere ni kwenye pschology looks like type A kama Magufuri na inchi ilienda.
Na pia Uraisi ni taasisi mapungufu yoyote yake yatakuwa resolved na baraza lake la mawaziri na pia kumbuka ni mtu ambaye anashaulika kama umshaulicho kina mantiki.
Kwa masuala ya Nje kukusaidia tuu yupo Mahiga au Migiro
Mimi kama mimi Tanzania ya sasa twaitaji mtu kama magufuri ili tuweze move ata kama mfumo uliopo ni mbovu bati it takes a man to change that.

NB>Type A" individuals as ambitious, rigidly organized, highly status-conscious, sensitive, impatient, take on more than they can handle, want other people to get to the point, anxious, proactive, and concerned with time management. People with Type A personalities are often high-achieving "workaholics" who multi-task, push themselves with deadlines, and hate both delays and ambivalence.[SUP][4][/SUP] It is therefore understood that "Type A" personalities are suited to smoking as a mechanism for relieving stress.
 
Trimmer uchaguzi ni kweli bado...

Lkn haya maelezeo ya mtoa thread ni kuonyesha tofauti ya kiongozi na mtendaji.
 
Last edited by a moderator:
TINGATINGA LAZIMA LIENDESHWE. LISIPOENDESHWA LITALETA MAAFA!

Hii statement haina mantiki hata kiduchu.
Tingatinga lisipoendeshwa litaletaje maafa??????
kivipi??
Lisipoendeshwa halina hatari yeyote.
Mtu akiitwa Jembe je utamjadili vipi?

Mtasema mengi sana safari hii.



 
Tunahitaji raisi dikteta ambaye anauwezo wa kukemea jambo na watendaji wote wakafyata.

Alikuwepo kikwete milikuwa mnamtukana kuwa n mpole hafuatlii mambo.
Kumbuka upole wa kikwete ndio ulisababisha yakatokea haya richmound, escrow n.k.

Sasa hapa ilitushike adabu lazma magufuli ashike nchi awawajibishe wazembe.

Karibu magogon mzee magufuli.
Naona wala rushwa, wafanyabiashara haramu na mafisadi wanaanza kufarakana.
Mm nakuombea uingie ikulu ili watafutane vzr
 
TINGATINGA LAZIMA LIENDESHWE. LISIPOENDESHWA LITALETA MAAFA!

Hii statement haina mantiki hata kiduchu.
Tingatinga lisipoendeshwa litaletaje maafa??????
kivipi??
Lisipoendeshwa halina hatari yeyote.
Mtu akiitwa Jembe je utamjadili vipi?

Mtasema mengi sana safari hii.




mkuu naona wameanza kujihofia walimwonea mzee wa msata sasa amewajia ngosha wanahaha hawajui wakimbilie wapi.
Hata mabubu sasa hivi naona wanaongea magufuli anatisha
 
Umenena vema mkuu. Ila ni bora kama dereva wake atakuwa mkapa, lakin akiwa Kikwete tumekwisha. Uswahiba hautaisha.

Asili yetu waafrica kudhalau tulichonacho na kujutia kilichopita. Wakati JK anaingia matusi haya alikuwa anapewa Mkapa na kusifiwa mwinyi na vivo hivyo wakati Mkapa anaingia Mwinyi alitukanwa sana... Miafrica Ndivyo Tulivyo
-Nyani Ngabu wa JF
 
Back
Top Bottom