Magufuli ni kweli amekosa watetezi?

Magufuli ni kweli amekosa watetezi?

Blackafrica

Senior Member
Joined
Jun 26, 2021
Posts
140
Reaction score
401
Hata siku moja huwezi kupendwa na watu wote, hii ndio hulka ya wanadamu, inasikitisha sana kuona sasa Magufuli amekosa kabisa watetezi, wale waliokuwa hawampendi na kumchukia, kwa sasa wanajiachia watakavyo kumsema vibaya watakavyo hata mazuri aliyofanya hayaonekani bali ni kumkebehi kumtukana na kumsema vibaya.

Nina Hakika hata angekuwa hai leo, wasingekosekana wa kumsema na kumshtumu vibaya, tofauti ya sasa ambapo huyu mtu hatupo naye kimwili tena ni kwamba hata wale watetezi wake waliokuwa Wanamkubali wamegawanyika wengine wamekaa kimya hawamtetei wala kuwa upande wake, wengine Wanahuzunika na hawaamini kama kweli jembe hayupo na mambo mengi wakitizama hayaendi au yamekwama, lakini hawana sauti ya kupaza labda ni uoga au maslahi wanayokuwa nayo katika ukimya wao, binadamu ni wanafiki sana naamini angekuwepo Magufuli hai, angepata watetezi wengi sana tena watetezi wa hoja zenye nguvu.

Lakini tukubaliane kuwa watanzania wengi wamekata tamaa haswa watanzania wale wa kipato cha kati na cha chini, ukipita kila mkoa utakutana na maneno angekuwepo Magufuli huu mradi ungeisha au hii Barabara ingekuwa imejengwa tayari au hii hospital ingekuwa imefunguliwa tayari au tungekuwa tumepiga maendeleo makubwa sana, kwahiyo tusizibeze hizi sauti zinazolalamika chini chini na hakika hizi sauti zikifika mahali zikaamua ziseme sauti ya juu ili zisikike, ndio utakuwa mwisho wa watawala kutudanganya, uongo una mwisho wake uongo una ukomo wake.

Tusimbeze sana Magufuli bali tuendeleze mazuri yake aliyoacha, mkiendelea kumbeza, mfahamu kuwa watetezi wake wapo tele na siku wakiamua kutetea haki zao na nchi yao mtatafuta mlango wa kutokea.
 
Hata siku moja huwezi kupendwa na watu wote, hii ndio hulka ya wanadamu, inasikitisha sana kuona sasa Magu amekosa kabisa watetezi, wale waliokuwa hawampendi na kumchukia, kwa sasa wanajiachia watakavyo kumsema vibaya watakavyo hata mazuri aliyofanya hayaonekani bali ni kumkebei kumtukana na kumsema vibaya

Nina Hakika hata angekuwa hai leo, wasingekosekana wa kumsema na kumshtumu vibaya, tofauti ya sasa ambapo huyu mtu hatupo naye kimwili tena ni kwamba hata wale watetezi wako waliokuwa Wanamkubali wamegawanyika wengine wamekaa kimya hawamtetei wala kuwa upande wake, wengine Wanahuzunika na hawaamini kama kweli jembe hayupo na mambo mengi wakitizama hayaendi au yamekwama, lkn hawana sauti ya kupaza labda ni uoga au maslahi wanayokuwa nayo katika ukimya wao, binadamu ni wanafiki sana naamini angekuwepo Magu hai, angepata watetezi wengi sana tena watetezi wa hoja zenye nguvu.

Lakini tukubaliane kuwa watanzania wengi wamekata tamaa haswa watanzania wale wa kipato cha kati na cha chini, ukipita kila mkoa utakutana na maneno angekuwepo Magu huu mradi ungeisha au hii Barabara ingekuwa imejengwa tayari au hii hospital ingekuwa imefunguliwa tayari au tungekuwa tumepiga maendeleo makubwa sana, kwahyo tusizibeze hizi sauti zinazolalamika chini chini na hakika hizi sauti zikifika mahari zikaamua ziseme sauti ya juu ili zisikike, ndio utakuwa mwisho wa watawala kutudanganya, uwongo una mwisho wake uwongo una ukomo wake.

Tusimbeze sana Magu bali tuendeleze mazuri yake aliyoacha, mkiendelea kumbeza, mfahamu kuwa watetezi wake wapo tele na siku wakiamua kutetea haki zao na nchi yao mtatafuta mlango was kutokea.

Kazikwe naye ….. nafasi ya lile kaburi ni self contained Bado vyumba vipo.
 
Sasa mtu aliyetangulia mbele ya haki unamtetea kwa maslahi ya nani mkuu.
Sasa hivi anajitetea mwenyewe huko aliko, Cha msingi marehemu huwa hasemwi vibaya , hata Kama kuna mabaya alifanya cha msingi ni kuendelea kumuombea ili muumba ampunguzie adhabu tu kwa mabaya aliyofanya.
 
Wanaomchukia Magufuli👇
-Waliotumbuliwa vyeti fake
-Wafanyakazi hewa
-Wafanyabiashara wakwepa kulipa kodi
-Viongozi waliokuwa madarakani wakatumbuliwa
-Wezi waliokuwa wakijinufaisha na uongozi wa awamu zilizopita
-Matajiri waliokuwa wakijinufaisha na nchi bila taratibu
-Mabeberu wapenda dezo za taifa
-Wezi waliotaka JPM nae aungane nao ili waibe wote
 
Sasa mtu alivetangulia mbele ya haki unamtetea kwa maslahi ya nani mkuu ,
Sasa hivi anajitetea mwenyewe huko aliko, Chamasingi marehemu hua hasemwi vibaya , hata Kama kuna mabaya alifanya cha msingi ni kuendelea kumuombea , ili muumba ampunguzie adhabu tu kwa mabaya aliyofanya .
Kama kusemwa angekuwa anasemwa huko aliko hoja yako ingekuwa na mashiko, ila anasemwa hapa Tanzania na yeye hayupo basi wenye kumtetea wamtetee.
 
Wanaomchukia magufuli
-waliotumbuliwa vyeti fake
-wafanyakazi hewa
-wafanyabiashara wakwepa kulipa kodi
-viongozi waliokuwa madarakani wakatumbuliwa
-wezi waliokuwa wakijinufaisha na uongozi wa awamu zilizopita
-Matajiri waliokuwa wakijinufaisha na nchi bila taratibu
-mabeberu wapenda dezo za taifa
-wezi waliotaka jpm nae aungane nao ili waibe wote
Simo kwenye hiyo list ila huyo mzee sitaki hata kumsikia
 
Wanaomchukia magufuli
-waliotumbuliwa vyeti fake
-wafanyakazi hewa
-wafanyabiashara wakwepa kulipa kodi
-viongozi waliokuwa madarakani wakatumbuliwa
-wezi waliokuwa wakijinufaisha na uongozi wa awamu zilizopita
-Matajiri waliokuwa wakijinufaisha na nchi bila taratibu
-mabeberu wapenda dezo za taifa
-wezi waliotaka jpm nae aungane nao ili waibe wote
Wale ndugu zao waliouwawa maiti zao hazikupatikana teena

Wale waliobomolewa nyumba zao kwa kigezo hawakumpigia kula ila wengine wakaachiwa sababu walimpigia kura

Ndoto za vijana wengi walioota wasomee ualimu na Udaktari kuzikomboa familia zao ambae yeye akaaminisha taaluma zimejitosheleza wakajiajiri huku wanae na watu wa circle yake wakila mema ya nchi

Wale waliotukanwa na kuvunjiwa heshima na kuwekwa ndani bila kosa lolote mbele ya Televisheni

Wale watanzania waliokufa kwa Covid-19 baada ya yeye kama kiongozi akikataa hatua za kujilinda wakati huo yeye kaenda zake Chato kuji- Quarantine

Ana Mazuri yake lakini ana wale kawapa majeraha ya kutosha

Sent from my SM-A032F using JamiiForums mobile app
 
Wanaomchukia magufuli
-waliotumbuliwa vyeti fake
-wafanyakazi hewa
-wafanyabiashara wakwepa kulipa kodi
-viongozi waliokuwa madarakani wakatumbuliwa
-wezi waliokuwa wakijinufaisha na uongozi wa awamu zilizopita
-Matajiri waliokuwa wakijinufaisha na nchi bila taratibu
-mabeberu wapenda dezo za taifa
-wezi waliotaka jpm nae aungane nao ili waibe wote

Tunamshukuru Mungu kwa kutuondolea yule kiongozi muovu bila damu kumwagika.
 
Kama kusemwa angekuwa anasemwa huko aliko hoja yako ingekuwa na mashiko, ila anasemwa hapa Tanzania nayeye hayupo basi wenye kumtetea wamtetee
Haya mtetee basi, maana hakuna aliyekatazwa kumtetea
 
Acheni kukuza hakuna utawala nchi hii ambao haujaumiza watu, punguzeni kujiliza.
Tutajie mtawala aliyefikia hadi hatua ya kujifananisha na Malaika.

Akifika huko ataongoza Malaika.
Hakukuwa na utawala wa sheria Wala kanuni achilia mbali misingi ya haki.

Watu walitekwa na kuuwawa si kwa kificho
Vikundi vya watu wasiojulikana walitamalaki.
Maiti ziliokotwa kwenye viroba na watu walipo hoji wakaambiwa ni wahamiaji haramu.
Je Wana haki ya kuuwawa?

Hofu ilitanda kila sehemu, sio mitaani Wala kwenye miji.
Watu wachache wakajitwalia ukwasi wa kutisha na wengi wakafuata mkumbo.

Miradi haikufuata sheria ya fedha ya mwaka husika yaani appropriation act ila ikawa one man's show.

Ajira hazikutolewa kiasi Cha kupoteza na kutweza Vijana wa nchi hii.
Mfumo wa Biashara uliyumba maana waliokuwa na fedha basi waliwajua Financial Intelligence Unit

Mfumo wa uchumi ulianguka mpaka mabenki kufilisika.
Purchasing power kwa Mtanzania mmoja mmoja ilianguka kiasi Cha kushindwa wabongo kumudu Milo mitatu.

Kutumika nguvu kubwa kwenye ukusanyaji wa mapato na kubambikiwa watu Kodi kubwa kubwa zisizo na uhalisia.

Kudhalilisha kundi la wasomi na taaluma mbalimbali kwa wanasiasa wanaojifanya kujua kila kitu.

Kuminywa na kutozingatiwa kwa stahiki na maslahi ya Wafanyakazi wa nchi hii ikiwemo kutopandishwa kwa mishahara kwa miaka yote alipoongoza.

Kuharibiwa kwa bodi ya mikopo ya elimu ya juu, kiasi Cha watoto wengi wa familia fukara kushindwa kuendelea na masomo.

Biashara za mazao kufa kipindi chake, chukua tukio la Korosho za Mtwara na Lindi.
Zao la Ufuta
Kilimo Cha mahindi kule Sumbawanga, Nyanya pale Iringa

Kifupi hakuwa na jema ila jiulize kwa nini waliipenda force account itumike kwenye miradi ambayo haikuidhinishwa na Bunge?

Kwa nini walimdisicredit report ya CAG na kazi yake?

Kwa nini hawakutumia Competitive tendering kwenye kupata mzabuni wa Ile miradi?

Kwa nini waliotumika chini yake Vijana wakawa matajiri ghafra?

Kwa nini alidharau Wazee kama mzee Warioba na Wastahafu wengine?
 
Hata siku moja huwezi kupendwa na watu wote, hii ndio hulka ya wanadamu, inasikitisha sana kuona sasa Magu amekosa kabisa watetezi, wale waliokuwa hawampendi na kumchukia, kwa sasa wanajiachia watakavyo kumsema vibaya watakavyo hata mazuri aliyofanya hayaonekani bali ni kumkebei kumtukana na kumsema vibaya

Nina Hakika hata angekuwa hai leo, wasingekosekana wa kumsema na kumshtumu vibaya, tofauti ya sasa ambapo huyu mtu hatupo naye kimwili tena ni kwamba hata wale watetezi wako waliokuwa Wanamkubali wamegawanyika wengine wamekaa kimya hawamtetei wala kuwa upande wake, wengine Wanahuzunika na hawaamini kama kweli jembe hayupo na mambo mengi wakitizama hayaendi au yamekwama, lkn hawana sauti ya kupaza labda ni uoga au maslahi wanayokuwa nayo katika ukimya wao, binadamu ni wanafiki sana naamini angekuwepo Magu hai, angepata watetezi wengi sana tena watetezi wa hoja zenye nguvu.

Lakini tukubaliane kuwa watanzania wengi wamekata tamaa haswa watanzania wale wa kipato cha kati na cha chini, ukipita kila mkoa utakutana na maneno angekuwepo Magu huu mradi ungeisha au hii Barabara ingekuwa imejengwa tayari au hii hospital ingekuwa imefunguliwa tayari au tungekuwa tumepiga maendeleo makubwa sana, kwahyo tusizibeze hizi sauti zinazolalamika chini chini na hakika hizi sauti zikifika mahari zikaamua ziseme sauti ya juu ili zisikike, ndio utakuwa mwisho wa watawala kutudanganya, uwongo una mwisho wake uwongo una ukomo wake.

Tusimbeze sana Magu bali tuendeleze mazuri yake aliyoacha, mkiendelea kumbeza, mfahamu kuwa watetezi wake wapo tele na siku wakiamua kutetea haki zao na nchi yao mtatafuta mlango was kutokea.
Watetezi wake walikuwa kwenye payroll yake... Payroll yake kazikwa nayo una lingine?
 
Back
Top Bottom