Filipo Lubua
JF-Expert Member
- Nov 18, 2011
- 339
- 578
Nawasilisha
Mkuu, kuna Ukweli na upotoshaji fulani ulivyorejesha, alichosema Magufuli ni kuwa kandarasi huyo atakapoanza Kazi barabara itafungwa lakini Kwa sasa huwezi funga Kwa vile hakuna kitu kilichofanyika kama ilivyokuwa inasadikika!
My take: Imekuwaje Mkandarasi huyo kalipwa boll join nane wakati hajazalisha kitu?? Navyojua ukifanya Kazi unaandaa certificate kuomba fedha against progress/production - sasa huyu imekaaje??? Hii ndo bongo land!
Wanajamii,
Nimeshangazwa na taarifa ya Star TV ikimuonyesha Dk. Magufuli akitoa msimamo wake juu ya amri ya kufungwa kwa barabara inayodaiwa kuzuia ujenzi wa Uwanja wa Ndege wa Mwanza. Kwa maelezo yake Magufuli, uwanja huo si kikwazo kama ilivyoelezwa na mkandarasi, maana hata upembuzi yakinifu wa ujenzi wa uwanja huo, hadi sasa ni asilimia thelathini na tano (35%) tu na imeshachelewa miezi minne zaidi. Magufuli ameiagiza wizara ya Uchukuzi imbane mkandarasi na si kuagiza barabara ifungwe.
Wakati huohuo, siku Waziri wa Uchukuzi alizoipa Wizara ya Ujenzi kuifunga barabara hiyo zimebakia nne tu. Dk. Harrison Mwakyembe ametoa kauli yake kuwa kesho itabidi tu agombane kabisa na Dk. Magufuli kwa ajili ya swala hilo.
Wanajamii, hii serikali inatupeleka wapi ikiwa wizara mbili za serikali moja zinatunishiana misuli na kuoneshana ubabe? Kweli kwa misingi hii tutayapata maendeleo?
Nawasilisha
Nashukuru kwa correction Mkuu. Ila sasa, kwa nini Mwakyembe naye anasema anataka kugombana na Magufuli kwa swala hilo? Naona hawa watu wanatofautiana katika maelezo yao
Nashukuru kwa correction Mkuu. Ila sasa, kwa nini Mwakyembe naye anasema anataka kugombana na Magufuli kwa swala hilo? Naona hawa watu wanatofautiana katika maelezo yao
Acha upotoshaji Ukweli ni huu:
1.Mkandarasi kasaini contract June 2012 (miezi nane tayari) mobilisation zero au suturing or 0%
2.Mhandisi Mshauri kutoka Gambia kakiri mbele ya Waziri Magufuli kuwa Mkandarasi hajafanya kitu tangu apewe mradi!
3.Magufuli kajionea Kwa macho yake pale uwanja Wa ndege Mwanza hata jembe la kupalilia site halipo?
4. Tayari Magufuli keshapata njia mbadala ambayo inatokea Nyakato kupitia Buswelu itakayotumika pindi hii ya airport itakapofungwa ( zote hizi jitihada kumaliza tatitizo)
5. Juzi Tabora Magufuli na Mwakyembe wameonekana wakiwa pamoja na raisi na hawana mgogoro wowote na ikumbukwe wamewahi fanya Kazi Pamoja hivyo wanajua wanachokifanya!
6. Ifike sehemu tuache uchonganishi Wa kihuni, tuwape moyo japo hawa wanaonyesha kufanya Kazi na segment kubwa ya watanzania inawakubali
Asante mkuu kwa uchambuzi makini.Acha upotoshaji Ukweli ni huu: