Magufuli: Mwaka 2020 uwe wa kujenga umoja

Bagamoyo

Platinum Member
Joined
Jan 14, 2010
Posts
30,057
Reaction score
34,212
Mh. John Pombe Joseph Magufuli Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania akiwa Chato katika misa siku ya Jumapili ya nne ya Majilio kuelekea Krismas na mwaka mpya, atoa ujumbe wa kipekee kwa wana Chato na Watanzania na kuwatakia sikukuu ya Krismas njema na Mwaka Mpya wa mafanikio, kujenga umoja wetu Watanzania wote, uwe mwaka mpya wa upendo na amani kwa Watanzania wote.

Source: MCL Digital
 
Huwezi kujenga umoja kama wasiojulikana wataendelea kuwepo na kupewa nguvu.

Huwezi kujenga umoja kama watu wataendelea kubambikiwa kesi za uhujumu uchumi na utakatishaji fedha.

Huwezi kujenga umoja kama watu wataendelea kutazamwa kikanda.

Huwezi kujenga umoja kama Polisi, mahakama na Bunge vitaendelea kutumika kama vyombo vya watu binafsi na CCM.

Huwezi kujenga umoja kama maDC na maRC wataendelea kuwaweka watu korokoroni kwa ubabe, uonevu na kukomoana.

Huwezi kujenga umoja kama utaendelea kuwaona wasio wanaCCM ni raia daraja la pili.

Huwezi kujenga umoja kama Polisi wataendelea kufanya kazi kama kikundi cha kigaidi. Kazi kubwa ya magaidi ni kujenga hofu. Leo polisi badala ya kuwakamata watuhumiwa, wanawateka watuhumiwa. Polisi wamebakia na kazi ya kuwaziba watu na kuwanyima watu haki zao za kikatiba.

Umoja wa kitaifa hauji kwa kauli bali kwa matendo. Mazuri mengi tuliyokuwa nayo zamani, yaliyokuwa yakilitambulisha Taifa letu yamevurugwa awamu hii. Kama hili limegundulika sasa, na kuna dhamira ya kuliondoa, ianze kufanyika kazi katika hayo niliyoyataja. Bila hivyo umoja wetu utaendelea kutetereka zaidi na zaidi, na uchaguzi wa mwakani utaongezea maradufu.
 
Ni utapeli tu maneno hayo angeyasemea arusha na kilimanjaro kulikojeruhiwa walau yangeleta maana.Upendo huanza na yeye kuwapenda watanzania wote bila kubagua na sii maneno ya kinywani pekee, afanye kwa vitendo
Huwezi kujenga umoja kama wasiojulikana wataendelea kuwepo na kupewa nguvu.

Huwezi kujenga umoja kama watu wataendelea kubambikiwa kesi za uhujumu uchumi na utakatishaji fedha.

Huwezi kujenga umoja kama watu wataendelea kutazamwa kikanda.

Huwezi kujenga umoja kama Polisi, mahakama na Bunge vitaendelea kutumika kama vyombo vya watu binafsi na CCM.

Huwezi kujenga umoja kama maDC na maRC wataendelea kuwaweka watu korokoroni kwa ubabe, uonevu na kukomoana.

Huwezi kujenga umoja kama utaendelea kuwaona wasio wanaCCM ni raia daraja la pili.

Huwezi kujenga umoja kama Polisi wataendelea kufanya kazi kama kikundi cha kigaidi. Kazi kubwa ya magaidi ni kujenga hofu. Leo polisi badala ya kuwakamata watuhumiwa, wanawateka watuhumiwa. Polisi wamebakia na kazi ya kuwaziba watu na kuwanyima watu haki zao za kikatiba.

Umoja wa kitaifa hauji kwa kauli bali kwa matendo. Mazuri mengi tuliyokuwa nayo zamani, yaliyokuwa yakilitambulisha Taifa letu yamevurugwa awamu hii. Kama hili limegundulika sasa, na kuna dhamira ya kuliondoa, ianze kufanyika kazi katika hayo niliyoyataja. Bila hivyo umoja wetu utaendelea kutetereka zaidi na zaidi, na uchaguzi wa mwakani utaongezea maradufu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Maneno mazuri ya faraja kutoka kwa JPM, inawezekana yeye ana nia nzuri ila wasaidizi wake ndio wanamuangusha, sasa ngoja tusubiri tuone kwenye utekelezaji.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
"Wakati huo Kabendera anaenda kula crismas akiwa jela kwa kesi yenye mkono wake"
 
Back
Top Bottom