Magufuli mpe kamishna generali mpya wa magereza pesa ya kutosha kibajeti ili akufanikishie unachokihitaji vinginenevyo unatwanga maji kwenye kinu

Mishenyi

JF-Expert Member
Oct 6, 2019
464
748
Miradi inafanikishwa na pesa,molari kwa askari anaoenda kuwaongoza italetwa na maslahi yao kufikiriwa vizuri.
Angalau nimekuwa katika kufatilia utekelezaji wa bajeti kimsingi Magereza unawaonea bure pamoja na kwamba wana mapungufu yao kama zilivyo taasisi nyngine za kijeshi na kiraia ila pesa mnayowapa ni ndogo sana.

Jana nimeshangaa kukuta bajeti ya magereza mpaka sasa imetekelezwa kwa %36 tu wakati nimeangalia JWTZ bajeti yao inaelekea %78 sasa hapa lazima mmoja anafanya vizuri na mwingine vibaya hata huyu br.gen usipompa pesa sahau matokeo mazuri utamlaumu tu we mpe hela alafu mdai matokeo.

Hilo jeshi si la askari magereza bali ni la watanzania linapofeli watz wanakuwa wamefeli hebu Mh. Lifikirie kwa kina hilo jeshi kama ukiwekeza vizuri huko utapata faida kubwa mno maana kuna nguvu kazi isiyohitaji mshahara(wafungwa) kaa na general mpya mlikwamue hilo jeshi mtapata matokeo makubwa.

Kuhusu mafunzo ya askari magereza sina wasiwasi kabisa wako vizuri sana bali tu wape kozi mbali mbali za Ku refresh kama ilivo kwa JWTZ.
 
Jeshi la magereza askari wake wamekata tamaa kabisa maana hawaheshimiwi kwa viwango vyao vya elimu.
Unakuta askari aliingizwa miaka minne iliyopita kama Warder akiwa na shahada ya chuo kikuu lakini analipwa na kufanya kazi za kuswaga wafungwa kama yule aliyeingia na cheti cha kidato cha nne.
Hapo moyo na ubunifu utatoka wapi? Wenye maamuzi ndani ya jeshi ni wale wa zamani ambao wengine ni darasa la sana au FF waliojiendeleza na sasa hawataki kabisa kuwaona wasomi wamatumia taaluma zao ndani ya jeshi tofauti kabisa na JWTZ au Polisi.
Bila kuliangalia hilo jeshi litabaki la kizamani hadi utawala wenye akili uingie madarakani.
Mtu ana shahada ya sheria au mhandisi mnamdharau? Wanafanya kazi magereza kwa vile hakuna sehemu nyingine tuu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ku husu maslahi wanakomoana wao wenyewe Kuna afisa utumishi wao pale makao anaitwa ssp Nyombi anaingiza allowances kwa watu wake wa karibu ni mshenzi kawaharibia wengi. Inasemekana yeye ndio Kila kitu kaharibu mfumo wa malipo kabisa
 
SIO KUTOA PESA TU PIA MASLAI YA ASKARI YAANGALIWE KAMA POSHO YA MAJI UMEME PANGO YA NYUMBA
LAKINI WAZINGATIE WASOMI NDANI YA JESHI USUSAN HATA KATIKA KUTOA MAWAZO CHANYA YA KULUPELWKA JESH MBELE TUWAPE NGUVU ASKAR WA CHINI KUELEZA CHANGAMOTO PILI JESHI ZIFANYIE KAZI CHANGAMOTO HIZO PIA KUWE NA USAWA NA JESHI LA POLISI KWANI WAO NA MAGEREZA NI WIZARA MOJA LAKIN KUNA UTOFAUT MKUBWA NAMNA WANAVYOSHUGHULIKIA MASLAHI YA WASOMI KATI YA MAJEZH HAYA MAWILI

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Jeshi la Magereza linajidharalisha lenyewe pia. Mafano, Jeshi likikuwa na mradi wa kutengeneza Viatu vya Ngozi katika Gereza la Karanga -Moshi , uzalishaji ukapungua. Serikali imetoa hela kupitia Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma lakini ujenzi wa kiwanda unasuasua licha ya fedha kutolewa! Ndiyo maana Mkuu wa Nchi anauliza kuna tatizo gani wakati Jeshi lina rasimali watu (wafungwa), kwa nini hwatumiki kusaidia ujenzi kama wanavyotumika katika kilimo na ufugaji! Ki ukweli kama Jeshi hili lingetumia vizuri lingekuwa na matokeo chanya nyuma ya JKT. Jeshi hili lina miradi ya kilimo, ufugaji, samani, kutengeneza viatu, ushaonaji na ufutuaji wa tofali.
 
Raisi huwa hatoi hela! raisi siyo mtoa hela!! Jifunze jinsi nchi yako huwa inaendeshwa!!
Alitoa 10bil wakakaa nazo mwaka mzima bila hata kuchimba msingi, zile nyumba wamekabidhiwa wameshindwa hata kuingia maji ndani, hata kufanya leveling. Poor magereza watawaliwe na jeshi tuuu
 
Back
Top Bottom