mama chupaki
JF-Expert Member
- Aug 23, 2015
- 940
- 768
Jamaa sijui analala usingizi au anakesha kwa kasi hii ya JPJM maana JK aliomba tumkichagua Magufuli atalala usingizi.
Ni vile katiba hairuhusu mgombea binafsi lakini Lowassa baada ya kukatwa na CCM asingekwenda UKAWA angegombea kama mgombea binafsi. JPM ni mgombea binafsi aliyewahadaa CCM wakadhani na wachache wanadhani ni mwenzao.
Wahafidhina wa CCM mpaka leo wanajuta kupitishwa kwa jina lake.kwenye kampeni alikwepa kutamka neno CCM kwa kadri alivyoweza na sasa anakwepa ilani ya CCM, na wafanyabiashara wa CCM kwa kadri anavyoweza.
Kama kuna mtu anadhani JPM yuko upande wa CCM unajidanganya. CCM ilikufa siku Lowassa alipokatwa na JK.J PM akijiuzuru leo serikali itakayokuja itafuata nyayo za JK na watangulizi wake kwani huo ndio utamaduni wao.
Hii ni serikali ya Magufuli, si serikali ya CCM kama tulivyozoeshwa
Ni vile katiba hairuhusu mgombea binafsi lakini Lowassa baada ya kukatwa na CCM asingekwenda UKAWA angegombea kama mgombea binafsi. JPM ni mgombea binafsi aliyewahadaa CCM wakadhani na wachache wanadhani ni mwenzao.
Wahafidhina wa CCM mpaka leo wanajuta kupitishwa kwa jina lake.kwenye kampeni alikwepa kutamka neno CCM kwa kadri alivyoweza na sasa anakwepa ilani ya CCM, na wafanyabiashara wa CCM kwa kadri anavyoweza.
Kama kuna mtu anadhani JPM yuko upande wa CCM unajidanganya. CCM ilikufa siku Lowassa alipokatwa na JK.J PM akijiuzuru leo serikali itakayokuja itafuata nyayo za JK na watangulizi wake kwani huo ndio utamaduni wao.
tuko pamoja. hii ni danganya toto. kama magu aliingia kwa uchakachiz na wale waliochakachua ndio wapga dili bandarini na tra, je jpm si atazma kama kibatari?hii ni comedy na kama si usanii aguse epa,escrow, tanapa, kagoda na richmond
Ni vile katiba hairuhusu mgombea binafsi lakini Lowassa baada ya kukatwa na CCM asingekwenda UKAWA angegombea kama mgombea binafsi. JPM ni mgombea binafsi aliyewahadaa CCM wakadhani na wachache wanadhani ni mwenzao.
Wahafidhina wa CCM mpaka leo wanajuta kupitishwa kwa jina lake.kwenye kampeni alikwepa kutamka neno CCM kwa kadri alivyoweza na sasa anakwepa ilani ya CCM, na wafanyabiashara wa CCM kwa kadri anavyoweza.
Kama kuna mtu anadhani JPM yuko upande wa CCM unajidanganya. CCM ilikufa siku Lowassa alipokatwa na JK.J PM akijiuzuru leo serikali itakayokuja itafuata nyayo za JK na watangulizi wake kwani huo ndio utamaduni wao.
Ni vile katiba hairuhusu mgombea binafsi lakini Lowassa baada ya kukatwa na CCM asingekwenda UKAWA angegombea kama mgombea binafsi. JPM ni mgombea binafsi aliyewahadaa CCM wakadhani na wachache wanadhani ni mwenzao.
Wahafidhina wa CCM mpaka leo wanajuta kupitishwa kwa jina lake.kwenye kampeni alikwepa kutamka neno CCM kwa kadri alivyoweza na sasa anakwepa ilani ya CCM, na wafanyabiashara wa CCM kwa kadri anavyoweza.
Kama kuna mtu anadhani JPM yuko upande wa CCM unajidanganya. CCM ilikufa siku Lowassa alipokatwa na JK.J PM akijiuzuru leo serikali itakayokuja itafuata nyayo za JK na watangulizi wake kwani huo ndio utamaduni wao.
JPM kawekwa na kitengotuachieni jpm wetu. mbona mnamdandia wakati kura mlimnyima na kumpa fisadi. nyie kazungusheni mikono huku mkipayuka- lowasaa fisadiii, fisadiii lowasaaa.
.
Watanzania wengi hawana kumbukumbu au kutokana na uhaba wa vyombo vya habari miaka iliyopita basi wengi walikua hawana fursa ya kupata habari au taarifa za mambo yaliyokua yanatokea.
Ndio maana wengi wanafikiri kuwa ufisadi umeletwa na Kikwete au Magufuli ndiye pekee aliyeanza urais kwa speed kubwa.
Nadhani pia wengi wanaoshangilia na kuruka ruka kama mazuzu ni vijana wa CCM wenye umri chini ya miaka 30.Hawa uchaguzi huu ndio uchaguzi wao wa kwanza na ni kipindi chao cha kwanza cha kufuatilia mambo ya historia.
Tukumbuke tu kuwa baada ya uhuru Nyerere alikuja na kasi kubwa na Matumaini Makubwa kwa wananchi. Chini ya sera za Ujamaa na kujitegemea.
Maadui zake ambao walikua ndio wakoloni alifanikiwa kuwaangusha kabisa na kuwaondosha kwenye ulingo wa kiuchumi na kisiasa.
Akaweka safu ya wakoloni weusi chini ya TANU na hatimaye CCM. Jambo alilolikwepa ndilo lililomwangusha na kuiporomosha sera yake ya Ujamaa na kujitegemea.Sio jambo lingine bali ni kuweka katiba ambayo ingiheshimiwa na watu wote na kumwajibisha mtu yeyote bila kujali madaraka yake.
Kutokuwekwa kwa kifungu ndani ya katiba cha kumfikisha rais mahakamani kuanzia uteuzi wake na awapo madarakani endapo atakiuka miiko ya uongozi lilikua na litaendelea kuwa jambo baya sana kwa mustakabali wa nchi yetu.
Nyerere aliwaamini wazawa na kuwakabidhi kila kitu wasimamiwa walishindwa kila kitu isipokuwa kuimarisha chama na kukifanya kuwa ni genge la wajanja kupata madaraka na maisha bora. Ni bora mtu afilisi kiwanda au kampuni au shirika la umma kuliko kukikosoa chama wazi wazi.
Ukikiuka sera za chama ulikua unadukuzwa hapo hapo lakini ukiibia shirika la umma ulikua unahamishwa tu na kupewa majukumu mengine alimradi uwe mwanachama wa chama dola. Nyerere pamoja na nia yake njema na speedi aliyoanza nayo alishindwa vibaya kutokana na kukumbatia maslahi ya chama kuliko maslahi ya Taifa. Hali hii iliwafanya wezi wote na wababaishaji kujificha chini ya ngome imara ya CCM. Yeyote aliyekua nje au aliyeipinga CCM hata kwa nia njema alionekana adui na asiyelitakia mema taifa letu. Hali hii ilijenga taifa la wanafiki wanotenda kile wasichokiamini. Waoga wa kukosoa hata pale kiongozi anapokose. Kazi yao ni kusifia na kupiga makofi tu.
Hawa ndio wazazi wa wanafiki wengi waliojazana nchi nzima kusifia kila jambo hata lile linaloonekana kuwa linafanywa kwa kukurupuka pasipokuwa na malengo ya kudumu.
Nyerere alikaa madarakani zaidi ya miongo miwili na huku hali ya nchi ikiporomoka kwenye sekta zote; elimu,afya,viwanda,mipango miji,kilimo cha kibiashara, nidhamu ya kiuchumi na kimaadili n.k.
Hali hii ilisababishwa na watu wake wa karibu aliowaamini kuishi kwa kujenga hofu ya kile lisichojulikana juu ya watanzania wenzao. Na kuishia kukumbatia katiba na sheria za mkoloni. Jeshi la polisi likaendelea kuwa la kikoloni. Sheria zikaendelea kuwa za kikoloni ma kuandikwa kwa lugha ya kikoloni.Sheria za ardhi na sheria za kazi pia zikabakia zile za mkoloni. Kilichobadilika ni rangi za watawala. Kutoka wakoloni weupe na kuwa wakoloni weusi.
Nyerere kwa utu na ubinadamu wake akashindwa kufikia ndoto zake kutokana na mfumo wa katiba ya nchi kushindwa kuweka dira na miiko kwa watawala.
Mwinyi alipokuja mwaka 1985 alikuja na kasi kama hii ya Magufuli tofauti yake ni kwamba alipokea taifa likiwa na umaskini mkubwa ,miundo mbinu haikuwa mizuri kwenye nyanja zote za kiuchumi.
Wananchi na serikali yao wate walikua maskini sana japo nchi ilikua na utajiri mkubwa wa rasilimali za asili.
Mwinyi alianza na kile alichokiita FAGIO LA CHUMA kwa wala rushwa na wahujumu uchumi.
Watu walifagiliwa na kutupwa nje bila huruma. Mwinyi akasifiwa kila pande za nchi na kuitwa mkombozu wa wanyonge. Waliokuwepo enzi hizo watakumbuka . Nyimbo ziliimbwa za kila namna za kumpamba kwa kila neno zuri.
Kasi yake iliporomoka baada tu ya kuchambua na kuwaweka madarakani watu aliowaamini. Mpaka leo hakuna aliyejua kuwa ni nani alisababisha mkwamo kwenye awamu ya pili. Ni rais Mwinyi au watendaji wake. Jibu la uhakika ni mfumo haukuwa na sheria kali kwa viongozi wa juu wawapo madarakani na wanapotoka.
Mwinyi naye akaondoka madarakani kimya kimya huku akiwa amesheheni mali na marafiki wa kibepari toka kona zote za dunia. Hakuna sheria iliyomdhibiti asijilimbikizie mali. Kila alichosema na kuamua kilishangiliwa na kupigiwa makofi hata kama alikosea.
Azimio la Arusha lilizimwa ghafla bila hata kutetewa na wale walioliamini na kulipigia makofi kwa miaka zaidi ya 20. Wale wale waliolisifu ndio waliolifuta. Huu ulikua ni unafiki unaoendelea mpaka leo.
Kasi ya Mwinyi ilipotea kwa kuwa haikua kikatiba bali ni utashi wake tu . Wezi waliokua wamemzunguka walimsifu na kumdanganya kuwa katiba iliyokuwepo ilikua na maslahi mapana kwa nchi kumbe ilikua ni maslahi yao na familia zao tu.
Akaja Mkapa kwa kasi kubwa ya kupunguza wafanyakazi na kuajiri wasomi.
Chini ya mfumo na katiba isiyowabana watawala aliishia kutengeneza kikundi cha watu waliokuwa wamejimilikisha kila walichoona kinawafaa.
Hawa wakamsifu kwa kila wimbo.
Mkapa kama watangulizi wake aliendelea kukumbatia katiba na sheria za kikoloni. Watendaji wake wakatumia mwanya huo kujineemesha na mwishowe wote wakaanguka kwenye tamaa ya mali kwani hakuna sheria iliyokua inambana kama mkuu wa nchi. Halikuwa kosa lake bali mfumo aliopewa autumie kuongoza ndio ulioruhusu.
Viongozi walikula na kusaza huku wananchi wakiwa wanashangilia kwa kile kidogo walichokua wanaokota kwani wanaona kama ni huruma tu na hawastahili kudai haki zao kama binadamu wengine.
Awamu ya Kikwete nayo ilianza kwa Nguvu Mpya ,Ari mpya na Kasi Mpya.
Miaka miwili ya mwanzo Speed ya serikali ya JK chini ya Waziri wake mkuu wakati huo Edward Lowasa. Tukiwatendea haki hawa wawili walianza kwa kasi kubwa sana.
Huko Bandarini watu walitimuliwa sana .
Kosa lililofanyika ni kwa mheshimiwa rais kutaka kumfurahisha kila kada wa chama.
Alitaka kukifurahisha chama na makada wake .Aliona ni bora kuua taifa kuliko kuua chama chake. Kikwazo kikubwa cha wezi waliojiandaa kujinufasha kupitia chama walikua wanamhofia Lowasa. Kikwazo kikubwa kilipoondolewa basi shamba la bibi likakosa msimamizi.
Mfumo ukashindwa Kuwaongoza kuwadhibiti katika kutetea maslahi ya umma. Baada ya kumtimua Lowasa kwenye uwaziri mkuu wapigaji wakamdanganya Jk kuwa sasa hali ni shwari na mambo yanakwenda vizuri hakuna wizi wala ufisadi tena hivyo rais alale tu na kusafiri kwa amani kabisa.
Ukatengenezwa mtandao wa mali tu. Hapa mali tu!! Biashara zote zinafanywa na kundi moja. Madini yupo,mafuta yupo,mahoteli yupo,malori yupo,mabasi yupo,siasa yupo,madawa yupo na mashamba yupo.
Tatizo ni nini Katiba haikuwabana viongozi.
Sasa Dr. Mafuli ameanza vyema kama walivyokuwa wameanza watangulizi wake.
Ushauri wangu kwake afanye marekebisho ya katiba au alete katiba ya Warioba ili atumbue Majipu kwa kusimamia katiba na maslahi ya wengi. Viongozi wawe watumishi tu wa watu na sio miungu watu.
Vyeo kama wakuu wa wilaya na mikoa havina tija yoyote kwa mfumo wetu wenye wawakilishi wa majimbo. Wakuu wa mikoa hawana baraza lolote la kutunga hata sheria ndogo. Wanasimamia nini sasa hawa zaidi ya kuimarisha chama chao huku wakifilisi nchi kwa matumizi yao.
Bila katiba inayowabana viongozi kasi ya magufuli itashuka kwani nchi inaongozwa kwa misingi ya sheria na sio matakwa ya mtu.