Magufuli - Mbunge Machemuri muongo

Magufuli punguza mdomo baba ona unavyoumbuka. Hadi kuhonga mabinti nyumba za serkali? Hii kitu si mara moja kuisikia. Niliickia mwaka jana nikiwa versty moja za Tumaini nikajisemea aah mambo za wasomi wachanga. Pia kwamba hata binti yake aliefariki kisa alikosa matibabu effectively ya maralia "very stupid" na hii huwa inawakumba wanandoa wanaoendekeza uzinzi. Ila huwa napata shida kidogo ni kwanini haya mambo huwa yanaibuka wanapokuwa wamewaguswa viongozi wa cdm? Kwamba wananchi wamewachoka viongozi walioko madarakani? Je habari hizo ni za ukweli? Vilevile napata picha kuwa watu wanafahamu sana viongozi wao kuliko wanavyofikiri. Basi ni vyema wawe wanapitia jf na wakachkua hatua. Na wafanye kazi na waache siasa za majukwaani watu wengi sasa hivi wanawachora tu hata wa vijijini.
 
Weweeee Magufuli, Nakushangaa una PHD ila umeweka akili pembeni unatumia akili za DR. DR DR Vasco Da gama.

Magufuli soma alama za nyakati, wananchi wa sasa hawadanganyiki tena.

Hivi CCM inayopesa za kujenga barabara, CCM inafanya biashara gani?

Barabara za Tanzania na Vivuko, meli vyoote vinajenga na kununuliwa na Kodi za watanzania.

Pamba ...fuuu kabisa. Komeniiii kuwadanganya wananchi


Magufuli ni msanii kama CCM, hakuna msafi CCM.

uchumi umeporomoka, bei za bidhaa muhimu zimepanda, mbona wewe magufuli na rais wako kimya??
 
Tetesi zinasema kwamba Mh. Pombe anaandaliwa kuchukua nchi 2015 baada ya Magamba na Sita kuonekana wanakiua chama. From now mpaka 2015 lazima atakuwa anaongea sana kumfurahisha mwenye kigoda. Mh ila ninawasiwasi na uchaguzi wa magamba mwakani maana inaonekana magamba wakuu wanataka kuweka mwenyekiti mpya.
To be honest ze magambas wako very complicated hata Ampiclox haziwezi kuwatibu.
 
Magufuli akienda UKEREWE kukanusha propodanda za kisiasa aende kwa HELA YA CCM kama ni serikali ina watendaji wa kutosha hapo ukerewe wanaweza kukanusha, kwa UKEREWE hakuna OFISI za TANROAD, viongozi popo kama hawa ndio wametufikisha hapa, anapiga siasa badala kufanyakazi zake za kiwaziri
 
Tetesi zinasema kwamba Mh. Pombe anaandaliwa kuchukua nchi 2015 baada ya Magamba na Sita kuonekana wanakiua chama. From now mpaka 2015 lazima atakuwa anaongea sana kumfurahisha mwenye kigoda. Mh ila ninawasiwasi na uchaguzi wa magamba mwakani maana inaonekana magamba wakuu wanataka kuweka mwenyekiti mpya.
To be honest ze magambas wako very complicated hata Ampiclox haziwezi kuwatibu.

RED
kama ni kweli ndio strategic yenyewe basi hatajimaliza maana anongea PUMBA na kuingilia majukumu ya watendaji wake wa chini, mfano ni hii habari yake, HAKUNA ANAYETAKA RAISI BULLYING tunataka raisi BOLD
 
Hao ndio mawaziri tulionao kwa karne hii! Analopoka tu kama mtu ambaye hajasoma kabisa. Mbunge ni lazima awape matumaini wapiga kura wake maana kama unaona hiyo barabara iko ndani ya ilani ya c c m kwanini hamkuijenga muda wote jimbo liliposhikiliwa na wabunge wa c c m? Lazima mbunge awaambie wapiga kura wake kuwa bila kumchagua yeye barabara hiyo ingekuwa hadithi. Tumeona majimbo mengi tu yaliyokuwa yakishikiliwa na wabunge wa c c m, baada ya kwenda upinzani tumeona barabara zikijengwa mathalani kwa zito kabwe! Magufuli ndio muongo kwani fedha anayotumia kujenga hiyo barabara ni kodi ya wananchi hata kama mmeweka ktk ilani ya ccm wao ccm hawana fedha ya kujengea barabara! Maana kama wana hiyo fedha tujiulize ni majimbo mangapi yanayoongozwa na wabunge wake hayana hata km 1 kwa kiwango cha lami? Magufuli acha maneno ya kuwaudhi wananchi, fanya kazi uliyotumwa siasa mwachie Nape na mukama wewe fanya kazi. Adios
 
Magazeti feki utayajua tu Kwanini hawa semi upande wa pili ulisemaje na alikuwepo kwenye eneo la tukio wanataka wote tuamini kama wao

Dr, CCM ilikuwa wapi miaka 50 hadi ianze ujenzi leo??

Ni kweli mbunge hajengi barabara kwa hela yake ila anahamasisha na hapo anayo kila sababu ya kujisifu kuwa anajenga barabara
 
Magufuli siku hizi amekuwa na kauli za ajabu zinazotufanya tuhoji kulikoni!! Amechanganywa na mabosi wake? Amekuwa mtu wa mipasho kama Wabunge wa CUF wa upande wa pili. Nlidhani angeweza kuja kuwa Rais wa nchi hii baadae lakini kwa kauli zake za siku hizi nimemuondoa kabisa ktk huo uwezekano.
 
Huyu Magufuli anasumbuliwa sana moyoni na kasi ya upinzani nchini hasa CDM. Kila anapokwenda kufanya kazi za Serkali haachi kusifia serkali na bosi wake JK na wakatii huo huo kuponda wapinzani. Mfululizo wa matukio umeonyesha kwamba ni mtu anayeumizwa sana na utendaji makini wa kambi ya upinzani. Kwanza ni ukweli upinzani ungependa ajibu tuhuma mbalimbali zinazoelekezwa kwake kuhusu sakata la nyumba za serkali walizojiuzia kwa bei ya dagaa. Asitake kuhamisha mawazo yetu juu ya uhujumu wa mali za umma kwa vichekesho vyake vya ajabu. Msomi makini na mahiri hapaswi kuwa kama roboti linalowashwa kwa remote na kuzunguka kila mahali: maneno yale yale na nyimbo zile zile. Abadilishe CD achape kazi zake na awwachie akina Nape wafanye propaganda zao za chama.
 
WAZIRI wa Ujenzi, Dk. John Magufuli, amemtaka Mbunge wa Ukerewe, Salvatory Machemuri (Chadema) kuacha tabia ya kudanganya wananchi wa jimbo lake kwamba mradi wa ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami unaotekelezwa wilayani humo ni wake.

Amesema mbunge huyo anapaswa kuwaambia ukweli wananchi kwamba huo ni mradi wa Serikali inayoongozwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Dk. Magufuli aliyasema hayo juzi wilayani hapa kwenye uzinduzi wa kivuko kipya cha mv Ujenzi, uliofanyika Kijiji cha Kisorya, ambapo pia Machemuri alikuwa ni kati ya wabunge waliohudhuria uzinduzi huo.

Wabunge wengine walikuwa ni Mbunge wa Viti Maalumu, Rosemary Kirigini (CCM), Mbunge wa Mwibara, Kangi Lugora (CCM) na Mbunge wa Musoma Mjini, Vincent Nyerere (Chadema).

Dk. Magufuli alisema mbunge huyo wa Ukerewe amekuwa akipotosha wananchi wa jimbo hilo kwamba mradi huo ameuleta yeye na kwamba ni wake, hivyo kumtaka aache mara moja tabia hiyo, kwani si mradi wake, bali ni wa Serikali inayoongozwa na CCM, chini ya Rais Jakaya Kikwete.

Alisema atapanga ziara ya kwenda wilayani Ukerewe ili awaambie ukweli wananchi kwamba mradi huo unatekelezwa na Serikali na si mali ya mtu ye yote, bali ni mpango wa Serikali na hivyo wasikubali kupotoshwa na mbunge wao anayetaka umaarufu wa haraka kupitia mradi huo.

“Serikali ya Rais Jakaya Kikwete inatekeleza mradi wa ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami katika Wilaya ya Ukerewe, lakini ninasikia mheshimiwa Machemuri, anasema mradi huo ni wake ndiye aliyeuleta.

Nitapanga niende huko Ukerewe niwaambie wananchi kwamba si mradi wake, bali ni wa Serikali ya Chama Cha Mapinduzi,” alisisitiza Dk. Magufuli.

Aliwataka viongozi wa vyama vya upinzani kuwaambia ukweli wananchi wao kuwa miradi ya maendeleo inayotekelezwa katika maeneo yao ni sera ya CCM, kwani iko ndani ya Ilani ya Uchaguzi ya chama hicho.

Alisema ujenzi wa barabara ya Nyamuswa, Bunda, Kisorya hadi Ukerewe mkoani Mwanza, kwa kiwango cha lami, tayari umeanza kutekelezwa katika hatua ya kwanza ambayo ni ya upimaji na kwamba kabla ya mwaka 2015 wananchi wataona mkandarasi anajenga barabara hiyo.

Source: gazeti la Habari Leo, December 19, 2011.

BIG UP MHESHIMIWA Magufuli kwa kuwapa ukweli watanzania kukusu utekelezaji wa sera za CCM

Huu ni mradi wa Watanzania wote Machemuli akiwemo kwa kuwa ni kodi zao
ndizo zinazotumika na wala si mradi wa CCM kama wanavyotaka kujigamba.
Kufanyika kwa kuwa serikali ya CCM inatawala si kigezo cha kudai ni mradi wao,
hatutaki siasa za majigambo wakati ukweli hauko hivyo...
 
Yaaani siku hizi silipendi hili li Magufuli limekuwa limtu la porojotu,alaa.
 
Back
Top Bottom