Magufuli - Mbunge Machemuri muongo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Magufuli - Mbunge Machemuri muongo

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by MAFILILI, Dec 19, 2011.

 1. MAFILILI

  MAFILILI JF-Expert Member

  #1
  Dec 19, 2011
  Joined: Apr 28, 2011
  Messages: 1,916
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 160
  WAZIRI wa Ujenzi, Dk. John Magufuli, amemtaka Mbunge wa Ukerewe, Salvatory Machemuri (Chadema) kuacha tabia ya kudanganya wananchi wa jimbo lake kwamba mradi wa ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami unaotekelezwa wilayani humo ni wake.

  Amesema mbunge huyo anapaswa kuwaambia ukweli wananchi kwamba huo ni mradi wa Serikali inayoongozwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM).

  Dk. Magufuli aliyasema hayo juzi wilayani hapa kwenye uzinduzi wa kivuko kipya cha mv Ujenzi, uliofanyika Kijiji cha Kisorya, ambapo pia Machemuri alikuwa ni kati ya wabunge waliohudhuria uzinduzi huo.

  Wabunge wengine walikuwa ni Mbunge wa Viti Maalumu, Rosemary Kirigini (CCM), Mbunge wa Mwibara, Kangi Lugora (CCM) na Mbunge wa Musoma Mjini, Vincent Nyerere (Chadema).

  Dk. Magufuli alisema mbunge huyo wa Ukerewe amekuwa akipotosha wananchi wa jimbo hilo kwamba mradi huo ameuleta yeye na kwamba ni wake, hivyo kumtaka aache mara moja tabia hiyo, kwani si mradi wake, bali ni wa Serikali inayoongozwa na CCM, chini ya Rais Jakaya Kikwete.

  Alisema atapanga ziara ya kwenda wilayani Ukerewe ili awaambie ukweli wananchi kwamba mradi huo unatekelezwa na Serikali na si mali ya mtu ye yote, bali ni mpango wa Serikali na hivyo wasikubali kupotoshwa na mbunge wao anayetaka umaarufu wa haraka kupitia mradi huo.

  “Serikali ya Rais Jakaya Kikwete inatekeleza mradi wa ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami katika Wilaya ya Ukerewe, lakini ninasikia mheshimiwa Machemuri, anasema mradi huo ni wake ndiye aliyeuleta.

  Nitapanga niende huko Ukerewe niwaambie wananchi kwamba si mradi wake, bali ni wa Serikali ya Chama Cha Mapinduzi,” alisisitiza Dk. Magufuli.

  Aliwataka viongozi wa vyama vya upinzani kuwaambia ukweli wananchi wao kuwa miradi ya maendeleo inayotekelezwa katika maeneo yao ni sera ya CCM, kwani iko ndani ya Ilani ya Uchaguzi ya chama hicho.

  Alisema ujenzi wa barabara ya Nyamuswa, Bunda, Kisorya hadi Ukerewe mkoani Mwanza, kwa kiwango cha lami, tayari umeanza kutekelezwa katika hatua ya kwanza ambayo ni ya upimaji na kwamba kabla ya mwaka 2015 wananchi wataona mkandarasi anajenga barabara hiyo.

  Source: gazeti la Habari Leo, December 19, 2011.

  BIG UP MHESHIMIWA Magufuli kwa kuwapa ukweli watanzania kukusu utekelezaji wa sera za CCM
   
 2. Shine

  Shine JF-Expert Member

  #2
  Dec 19, 2011
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 11,514
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Unashangaa hilo mbona ccm hakuna mkweli wala mwaminifu hata kwenye ndoa zao nadhani wako hivyo hivyo
   
 3. Pota

  Pota JF-Expert Member

  #3
  Dec 19, 2011
  Joined: Apr 8, 2011
  Messages: 1,813
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  ni mradi wa cdm (machemuri).....serikali imeajiriwa tu na cdm. majimbo yote ambayo kuna vyama vya upinzani kumechangamka na kuna maendeleo coz of upinzani. kama huamini njoo tanga ucheki mambo yalivyoovyo coz of ccm.

  kwani hakuna hata jimbo moja la upinzani. matokeo yake viwanda vingi vimekufa, na cha kusikitisha zaidi ni kiwanda cha unga cha pembe ambacho watu wengi walipata ajira.

  pale lakini kimizengwezengwe kimefungwa.....kwa nini? hatuna serikali inayojali maisha ya wananchi wake.
   
 4. Mabagala

  Mabagala JF-Expert Member

  #4
  Dec 19, 2011
  Joined: Nov 27, 2009
  Messages: 1,465
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  Maskini Ukerewe! kumbe mradi wenyewe mpaka 2015? tumeliwa! hapo tuhesabu maumivu tu.
   
 5. MBURE JASHA

  MBURE JASHA JF-Expert Member

  #5
  Dec 19, 2011
  Joined: May 7, 2011
  Messages: 200
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Ah! na kuchelewesha mishahara ya watumishi ili waendelee kuadhirika nazo ni sera nzuri! wabongo wake up and perish this nonsense sentences. huo ukweli anaoenda kusema huko ukerewe ni upi! sio kodi zetu hizo hizo zinazojenga barabara ndio posho za huyo hayawani! aache unafiki wake pesa za barabara , hizo wanazogombea kama posho si za CCM ni zetu watz. Nawe mleta huu uzi kichwa chako kipo masaburi masaburi tu
   
 6. Chakaza

  Chakaza JF-Expert Member

  #6
  Dec 19, 2011
  Joined: Mar 10, 2007
  Messages: 23,650
  Likes Received: 21,865
  Trophy Points: 280
  Toka Magufuli aanze kujiingiza kwenye siasa za kijinga na uongo akiwa Igunga naona sasa anapoteza mwelekeo
   
 7. Daudi Mchambuzi

  Daudi Mchambuzi JF-Expert Member

  #7
  Dec 19, 2011
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 31,782
  Likes Received: 36,777
  Trophy Points: 280
  Na huu mchakato wa katiba mpya ni utekelezaji wa sera ya chama gani??
   
 8. ntamaholo

  ntamaholo JF-Expert Member

  #8
  Dec 19, 2011
  Joined: Aug 30, 2011
  Messages: 10,144
  Likes Received: 2,104
  Trophy Points: 280
  ni wa mbunge cdm kwa kuwa unafanyika katika himaya yake, yeye ndo msimamizi wa kuhakikisha unafanikiwa. kutoa mpesa ni suala moja, lakini utekelezaji ni suala lingine.

  hata hivyo, pesa zote ni za wananchi, c za ccm wala cdm, lakini ccm wameziiba kwa mda mrefu huku wakitutuliza kwa utekelezaji wa miradi midogomidogo
   
 9. ntamaholo

  ntamaholo JF-Expert Member

  #9
  Dec 19, 2011
  Joined: Aug 30, 2011
  Messages: 10,144
  Likes Received: 2,104
  Trophy Points: 280
  malock atakwambia CCM
   
 10. L

  LATTICE BOND JF-Expert Member

  #10
  Dec 19, 2011
  Joined: May 30, 2011
  Messages: 219
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwako Magufuli:-
  Kama huo ni mradi wa ccm. mbona kuporomoka kwa uchumi husemi kuwa kumesababishwa na ccm?
   
 11. B

  Bobuk JF-Expert Member

  #11
  Dec 19, 2011
  Joined: Oct 8, 2010
  Messages: 5,876
  Likes Received: 481
  Trophy Points: 180
  Ukweli ni kwamba hiyo ni hongo ya CCM kupitia kodi zetu ili Wakerewe 2015 wamurudishe mbunge wa CCM.
  BTW, hivi ahadi ya JK ilikuwa moja tu Ukerewe? Machemuri ndaa orodha ya ahadi zote alizozitoa JK UK
  halafu amukabidhi Magufuri azisome mbele ya wakerewe akishindwa wewe fanya hivyo.
   
 12. K

  Kolero JF-Expert Member

  #12
  Dec 19, 2011
  Joined: Apr 11, 2010
  Messages: 493
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Mbunge ana nafasi kubwa katika jimbo lake kumbe ni mradi wake huo wala hakuna ubishi ila kauleta nani ni jambo lingine maana huduma muhimu kwa jamii hazibebi chama bali kodi yetu wananchi wote na hata Serikali iliyopo ni yetu wote, ni lazima watofautishe Chama na Serikali ingawa wanasema Serikali ya Chama cha Mpainduzi, si kweli ni Serikali ya Tanzania.
   
 13. M

  Mfwatiliaji JF-Expert Member

  #13
  Dec 19, 2011
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 1,325
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  huyu jamaa anaelekea kuwa mwehu sasa..kama anadandia treni kwa mbele vile..
   
 14. T

  Tanzaniaist Senior Member

  #14
  Dec 19, 2011
  Joined: Nov 29, 2011
  Messages: 162
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Huyu Magufuli sijui ana matatizo gani! au nadhani kile kikombe cha babu lioliondo kilimu overdose...
  Hajui kutofautisha shughuli za kiserikali na shughuli za kichama...ndio maana ataiponza CCM igunga...kwani
  CDM wanaweza kushinda kesi kutokana na kidomo domo cha Magufuli katika kampeni Igunga kuhusisha shughuli za kiserikali na mambo ya kichama

  Vile vile huo mradi...ni wake machemli...kwani kazi yake ni kuusimamia na aliwaahidi wapiga kura wake wa ukerewe...,bila yeye pesa zinaweza kuliwa na watendaji..
  Kwahiyo ni haki yake kujidai ni mradi ni wake..

  Namshauri tu magufuli..naona ana tamani sana kupambana na CHADEMA..namshauri ajivue gamba agombee tena ubunge ili apambane na chadema! naona anapenda sana mapambano nao
   
 15. H

  Hofstede JF-Expert Member

  #15
  Dec 19, 2011
  Joined: Jul 15, 2007
  Messages: 3,584
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 0
  Hivi kumbe hii miradi inaendelea kwa feadha za walipa kodi ina ownership ya vyama au mtu binafsi?. Mi nilidhani ni miradi inayofanywa kwa ajili ya watanzania ikisimamiwa na serikali ya watanzania regardless chama gani kinaongoza serikali hiyo. Kwa style hii ya mawazo kama ya kina maghfuli sasa nimeamini kwa nini Tanzania tunasuasua. Yaani kila kitu siasa mbele. Hakuna mbunge wala waziri yeyote anyeweza kujilimikisha mradi isipokuwa tu kupata credit kwa ushawishi na utekelezaji wa mradi. Maghufuli jenga barabara mambo yakiwa sawa wananchi wenye wataamua katika sanduku la kura.
   
 16. T

  TanzActive JF-Expert Member

  #16
  Dec 19, 2011
  Joined: Nov 14, 2007
  Messages: 350
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Mbona yeye si Mkweli hadi kwa Mkewe
  Mbona yeye si Mkweli kwa watanzania , alimptatia hawara wake Nyumba tena akiwa mwanafunzi wa chuo kikuu na hajawahi kufanya kazi serikalini hata kidogo. Yaani Magufuli na uzeee wake wote anatembea na Sundi ambaye anafaa kuwa mwanae wa kumzaa kabisa
   
 17. Raia Fulani

  Raia Fulani JF-Expert Member

  #17
  Dec 19, 2011
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 10,220
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  naona huu ni mwendelezo wa porojo za Magufuli. 'sera za ccm...'
   
 18. Amiliki

  Amiliki JF-Expert Member

  #18
  Dec 19, 2011
  Joined: May 6, 2011
  Messages: 2,087
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Na kuhusu ile Ilani ya CCM ya kutujengea barabara za juu huku Dar ameuzungumzia au ile ilikuwa ni Ilani ya Chadema?
   
 19. TOWNSEND

  TOWNSEND JF-Expert Member

  #19
  Dec 19, 2011
  Joined: May 8, 2011
  Messages: 2,597
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 145
  mwambieni maku lock aache ujinga mradi ni wetu wote tunalipa kodi....msimamizi mwakilishi wa wananchi ni mbunge ,,,labda kipara kinapunguza uwezo wa kufikiri nawe ulieleta hii weka picha yako labda na wewe una bold
   
 20. N

  Ndole JF-Expert Member

  #20
  Dec 19, 2011
  Joined: Jul 1, 2011
  Messages: 352
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35

  Nilijua tu hili jina ni la kule. BTW kwani chama tawala kinajenga barabara kwa kutmia hela za chama au wanachi wote??? kwa hiyo hao wananchi hawana hata uhuru wa kusema barabara hii ni ya kwetu bali wanatakiwa kusema ni ya ccm siyo. Shame on you magufuli.
   
Loading...