Hii ni hatua nzuri kwa kuanzia. Ingekuwa ni uongozi uliopita haya matokeo yangechakachuliwa asilimia 75 ikapasi!
Naamini kuwa KUKUBALI UKWELI unaouma ni hatua ya kwanza ya kuweza kujirekebisha. Hivyo tukubaliane kuwa shule sio majengo mazuri, madawati, vitabu na mtaala. Bila kuwa na walimu wenye sifa na weledi hatufiki mbali. Hata kama mtanisema humu, lakini ukweli ni kuwa waalimu wetu wengi hawana sifa za kuwa waalimu. Wengi wanafundisha masomo wasioyajua vizuri kwani msingi wao haukuwa mzuri. Kibaya zaidi ni kuwa wakishapata kazi, hawajiendelezi wala kujisomea nyumbani. Wanaingia darasani kwa mazoea. Nafikiri Magufuli analijua hili kwa hiyo ili kuongeza kiwango cha taaluma, tutumbue jipu la walimu incompetent.
Hivi kwanini kila matokeo mabaya yakitoka lawama ni kwa waalimu na serikali tu? Wazazi mnawaacha wapi? Watoto wa siku hizi hata wakafundishwe na nani bado ufaulu wao kupanda ni kidogo sana na hii ni kutokana na malezi ya siku hizi wazazi jukum la elimu wanawaachia waalimu na serikali.
Nidhamu humsaidia mwanafunzi kufanya vizur katika masomo yake lakini utakuta mtoto anatoka nyumbani kwa wazazi wake yani ka kaaga anaenda kupiga show na diamond. Kanyoa kiduku, sketi fupi mara kusuruali kinambana.
Hivi kama mzaz anashindwa kumcontrol mwanae je mimi mwalimu au serikali nawezaje? Una hisi mwalimu akipewa mshahara mkubwa na motisha ndo ataweza kumbadili huyo kijana?
Mimi ni mwalim, na nina uzoefu na kazi, tatizo kubwa kwa hiki kizaz cha saiz ni kuporomoka kwa maadili na wazazi kuwa bize na mambo yao kiasi kushindwa kumfuatilia mwanae anafanya nn shuleni.
Hata nkiuliza saizi wangap toka wiki imeanza wameharibu kuangalia maendeleo ya watoto wao shuleni, utakuta hamna au wachache sana zaid wazaz wanachojua ni mtoto kapewa nauli, kalipiwa ada na anaenda shuleni ila kujua anafanya nn huko wala hawaangaiki wanasubiri tu matokeo yatoke waanze kulalama mara waalimu mara serikali.
JIULIZE WEWE KAMA MZAZ AMBAYE NI MDAU MUHIMU KATIKA ELIMU UMEFANYA NINI KUHAKIKISHA MWANAO ANAFAULU mbali na kuangalia WAALIMU NA SERIKALI?
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.