Magufuli kachukue Wanyarwanda uwaajiri watusaidie sehemu ambako kuna watendaji wabovu

YEHODAYA

JF-Expert Member
Aug 9, 2015
36,902
51,992
Magufuli anapenda nchi iende kasi kimaendeleo.Lakini kuna maeneo watendaji wanavuta miguu na kubinya midomo hawaendani na kasi anayotaka kwenda nayo Magufuli.

Ni kawaida kwa mkuu wa nchi ukiona mambo hayaendi kwenye sehemu unazotaka ziende kasi kutafuta wataalamu wenye uwezo,ari,na nguvu kwenye maeneo husika kuwaajiri kukusaidia toka nchi zingine.

Tanzania haihitaji kwenda kuwafuata Ulaya au Marekani wanakoweza taka mishahara mikubwa.Magufuli amwombe Kagame ampe watu wenye uwezo washike sehemu zinazozengua ambako watendaji si wabunifu na ni watu wa kubeza beza tu aweke wanyarwanda walau washike kwa miaka mitano kwa mishahara anayotaka Magufuli.Atawapata kibao.

Hili si la ajabu.Mfano sekta ya elimu Kenya ilikuwa mbaya mno na ilikuwa hovyo sana miaka ya sabini.Uganda walikuwa wako vizuri sana kwa nchi zote Afrika mashariki.Idd amin aliposhika Uganda walimu wengi walikimbia uganda wakatorokea Kenya.Kenya ikaamua kuwatumia kwa kuwapa kazi na vyeo kama walimu wa shule za serikali za kawaida,walimu wakuu hadi maafisa elimu wa wilaya na mikoa na wizarani.Sekta yote ya Elimu walikabidhi kwa waganda.Waganda wakaitengeneza na kuisuka sasa hivi kenya inaongoza Afrika mashariki nzima kwa uzuri.Uganda baada ya Amin kuiporomosha na viongozi waliofuata kutoitilia maanani imebaki kusuasua

RWANDA imeonyesha kuna watu wanaweza tuwachukue tuwatumie.Eneo kama la SHIRIKA LA ndege awachukue toka Rwanda kuanzia Marubani,mainjinia hadi ma AIR HOSTESS,menejiment nk watutengenezee shirika.

Pia aangalie maeneo mengine kama Mipango miji nk na kule ambako anaona Rwanda imefanya vizuri waje watusaidie.

Sioni sababu kwa nini Raisi aendelee kuumiza kichwa kwa ajili ya watendaji ambao hawaendi na kasi yake.Aangalie nje awalete haraka twendelee na safari.

Rwanda ni rahisi kupata wataalamu wazuri kwa mshahara mdogo wa kawaida tofauti na kuwachukua wataalamu hao toka nchi zingine kama Kenya,Uganda au nchi zingine za nje au DIASPORA watanzania walioko nje.Wanadai bei kali utafikiri sio watanzania.
 
Bangi za mapushapu!! Kweli niambie rafiki zako nikujue.

Mumekaa kimizuka mizukaaa!
 
Hii nchi ina kazi!
YEHODAYA umewahi kufika Rwanda?
Maana mimi nimefika!
Unajua ukubwa wa Rwanda?
Unajua idadi ya watu Rwanda?
Unajua mentality za wanyarwanda?
Unajua matatizo ya Rwanda na majirani zake?
Umewahi kupata au kusikia usanii wa Rwandiar? Maana mimi imewahi kunishindisha Jomo Kenyata kutwa nzima!
Nenda Rwanda, pita pale Genocide memorial utalii kama masaa mawili halafu uingie mtaani!
Rwanda hata kama kuna buffee, wao ndio wanakuchagulia ule nini.
Yani nilikuwa najuaga na wewe ni mtu kumbe ni hewa tu!
 
Kama wewe ni miongoni mwa book saba wa rumumba basi wanatakiwa wakufutie usajili maana hii pumba inawaathiri hata wao. Umewavua nguo hadharani kbs. Halafu kesho utajiita mzalendo.​
 
Hasa mipango miji mimi huwa inaniuma sana kila nilinganishapo na nchi zilizoendelea. Unakuta halmashauri/jiji/manispaa inagawa viwanja halafu haipeleki miundo mbinu, haitoi muongozo wa majengo, na mwisho kila mtu anajijengea ovyo ovyo na kila kitu kinaishia kuwa ovyo ovyo, wakati huo huo sheria na kila mpango na taratibu zipo ila wakurugenzi hawazifutai kabisa.
 
Mnakubali nyie ccm ni vilaz hamuwezi kumsaidia rais kabidhi nchi upinzani mkali muone.
 
Umetumia haki yako ya kikatiba kutoa maoni.... Naheshimu mawazo yako lakini nakuomba uende milembe ukatibiwe kwanza ili siku nyingine utoe maoni mazuri kama hayo....
 
Mnakubali nyie ccm ni vilaz hamuwezi kumsaidia rais kabidhi nchi upinzani mkali muone.

Halmashauri ya HAI ambayo iko chin ya CHADEMA na Mbowe ilipata hati chafu ya ukaguzi wa mahesabu ya CAG
 
Mmewachukulia hatua gani hao waliopata hati chafu.

Mbowe kabanwa na woga.Alijua HILO LA HATI CHAFU HAI NA UBADHIRIFU litaibuka bungeni.Ndio akaja na gia ya kuwaambia wabunge wote wa UKAWA wasuse Bunge kwa visingizio vya kutunga akiogopa kuadhirika ikiibuliwa akiwemo bungeni akiwepo.Kwa hiyo kabla ya kuanza majadiliano ya bunge anakimbia na wenzie akihofia isije ikaanza hiyo hoja likatolewa azimio la bunge hapo dhidi yake.

Lakini dawa iko jikoni inachemka
 
YEHODAYA hujajua, suluhu ya yote ni kuitoa CCM madarakani. Yani wala hutaona uhitaji wa wanyarwanda na Wachina.
'NCHI ITATULIA TULI, KAMA MAJI YA MTUNGI' by Baba yetu Lowassa.
 
YEHODAYA hujajua, suluhu ya yote ni kuitoa CCM madarakani. Yani wala hutaona uhitaji wa wanyarwanda na Wachina.
'NCHI ITATULIA TULI, KAMA MAJI YA MTUNGI' by Baba yetu Lowassa.

SiJAROGWA kama wewe ulivyorogwa

LOWASA.jpg
 
Back
Top Bottom