MAGUFULI EPUKA MAJARIBU, RUHUSU UKUTA KUEPUKA MTEGO
Mh Rais kama unapitiaga huku, nikushauri kidogo na kwa ufupi tu jinsi ya kuruka huu mtego wa UKUTA uliojitengenezea mwenyewe kwa kutotazama mambo katika mapana yake.
Inavyoonekana Maandamano ya UKUTA yatafanyika Sept Mosi, sio kauli za viongozi wala mazoezi ya polisi yatakayorudisha maandamano hayo nyuma. Vyama vya upinzani vinaamini kabisa kuwa polisi watatumia nguvu na hata kuumiza ama kuua watu na wamejipanga kuhakikisha vurugu zozote zitakazotokea zitapewa coverage ya vyombo vya habari hasa international media. Mashirika ya habari ya kimataifa yamejipanga kukuza hiyo habari zaidi ya unavyofikiria. Kumbuka tumeshawaudhi baadhi ya nchi kubwa kwa kuwachunia na kuwabania maslahi nchini. Watafurahi sana wakipata pa kuanzia kukuweka madoa na kuku-destabilise. Wakati ule wa kusaini tu sheria ya makosa mtandaoni, nchi zaidi ya 10 za magharibi zililaani hilo na hata kupelekea kunyimwa misaada fulani. Wanakucheki tu. Kuna watu wengi wanatamani sana mambo yakuharibike uonekane huwezi kuongoza.
Lengo lako ni zuri, tunahitaji kufanya kazi, tuna deni kubwa la Taifa la kulipa, hatuna pesa za kulipia huduma za jamii. Kila kona umekuta mambo ni hewa, hewa tu. Binafsi naamini watanzania wengi wa kawaida wanahitaji zaidi uhakika wa chakula, maji, makazi kuliko haki ya maandamano ama majumuiko. Ila haki za majumuiko ni muhimu pia, kinachotakiwa ni utaalam wa ku ”manage” ili zisikutoe kwenye mstari.
Cha kufanya sasa ni kuhakikisha maandamano ya UKUTA yanafanyika kwa amani na kwa msaada mkubwa wa vyombo vya usalama. Ndio fanya hivyo. Sasa hivi upinzani unategemea msuguano na vyombo vya dola ili kupata sera ya kujinadi zaidi. Na polisi nao ni vipofu hawaoni hilo. Ukiruhusu Maandamano, niamini, kwanza unashusha mihemko ya watu kwa 50%; watu wengi wataona hakuna jipya, hawatapa kuona ule mkwaruzano waliotegemea, na believe me maandamano yakipewa go ahead, idadi ya wanaotarajia kuandamana itapungua kwa kiasi kikubwa.
Ondokana na hofu ya kuonekana ”umebana, umeachia”, Kwa kuruhusu UKUTA ni positive kwako, na kwa UKUTA sio. Waambie anayetaka kuandamana aende barabarani, aandamane salama, anayetaka kufanya kazi tuonane makazini. Ukiendelea na msimamo wako wa kukataza , halafu wao waka-force kufanya maandamano ni hasara kwako, kwa sababu serikali italazimika kutumia nguvu ili isionekane imeshindwa na pengine kusababisha watu kuumizwa. Tusingependa kuona we Rais wetu , the special one, ukianza kwa kumwaga damu, na hilo ndilo baadhi ya wanasiasa wanaliombea ili kuharibu rekodi, wasifu na sifa nzuri ulizojitengenezea ndani ya muda mfupi. Wanasiasa wa UKUTA hawatajali kuona baadhi wa wananchi wa kawaida wakipoteza maisha kwenye maandamano, kwanza hilo litawasaida kukuza hoja yao ya dikteta asiyeruhusu mikutano ya kisiasa (ikitokea vurugu watu wakaumizwa watsema dikteta muua watu). Hilo ndilo jaribu kubwa liliopo mbele yako
Pia wakanye watendaji wako wasiwe wanadakia kauli zako na kuzifanya zao ama kuzivumisha. Hili linakuharibia maana wakati mwingine wanaishia kukuza ishu au tatizo kuliko hata wewe ulivyomaanisha. Hili ni muhimu kwani wakati mwingine utalazimika kuja kutoa ufafanuzi unaopingana na matamshi wanayotoa na hivyo kuonekana hamshauriani vizuri.