Magufuli bila madaraka yukoje?

hasante sana mkuu.
 
/.
Mkuu , labda niongelee kwa nafsi yangu kuwa nipo na nafuatilia mjadala kila nikipata fursa

Levictus alitaka kujua kama niliyoandika 2011 bado nasimama nayo. Nimemjibu bandiko 237 nikimujumuisha mpwa wangu Judi wa Kishua

Nilisema hivi, tunahitaji nidhamu nchini na kwamba nidhamu inaanzia kwa mtu kwanza kabla ya kusambaa.

Nidhamu ni utartaibu unaofuatwa kwa kuzingatia taratibu.

Kuna tofauti ya nidhamu na woga. Ninasimama katika nidhamu kwani ndicho tunahitaji

Nikasema sote tunataka mapambano dhidi ya uovu na waouvu wanaoifasidi nchi

Nimerejea kwa hili kwasababu kuu moja.
Wapo wenzetu wanaoamini wale wanaosimamia nidhamu na mapambano ya ufisadi n.k.

Halafu wapo (nikiwemo) tunaoamini katika nidhamu na mapambano ya ufisadi kwa udhati, kwa nidhamu bila kupepesa macho, bila mahaba, bila kuonea au kuhurumia.

Nitoe mifano. Jana Rais alikuwa Unguja katika ziara inayosemwa ya kiserikali.
Wasoma risala walizungumzuia habari za CCM. Shughuli ilikuwa ya CCM kwa kila mantiki.

Sasa kama mikutano ya siasa imepigwa marufuku mbona huu wa ''ccm' umeruhusiwa?

Je, hapo kuna nidhamu ya kutekeleza yale yanayosemwa?
Wapo wapi wanaokemea maandamano na mikutano ya siasa?

Je, huo si uoga? Tofauti ya nidhamu na uoga ipo wapi?

La pili, tumesikia Rais akisema kitendo cha mtu fulani kukataa kutoa mkono kwa Rais wa Zanzibar asingeweza kusaini makaratasi ya mtu huyo kwenda kutibiwa.

Kwamba mzozo wa mambo yao binafsi unaingiaje katika haki zao kisheria

Aliyekataa kutoa mkono ana haki ya kufanya hivyo kama binadamu

Hakuna sheria ya nchi inayolazimisha wawili hao kupeana mikono kwa namna yoyote

Haki ya kutibiwa nje ni ya kisheria , si favor wala hisani.

Kama ni ku sign karatasi Rais wa ZNZ hana chaguo, ni wajibu wake kisheria na kikatiba
Ndivyo nidhamu inavyotaka, kwamba kuheshimu taratibu

Katika hali kama hii inawezekanaje kuwaambia wananchi kuhusu nidhamu ya kazi?

Hivi kuna karani gani atakayepeleka faili bila kuogopa kumuudhi Rais?

Je,atakuwa ametendewa haki? Je, karani atakuwa ametimiza wajibu wake kwa nidhamu?

Tunaposema kiongozi asimamie nidhamu tuna maana hiyo kuwa nidhamu kila eneo bila chuki , husda au upendeleo.

Ukiangalia Taifa kwanza, utaona sote tunazungumzia umuhimu wa nidhamu na mapambano ya ufisadi, ufujaji na wizi.

Ukiangalia kwa jicho la 'uchama' mahaba n.k. utaiona nidhamu kwa mtu, utaona mapambano ya ufisadi kwa mtu.

Utaweza ku trade nidhamu kwa woga. Utaufumbia macho ufisadi kwa kuuita ujasiriamali.

Nasimama na bandiko langu la 2011 kwa asilimia zote.
 
mlitakiwa kusoma bandiko hili la mwaka 2011 ili kumjua na kumuelewa magufuli

mwanakijiji ni nabii wa haya mambo

swala eti anamsifia magufuli ni kwa sababu , hakuna wa kusifiwa upinzani!!

mwanakijiji ni muumizwa wa kuondolewa kwa akina slaa,

mrudi nyuma angalieni mlianguakia wapi, mtalaumu sana. na the fact kuwa Magufuli ndio rais, mtaongea kwa kinyongo kila siku kwa miaka 10 ijayo!!!

badala ya kuweka hoja za msingi, hoja zenu ni kumshambulia na kurudi nyuma kufuatilia MKJJ alisema nini


tukirudia misimamo yetu ya nyuma, nani atapona humu??

tujadili hoja hasa kwa nyie wakongwe, heshima zenu za ukongwe na mawazo yenu yanahitajika sana

ila inabidi kuwa na uhuru wa mawazo, na uwezo wa kukataa hata unachokipenda, uwezo wa kukosoa hata pale utakapoona aibu, uhuru huu wengi wenu hamna!! hamuwezi kusifia wala kukosoa kwa akili huru, pasi kuongozwa na emotion na madonda ya moyoni ambayo ndio haya yanafanya ndugu mgombane na kutengeneza mipasuko

iko wapi JF ya kujadili hoja kwa hoja, pasi kutajana eti ulisema hivi jana, ulisema hivi juzi, unasema hivi leo....why??


tunaiharibu JF

Fact ni kuwa Magufuli kuna mazuri mengi anafanya! halina ubishi hili
Fact ni kuwa juzi alikosea kusema 'siasa hazitakiwi' hili nalo halina ubishi

Fact ni kuwa upinzani mpaka leo, hauna hoja ya kuisumbua serikali kwa mambo ya msingi ya kuleta maendeleo, akili hii...haiko upinzani, hamna, na haileti faida kwa mtanzania wa kawaida.

Fact ni kuwa kosa hili la Magu limewaamsham at least iobekane kuna uhai......ila mmesahau hamna la kusema, hamna hoja, msijifiche huko!

mbali ya hoja ya UKUTA hamna lingine lililo mioyoni mwa watu ambao wapinzani wanaweza kuisumbua serikali...hamna, hakuna, halipo na naona halitakuwepo

we need brain kwa wapinzani...zimepotea sana na hata wale niliowategemea kama akina zitto wote kimya!
 
I respect every line of your argument
 
Shikamoo MM.
Hii uliandika miaka 6 iliyopita, Kweli una maono
 
Umeongea fact sana!
Kiukweli sio JF tu, social media imeshindwa kujenga viongozi wetu. Wengi tumetumia vibaya nafasi Hii ku-bully others na kufanya intimidation au assassination ya sifa za watu hasa viongozi.
Kuna sehemu nyingi JPM na viongozi wetu wengine wameteleza, kama binadamu wanayajua hayo tena baada ya kusoma reactions za watu au feedback kwa njia nyingine zozote.
Shida ipo kwa watu wanao-abuse nafasi Hii kwa kutaka kumtishia kiongozi, unapomuwekea conditions au ultimatum, kwamba he was suppose kufanya hivi, au mtoe x, etc.
Bullying kwa kiongozi wa juu kabisa wa Nchi ni kukaribisha trouble, he will never bend na sote tunakuwa losers.
Nadhani JF inapaswa Kurudi kwenye level yake ya kuanalyse issues na kuwekea mizania ili actors angalau wajisahihishe! maana what is the use ya kufanya hiki kuwa ni kijiwe cha kutusi au kushambulia viongozi au watu wengine!
 
Mwanakijiji wa wakati aliyetumia mali na muda wake mwingi kuandika article zilizotulia sana na kupendwa na Watanzania wengi waliobahatika kuzisoma kabla hajaamua kuhamisha goli.

Duh.. na wewe inaonekana umesoma kichwa cha habari tu; kinyume na mliobadilika sisi wengine kanuni zinatukataza kubadilika!
 
watu mnaona mbali
 
Sijawahi kubadilika kuhusu fisadi yoyote nchi hii na wala sina sababu ya kufanya hivyo ila wewe wanaokufahamu na mabandiko yako wanakushangaa sana.

Duh.. na wewe inaonekana umesoma kichwa cha habari tu; kinyume na mliobadilika sisi wengine kanuni zinatukataza kubadilika!
 
Dah hahaha vipi bado mgonjwa au macho hayaoni tena
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…