Magufuli azua Taharuki CUF, wajipanga kimya kimya kushiriki Uchaguzi

TataMadiba

JF-Expert Member
Feb 7, 2014
9,866
5,743
5.jpg
 
Wallah hii habari hakuna mwana-CCM hata mmoja anayeweza kuifurahia kwahiyo kwamba eti JPM azua taharuki ni kujifariji! Na endapo CUF watashiriki, basi hata baadhi ya wana-CCM wenyewe wanaweza kupiga kura za hasira dhidi ya chama chao kutokana na uhuni wa wazi ambao umeoneshwa na CCM!!
 
RAIA MWEMA!! TEHE! Tehe! Tehe! Mko Vizuri Ktk Propaganda Za Lumumba, Chini Ya KITENGO Cha Propaganda!!! Tokea Kipindi Kile Cha Harakati Za UCHAGUZI Mkuu 2015, Watanzania Wameshalitambua Rangi, Itikadi Na Mlengo Wa Gazeti LENU! HIVYO Wala Hawapati SHIDA Na Kuusoma UPUUZI Wenu Mnaojaribu KUPELEKA Kwao, Kama Ilivyokuwa Kipindi Kile Na Sasa Vivyo Hivyo!!! HBR Zenu Zisizo Na VYANZO, USHAIDI, MUANDISHI ALIYERIPOTI, UWIANO N.k!! ALAFU Siku Zoote HBR Mbaya Kutoka UPINZANI Tu Na Nzuri Tupu Toka CCM!!!! KUMBUKENI Watanzania Wa Sasa Sio Wala Wa 1995!!!!!!?? ILA Nawapongeza Kwa Kuichangamkia Fursa Ya Kujiingizia Kipato Cha Kuwawezesha Kuishi!!! INGAWA Mnalipwa Na Kuishi Na Familia Zenu, Nafsi Zenu Zinawasuta Kwa Kusambaza Uongo Na Kuacha Ukweli!!!! WENZENU Wanapongezwa Kwa Kuandika Hbr Zenye Tija Kwa TAIFA (JAMHURI) NINYI Subirini Nape Awape Tunzo!!!
 
Hata mimi nimeishangaa hii habari ya "watu eti kujipanga kushiriki kimyakimya" wakati walishautangazia umma wa Tanzania na Dunia nzima kwa sauti kubwa na ya juu kabisa kuwa hawatashiriki na kwa sababu ambazo ni very valid na kila mmoja anazijua ikiwemo kubwa na kuu kuliko zote ya uchaguzi wenyewe uitwao "wa marudio" kuwa haupo na kwa hiyo si halali na ni batili kisheria na kikatiba!!

Utawezaje kushiriki kwenye jambo kubwa kama uchaguzi ambao hauko supported na sheria wala katiba iwe kwa "sauti ya juu" au kwa kunyetia "kimya kimya" kama ambavyo wanapropaganda wa CCM wanavyojaribu kutuhadaa kupitia vipeperushi vyao hivi?

Nadhani hii ni propaganda tu ya kujaribu kuwachanganya baadhi ya wazanzibar na watu wengine ambao hawana taarifa za kutosha juu ya ujinga na upuuzi unaoendelea huko Zenj. Hii ni dalili kwamba Jecha na CCM yake wamekabwa koo!
Tata Madiba,
Hiyo si kweli ni propaganda.

CUF ina ''election machinery'' nzuri sana ambayo inajua nini cha
kufanya katika kupiga kura.

Hii moyo wake ni kuapashana habari.

Licha ya hilo huwezi kufanya uchaguzi kimya kimya juu ya kuwa
CUF ishasema haitashiriki uchaguzi wa marudio.
 
Wallah hii habari hakuna mwana-CCM hata mmoja anayeweza kuifurahia kwahiyo kwamba eti JPM azua taharuki ni kujifariji! Na endapo CUF watashiriki, basi hata baadhi ya wana-CCM wenyewe wanaweza kupiga kura za hasira dhidi ya chama chao kutokana na uhuni wa wazi ambao umeoneshwa na CCM!!

Nimependa maandiko yako Ndugu yangu, ila unadhani hakuna wana-CUF wanaopenda CUF ishiriki uchaguzi? Au unadhani hakuna wana-CUF wanaoweza kumpigia mgombea wa CCM? Siasa ni mchezo wa ajabu, niliwahi kuona familia moja na ambayo iko katika chama kimoja lakini hawakumpigia mgombea kutoka katika familia yao.
 
Jenerali Twaha Ulimwengu umeshuka kiasi cha kuendesha gutter press?
Ezekiel Kamwaga amelifanya raia mwema kuwa chini hata ya Mzalendo
 
Back
Top Bottom