MAGAMBA MATATU
JF-Expert Member
- Jul 2, 2011
- 646
- 1,187
Katika maisha hakuna kizuri kinachokosa kasoro, hata ufanyeje hapa duniani hauwezi pendwa na wote hata kama utagawa pesa bila watu kufanya kazi, wapo watakaosema mbona haongezi pesa japo ni bure.
Mwaka 2015, mimi, mama yangu na mke wangu hatukuweza kumpigia kura ya ndio katika uchaguzi mkuu sio kwa sababu hawezi kuiongoza nchi bali kwa kujua hawezi futa falsafa ya chama ya kuiba pesa za walipa kodi,
Ila sasa ndo nimeamini kuwa aliposema "watanzania mnichague sitawaangusha" alikua anamaanisha, rais kafanya uwajibikaji ndani ya serikali kuwa mkubwa, kaondoa kwa 90% ule mlija wa watu kujilipa mishahara bila kuwepo watu wahusika, ameondoa mianya ya watu kuiba pesa kupitia mapato ya TRA, kaamua kufanya uhakiki wa watu kufanya kazi huku sifa siyo zao maana wanagushi vyeti ili kujaza ndugu zao na hili likikamilika watanzania tutegemee ajira nyingi kutangazwa na watoto maskini nao kufaidi matunda ya walichosomea,
Kaamua kuhakiki vyeti vya wanachuo na kujua kama kweli wamepata mikopo kihalali ili atakayepata mkopo afaidi usingizi aliokua anaupoteza ikiwa ni pamoja na kuweka sifa stahili za kujiunga na chuo kikuu na siyo unaingia chuo kiujanjaujanja,
Hatimaye kufikia Mwaka 2019 nchi za Africa zitamuomba ushauri Magufuli jinsi alivyofanikiwa.