Magufuli avuruga mchoro wa Lowassa na CHADEMA!

Magufuli avuruga mchoro wa Lowassa na CHADEMA!

shige2

JF-Expert Member
Joined
Oct 11, 2016
Posts
8,106
Reaction score
3,967
Katika kampeni za kugombea urais nchini Kenya.LOWASSA na CHADEMA
walitaka kutumia tetesi zilizokuwepo kuwa Magufuli anamuunga mkono Raila Odinga.

Hivyo nao katika kulipiza uchungu wa kushindwa uchaguzi wakasema WATAAMUUNGA mkono Uhuru Kenyatta ili Magufuli asikie naye uchungu.

Lakini cha kushangaza ni kuwa Rais Magufuli AMETUMA haraka salamu za PONGEZI kwa rais Kenyatta kwa KUCHAGULIWA tena kwa MUHULA wa pili wa utawala wake. Mara tu zilipotangazwa.

Na hivyo KUSAMBARATISHA KABISA mbinu za KUNGONGANISHA kati ya Serikali ya Tanzania na Kenya. Huku akiwaacha Chadema na Lowassa WAKISHANGAA wasijue nini cha kufanya.

Ikikumbukwa Lowassa alitoa waziwazi kauli yake na chama chake kuwa kinamuunga mkono Kenyatta(.....) NIA kubwa ilikuwa ni kwamba Rais Magufuli aonekane kuwa HAMPENDI Uhuru Kenyatta. Na pia aonekane kama ni Kiongozi asiyejua mambo ya
Utawala,
Protokali na
Diplomasia.

Lakini kwa HEKIMA na USHAURI aliopata akaamua kumpongeza Uhuru kenyatta HARAKA sana na kuwaacha CHADEMA na Lowassa wakishangaa tu wasijue nini cha kufanya.

Maana walikuwa wakifikiri Rais Magufuli ANGEJIKOKOTA kwa muda mrefu KUMPONGEZA Kenyatta katika ushindi wake.

Rais Magufuli aliangalia picha kubwa kati ya URAFIKI na MASLAHI ya NCHI. Na akachagua MASLAHI ya nchi/National Interests badala ya URAFIKI.
kwa Hilo tunampongeza sana.

ITABIDI basi Lowassa and Co. KURUDI kwenye drawing board/ Meza ya KUCHOREA maana MCHORO wao Magufuli AMEUVURUGA na sasa ni HISTORIA.
Hongera Magufuli kwa Hehima hiyo.
 
Kosa kubwa Chadema na hasara kubwa kwao ni kwamba wamefanya jambo litakalowakosesha ushirikiano wa vyama vya upinzani vya kenya.
Maana sidhani kama Uhuru atawapa sapoti yoyote ya maana ili kuwawezesha wao kushika serikali.
 
Pongezi za Magufuli kwa Kenyata ni pongezi za Kenyata pamoja na wote waliochangia ushindi wa Kenyata ikiwa ni pamoja na CHADEMA ambao hawakuishia kumuunga mkono Kenyata peke yake bali walishirika mpaka kwenye kampeni zake kuhakikisha Kenyata anashinda.
 
Jamani ccm mna mambo ! Huo mchoro Lowasa aliuweka meza au kabati ipi mpaka magufuli aufikie na ku uvuruga?mbona hampendagi kauli za kujenga nikuwasha moto tu kila siku ili kumchafua tu Lowasa ? Sasa huko kujipendekeza kutoa hongera na wengine nao wakuvalie Bango ? Manake tunaelewa kilichopo kati ya hawa !. Mtakua mbele kwa mabaya hadi lini? Kwanini atoe pongezi kwa ajili ya kuzima moto wa Lowasa,asitoe tu pongezi ya kawaida ? Wewe ni nani wake mpaka akueleze kua anazima moto wa Lowasa ? Hakika mbea hana likizo,likizo yake ni kaburi ! Huoni hata woga kuzua jambo baya kama hili ? Akisema mpinzani chochote ni uchochezi,lazima apimwe mkojo akiwa rumande !.lakini nyie mnaweza kuvuruga nchi mtakavyo nakuchonganisha mwanzo wa nchi hadi linakotua jua ,na majirani wa nchi ruksa.sasa mmesha chokoza uislamu tusubirini kifuatacho baada ya tafakari yao.sisiemu,mtakufa lini tupumue sisi wanyonge ?
Mungu tuviringishie hili jiwe la kusagia lili tuvaa shingoni,ukalitose baharini, utukomboe,nakuamini mfalme,Amen.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kosa kubwa Chadema na hasara kubwa kwao ni kwamba wamefanya jambo litakalowakosesha ushirikiano wa vyama vya upinzani vya kenya.
Maana sidhani kama Uhuru atawapa sapoti yoyote ya maana ili kuwawezesha wao kushika serikali.
Magufuli kawafunga Ten Nil. Mabao 10 kwa bila.
Msemo wa kisiasa:
" In Politics there is neither a permanent FRIEND nor permanent ENEMY but PERMANENT interests"/
"Katika sisa kamna RAFIKI wa KUDUMU ama ADUI wa kudumu. Bali MSALAHI ya KUDUMU".
Ni nini Kenya itapata toka Lowassa as far as politics is concerned.
Hasa baada ya ngoma ya kali Magufuli?
 
Nadhani hii habari niya umbeya! Umejuaje nia ya Magu na hata ya EL? Una ushahidi gani zaidi ya kufanya umbeya? Achana nazo! Ningeshangaa sana kama Magu asingekuwa wa kwanza kumpongeza Uhuru
REJEA. Gazeti la Kenya The daily nation.
 
Back
Top Bottom