Magufuli ataweza kuitosa CCM?

Magufuli ataweza kuitosa CCM?

naona sasa hivi mmeanza kumpotezea Lowasa hahaha
Mada ni Magufuli kujitenga na chama chake siyo Lowassa,

Magufuli leo anaisema ccm kwa mabaya, kwenye hotuba zake hatumsikii akitoa kejeli, vijembe wala kuipamba ccm kama mtangulizi wake anazungumza kama rais wa nchi.
 
Mkuu umepiga penyewe!! Sasa tunasuburi kuona vikao vya CCM kama vitajaribu kumpungza speed kama vitafaninkiwa.

Hawa mafisadi papa wengi wao ni wadau wakuu wa CCM na sasa wamekalia kaa la moto - kweli nii ni SERIKALI YA MAGUFULI.
e/
Wafanye vikao wana hela..? manji kesha pigwa za uso kwisha coco beach lazima irudi kwa watu wa manzese na mbagala..MAGUFULI KESHAJITENGA NA CCM...next step ni kitangaza katiba ya warioba na kuanzishachama kingine mengi kuwa mfadhili wake mkuu na siyo huyo azam mwizi mkubwa mgfadhili wa ugaidi zanzibar
 
Salama ya Magufuli ni katiba mpya kama ilivyopendekezwa na kamati ya Warioba, basi. Bila katiba mpya atafungwa spidi gavana sasa hivi na watanzania tutapoteza matumaini tulioanza kuwa nayo.

Kule CCM ya Nape kumejaa mafioso waliokubuhu. Watamkumbushakuwa yeye hakuwa chaguo la chama chake kwani nguvu ndani ya CCM ilikuwa kwa El, watamtahadharisha pia kwamba hata EL hakuwa kipenzi cha JK ndo maana jina la Membe ndo lililokuwa likipigiwa chepuo na JK. Wanaweza pia kumwonyesha vielelezo kuwa hata wananchi hawakumpa kura ila amepewa tu urais kwa nguvu ya chama kwa kuiba kura na kutumia vyombo vya dola.

Naitamani hiyo siku nikisikia akina Ritz1 wanaulizwa wapi walikopata mtaji wa utajiri wanaotunisha kila kukicha bila kulipa kodi............ na kufanya jambo kama hili Magufuli anapaswa asijipambanue kama mwana CCM.


 
Uchaguzi ukifanyika tena leo, nitamoatia kura yangu, na hiyo ni kwasababu hadi sasa amefanikiwa 'kujitenga' na CCM.
Na ninaamini kuwa uchaguzi ukifanyika hivi sasa atapata upinzani mkubwa sana ndani ya CCM na ikitokea akaoitishwa basi upinzani utajiweka kando na kumuunga mkono na hivyo kupita bila kupingwa. Tofauti na hapo labda CCM ijimege tena halafu wale watakaokatwa waende Upinzani eg ACT, ili kupambana naye.

Na kweli kabisa, uchaguzi ukifanyika hivi sasa mambo yatakuwa tofauti kabisa. kuna uwezekano mkubwa akapata sapoti ya upinzani zaidi kuliko ndani ya chama chake cha CCM
 
naona sasa hivi mmeanza kumpotezea Lowasa hahaha

Nadhani ni vizuri tuchambue hali halisi ilivyo. ishu sasa hivi siyo Lowasa anafanya nini. ishu ni chama kilichoko madarakani kinafanya nini. kwa mujibu wa katiba yetu, CCM ndio chama kilicho madarakani. sasa tunaangalia utendaji wa Rais ambaye amepatikana kwa tiketi ya CCM, lakini anavyofanya siyo kama ilivyozoeleka. kiasi kwamba hata CCM wenyewe wanaonekana kuwa baridi hawajui wafanye nini. Lowasa hakushinda uchaguzi kwa hiyo hatuwezi kumuongelea kama mtu aliyeko madarakani. anaweza kuongelewa katika muktadha mwingine, lakini sidhani kama hii mada inamhusu
 
Usiamini sana CCM Tegemea usicho kitarajia. Ni watu wa level nyingine kabisa. Yanabadilika kulingana na upepo kama Nepi

Kwa hiyo tutarajie watajiunga na Magufuli katika kasi yake?
 

Naitamani hiyo siku nikisikia akina Ritz1 wanaulizwa wapi walikopata mtaji wa utajiri wanaotunisha kila kukicha bila kulipa kodi............ na kufanya jambo kama hili Magufuli anapaswa asijipambanue kama mwana CCM.

Inaonekana ndiko anakoelekea haswa. wengi tuliona ni nguvu ya soda. lakini dalili zinaonesha siyo nguvu ya soda. inavyoonekana kitakachoamua mustakabali wa mwelekeo wa baadaye wa JPM ni matokeo ya mtanange wake na CCM. atakayeibuka mshindi ndio ataendelea kutoka hapo, na hapo ndio wapinzani wataingia kazini. akishinda JPM, watalazimika kujiunga naye. wakishinda CCM-ufisadi, basi wapinzania watarudi vitani kupambana. kwa sasa hivi kuna wingu nene kwa hiyo kisiasa kuna utata
 
Wakishamvalisha kofia ya Mwenyekiti wa chama atawezaje kukitosa? CCM ndo imemfikisha hapo alipo na kama 2020 anategemea kugombea kupitia chama hiki basi ni lazima alinde maslahi ya chama. Nitofautiane na maoni ya watu wengi sana ambao walishindwa kuelewa au walielewa nusunusu ile video ya kale ka kijana ka mkulu aliepita kwamba "tutawala hata miaka 200".... dogo alimaanisha CCM ni mfumo na ni itikadi.
 
Mhe. Magufuli hana haja ya kufanya kampeni ya hasara elfu 2020, kwakupitia vyombo vya habari ataomba kura. Hakuna haja ya kuzurura kuomba kura wakati utendaji wake unaeleweka.
 
hayo ni maneno ya kujifariji tu nyie ukawa/ukiwa lakini ukweli unabaki palepale kuwa magufuli ni rais kupitia ccm na 2017 ndo mwenyekiti wa ccm.


Ndugu zangu mtakumbuka kwamba wakati wa Kampeni, Rais John Pombe Magufuli, (JPM) alionekana kujitenga na chama chake cha CCM. ukiachia magwanda ya kijani aliyokuwa anayavaa (ambayo sijamuona kuyavaa tena toka ameapishwa), kauli zake, vibwagizo, vyote vililenga kujenga hoja kwamba siyo CCM inayoomba kura bali ni MAGUFULI. "SERIKALI YA MAGUFULI" , "CHAGUA MAGUFULI". Matarajio ya wengi, nadhani hata wanaccm, ni kwamba kwa kuwa CCM imechafuka mbele ya wananchi, ni sawa kuiweka pembeni kwanza, lakini mara ingetokea akawa mshindi, basi CCM ingechukua nafasi yake kama kawaida.

Baada ya kuapishwa, Magufuli hakuonesha jitihada ya pekee kujishughulisha na CCM, na katika hatua zake za mwanzo ambapo alifanya ziara kadhaa za ghafula, akatoa hotuba ya bunge ambapo alimshambulia waziwazi mtangulizi wake, rais mstaafu Jakaya Kikwete, ambaye alimbatiza jina la "mzee wa maisha bora" (kejeli?) tena kwa takwimu kuhusu safari zake za nje. hili lilikuwa jambo ambalo wapinzani na wanaharakati walilipigia kelele sana lakini CCM na serikali yake walitetea kwamba safari hizi zina tija. kurugenzi ya mawasiliano ikulu ilifanya kazi yake kutetea hili kwa nguvu zote. sasa leo Rais JPM analisema mbele ya vigogo wa ccm, na JK mwenyewe, tena kwa kusisitiza kwamba hataki kuwa mnafiki, ilikuwa ni ngumi nzito sana siyo kwa JK tu bali kwa CCM pia.

Tumeshuhudia hali ya ubaridi usio wa kawaida kwa upande wa CCM. tulizoea kuona kauli za kupongeza na maandamano ya kuunga mkono. safari hii kimya. lakini kilichonifanya kutoa mchango wangu kwenye hili jambo, ni ile hotuba ya Rais JPM kwa wafanyabiashara jana. wakati pekee ambapo aliitaja CCM, ilikuwa ni katika mabaya. ni pale alipokuwa anaeleza kuhusu ufisadi katika ubinafsishaji wa viwanda kule Morogoro, ambapo alisema kwamba viongozi wa CCM walihusika katika ubinafsishaji huu ambapo viwanda vimegeuzwa mahali pa kulala mbuzi. Hii hali ya kutoitaja kabisa CCM, au inapobidi aitaje, basi anaitaja katika mabaya, inanikumbusha mgomo wa wanahabari kwa aliyekuwa katibu mwenezi wa CCM wakati huo, na waziri wa mambo ya ndani, Ramadhani Mapuri (sijui yuko wapi siku hizi). wanahabari waliamua kususa kuandika habari yoyote kuhusu Mapuri, isipokuwa tu pale itakapokuwa ni habari mbaya! ilibidi msemaji wa CCM awe Mangula wakati huo kama sikosei, aliyekuwa katibu mkuu.

Katika hotuba yake kwa wafanyabiashara, kuna wakati amesisitiza kwamba serikali ipo, na kwamba serikali hii - (siyo ya CCM, bali ) ni ya JPM. hiyo ilikuwa ni ngumi nyingine kwa CCM. kwamba amekusudia kujitenga kabisa na CCM kadiri anavyoweza. na kusisitiza zaidi hilo, akasema pia kwamba hakuchukua fedha ya mfanyabiashara yoyote. sasa mimi sina hakika kama wale waliokuwa wanabandika matangazo walitumia fedha kutoka wapi. fulana na kofia zilitoka wapi. na je, kampeni yake aligharimia yeye mwenyewe? maana kama ni chama kiligharimia, kuna uhakika gani kwamba wafanyabiashara na wengine hawakupenyeza rupia zao? lakini la muhimu ni kwamba hata kama hayo yalifanyika, yeye hayatambui na hii siyo serikali ya CCM bali ni ya JPM. kwa maana hiyo, hata kama kuna vigogo katika CCM walipokea fedha kwa ajili ya kampeni, ili baadae wakikaa kugawana nyama ya mzoga, wapate mgao wao, basi imekula kwao. JPM hatambui hayo.

Ni kweli kwamba kwa kasi aliyonayo mpaka hivi sasa, Rais Magufuli anavifanya vyama vyote vya siasa kuonekana kama havina umuhimu, kikiwemo chama chake cha CCM. na kwa kutekeleza yale ambayo yalikuwa yanapigiwa kelele sana na vyama vya upinzani, anapunguza nguvu ya vyama hivyo, ambayo imekuwa ikikua kwa kasi miongoni mwa watanzania hasa kutokana na kiburi cha CCM.

sasa je, JPM anawezaje kujitenga kabisa na CCM? tuseme kikatiba na kisheria JPM ana wigo mpana kiasi gani kuiweka CCM pembeni? na CCM nayo je, itamwangalia tu bila kufanya mbinu za kumrejesha kundini? mahali ambapo CCM wanaweza kumkaba koo ni katika bunge. ambapo wabunge walio wengi wa CCM wanaweza kutaka "kumtia adabu". lakini hapo nadhani UKAWA wanaweza kugeuka na kumuunga mkono? lakini kwa uchaguzi tulioshuhudia, hivi kuna kundi linaweza kuthubutu kufanya kinyume na matarajio ya wananchi? naomba tujadili.
 
Kiukweli wapinzani tulikuwatunataka haya ambayo Dr wa ukweli JPM anafanya, siyo kama alivyobolonga yule Dr wenu wa kichina. Kazi kuchekacheka tu hata kwenye mambo mazito kitaifa.
 
Kichekesho! mnajitahidi kumtenganisha JPM na CCM kwa hoja zilizooza, JPM si kiongozi wa CCM hivyo hawezi kuzungumzia siasa. Ilani ilimwelekeza apambane na ufisadi na kutekeleza yote yaliyomo kwenye ilani, na hayo ndio anafanya bila kujali nani kitamgusa.
SASA NYINYI CDM MMECHANGANYIKIWA NA MMEKUWA SHOCKED kwa sababu mliaminisha watu kuwa mfumo (wanamtandao) hatauweza, mlikosea. Lowasa ndio anaamini siasa za mtandao.
 
Magufuli nje ya CCM hayuko salama. Kama tulivyosema wakati ule, Lowasa nje ya CCM si salama. Matokeo yake mliyaona.
 
Jaman acheni kuongea kama mpo usingizin, maguful hawezi kuitosa ccm ni figisu tu hizo.
Huu ni mchezo wa kisiasa tu, tena huyo magufuli atasimamia mambo yanatotendeka saizi tu lakin uozo, ufisadi, na mikataba mibovu iliyokwisha sainiwa hataweza kabisa kuvigusa.
kuna watu wanaota kuwa magufuli atamuwajibisha Riz1 na jk hilo wasahau.
Bado jamaa anakihitaji chama kuliko mamlaka aliyonayo kama kiongozi.
NAJUA WENGINE MTAPINGA LAKIN MTANIKUBALI PINDI KASHIFA ZINAZOWAHUSU WAKUBWA WA CCM ZIKIANZA KUIBULIWA NA WAPINZAN BUNGENI.
 
Inaonekana ndiko anakoelekea haswa. wengi tuliona ni nguvu ya soda. lakini dalili zinaonesha siyo nguvu ya soda. inavyoonekana kitakachoamua mustakabali wa mwelekeo wa baadaye wa JPM ni matokeo ya mtanange wake na CCM. atakayeibuka mshindi ndio ataendelea kutoka hapo, na hapo ndio wapinzani wataingia kazini. akishinda JPM, watalazimika kujiunga naye. wakishinda CCM-ufisadi, basi wapinzania watarudi vitani kupambana. kwa sasa hivi kuna wingu nene kwa hiyo kisiasa kuna utata

Mkuu nimekukubali
 
Back
Top Bottom