Magufuli ataweza kuitosa CCM?

Magufuli ataweza kuitosa CCM?

Mindi

JF-Expert Member
Joined
Apr 5, 2008
Posts
3,523
Reaction score
4,998
Ndugu zangu mtakumbuka kwamba wakati wa Kampeni, Rais John Pombe Magufuli, (JPM) alionekana kujitenga na chama chake cha CCM. ukiachia magwanda ya kijani aliyokuwa anayavaa (ambayo sijamuona kuyavaa tena toka ameapishwa), kauli zake, vibwagizo, vyote vililenga kujenga hoja kwamba siyo CCM inayoomba kura bali ni MAGUFULI. "SERIKALI YA MAGUFULI" , "CHAGUA MAGUFULI". Matarajio ya wengi, nadhani hata wanaccm, ni kwamba kwa kuwa CCM imechafuka mbele ya wananchi, ni sawa kuiweka pembeni kwanza, lakini mara ingetokea akawa mshindi, basi CCM ingechukua nafasi yake kama kawaida.

Baada ya kuapishwa, Magufuli hakuonesha jitihada ya pekee kujishughulisha na CCM, na katika hatua zake za mwanzo ambapo alifanya ziara kadhaa za ghafula, akatoa hotuba ya bunge ambapo alimshambulia waziwazi mtangulizi wake, rais mstaafu Jakaya Kikwete, ambaye alimbatiza jina la "mzee wa maisha bora" (kejeli?) tena kwa takwimu kuhusu safari zake za nje. hili lilikuwa jambo ambalo wapinzani na wanaharakati walilipigia kelele sana lakini CCM na serikali yake walitetea kwamba safari hizi zina tija. kurugenzi ya mawasiliano ikulu ilifanya kazi yake kutetea hili kwa nguvu zote. sasa leo Rais JPM analisema mbele ya vigogo wa ccm, na JK mwenyewe, tena kwa kusisitiza kwamba hataki kuwa mnafiki, ilikuwa ni ngumi nzito sana siyo kwa JK tu bali kwa CCM pia.

Tumeshuhudia hali ya ubaridi usio wa kawaida kwa upande wa CCM. tulizoea kuona kauli za kupongeza na maandamano ya kuunga mkono. safari hii kimya. lakini kilichonifanya kutoa mchango wangu kwenye hili jambo, ni ile hotuba ya Rais JPM kwa wafanyabiashara jana. wakati pekee ambapo aliitaja CCM, ilikuwa ni katika mabaya. ni pale alipokuwa anaeleza kuhusu ufisadi katika ubinafsishaji wa viwanda kule Morogoro, ambapo alisema kwamba viongozi wa CCM walihusika katika ubinafsishaji huu ambapo viwanda vimegeuzwa mahali pa kulala mbuzi. Hii hali ya kutoitaja kabisa CCM, au inapobidi aitaje, basi anaitaja katika mabaya, inanikumbusha mgomo wa wanahabari kwa aliyekuwa katibu mwenezi wa CCM wakati huo, na waziri wa mambo ya ndani, Ramadhani Mapuri (sijui yuko wapi siku hizi). wanahabari waliamua kususa kuandika habari yoyote kuhusu Mapuri, isipokuwa tu pale itakapokuwa ni habari mbaya! ilibidi msemaji wa CCM awe Mangula wakati huo kama sikosei, aliyekuwa katibu mkuu.

Katika hotuba yake kwa wafanyabiashara, kuna wakati amesisitiza kwamba serikali ipo, na kwamba serikali hii - (siyo ya CCM, bali ) ni ya JPM. hiyo ilikuwa ni ngumi nyingine kwa CCM. kwamba amekusudia kujitenga kabisa na CCM kadiri anavyoweza. na kusisitiza zaidi hilo, akasema pia kwamba hakuchukua fedha ya mfanyabiashara yoyote. sasa mimi sina hakika kama wale waliokuwa wanabandika matangazo walitumia fedha kutoka wapi. fulana na kofia zilitoka wapi. na je, kampeni yake aligharimia yeye mwenyewe? maana kama ni chama kiligharimia, kuna uhakika gani kwamba wafanyabiashara na wengine hawakupenyeza rupia zao? lakini la muhimu ni kwamba hata kama hayo yalifanyika, yeye hayatambui na hii siyo serikali ya CCM bali ni ya JPM. kwa maana hiyo, hata kama kuna vigogo katika CCM walipokea fedha kwa ajili ya kampeni, ili baadae wakikaa kugawana nyama ya mzoga, wapate mgao wao, basi imekula kwao. JPM hatambui hayo.

Ni kweli kwamba kwa kasi aliyonayo mpaka hivi sasa, Rais Magufuli anavifanya vyama vyote vya siasa kuonekana kama havina umuhimu, kikiwemo chama chake cha CCM. na kwa kutekeleza yale ambayo yalikuwa yanapigiwa kelele sana na vyama vya upinzani, anapunguza nguvu ya vyama hivyo, ambayo imekuwa ikikua kwa kasi miongoni mwa watanzania hasa kutokana na kiburi cha CCM.

sasa je, JPM anawezaje kujitenga kabisa na CCM? tuseme kikatiba na kisheria JPM ana wigo mpana kiasi gani kuiweka CCM pembeni? na CCM nayo je, itamwangalia tu bila kufanya mbinu za kumrejesha kundini? mahali ambapo CCM wanaweza kumkaba koo ni katika bunge. ambapo wabunge walio wengi wa CCM wanaweza kutaka "kumtia adabu". lakini hapo nadhani UKAWA wanaweza kugeuka na kumuunga mkono? lakini kwa uchaguzi tulioshuhudia, hivi kuna kundi linaweza kuthubutu kufanya kinyume na matarajio ya wananchi? naomba tujadili.
 
Uchaguzi ukifanyika tena leo, nitampatia kura yangu, na hiyo ni kwasababu hadi sasa amefanikiwa 'kujitenga' na CCM.
Na ninaamini kuwa uchaguzi ukifanyika hivi sasa atapata upinzani mkubwa sana ndani ya CCM na ikitokea ukaitishwa basi upinzani utajiweka kando na kumuunga mkono na hivyo kupita bila kupingwa. Tofauti na hapo labda CCM ijimege tena halafu wale watakaokatwa waende Upinzani eg ACT, ili kupambana naye.
 
CCM nawavimbe wapasuke watajijua wenyewe, acha waisome namba eenh Magufuli mbele kwa mbele , ule wimbo tafadhali waubadilishe uimbike hivi
 
Usiamini sana CCM Tegemea usicho kitarajia. Ni watu wa level nyingine kabisa. Yanabadilika kulingana na upepo kama Nepi
 
Ccm in ile ile maoni yangu in kuwa panatengenezwa mazingira tu na sehem muhim ya kutengeneza" dili" ni bandari na makusanyo ya kodi wale majizi sugu wanaangalia upepo unapovuma tu.Wapo walioanza zaid ya hivyo na matokeo take wakachukuwa ( kiwira) kwa being ya kutupa
 
Uchaguzi ukifanyika tena leo, nitamoatia kura yangu, na hiyo ni kwasababu hadi sasa amefanikiwa 'kujitenga' na CCM.
Na ninaamini kuwa uchaguzi ukifanyika hivi sasa atapata upinzani mkubwa sana ndani ya CCM na ikitokea akaoitishwa basi upinzani utajiweka kando na kumuunga mkono na hivyo kupita bila kupingwa. Tofauti na hapo labda CCM ijimege tena halafu wale watakaokatwa waende Upinzani eg ACT, ili kupambana naye.
Lowassa alipo katwa alienda wapi

Sumaye alipo katwa alienda wapi

ACT si Chama cha MAZUZU
 
naona sasa hivi mmeanza kumpotezea Lowasa hahaha
 
Mtu akiangalia kwa makini atagungua kuwa Uchaguzi huu CCM imeshindwa ila Magufuli (personal) ameshinda. Hata upinzani mtu waliye msimamisha (Lowasa na wengine) wameshindwa ila makusudio yao yameshinda. Maana yale yote waliyokuwa wanataka yameanza kufanyiwa kazi.
Ki ukweli CCM kama chama wameshindwa na kubaki na mshangao thats why wako kimya huku wakipigwa huku na kule.
Kauli ya jana ya JPM kuhusu Coco beach na kurudia tena kuwa hii ni serikali ya Magufuli (sio ya ccm) ni ishara kuwa HAWATAKI TENA CCM
 
naona sasa hivi mmeanza kumpotezea Lowasa hahaha

Tunajenga nchi hatumjengi mtu individual, hata Mgwira angeshinda na kufanya yale Watz wanataka tungemuunga mkono.
Wewe uchaguzi umeisha bado una ndoto za kichama? Hata JPM Akikosea bado atapewa za uso tuu
 
baada ya siku mia moja kuisha ndo tutaijua sura halisi ya magu
 
Mtu akiangalia kwa makini atagungua kuwa Uchaguzi huu CCM imeshindwa ila Magufuli (personal) ameshinda. Hata upinzani mtu waliye msimamisha (Lowasa na wengine) wameshindwa ila makusudio yao yameshinda. Maana yale yote waliyokuwa wanataka yameanza kufanyiwa kazi.
Ki ukweli CCM kama chama wameshindwa na kubaki na mshangao thats why wako kimya huku wakipigwa huku na kule.
Kauli ya jana ya JPM kuhusu Coco beach na kurudia tena kuwa hii ni serikali ya Magufuli (sio ya ccm) ni ishara kuwa HAWATAKI TENA CCM
Mkuu umepiga penyewe!! Sasa tunasuburi kuona vikao vya CCM kama vitajaribu kumpungza speed kama vitafaninkiwa.

Hawa mafisadi papa wengi wao ni wadau wakuu wa CCM na sasa wamekalia kaa la moto - kweli nii ni SERIKALI YA MAGUFULI.
 
Mnawaza kama mko usingizini. Hamjui kisiasa chama kiko juu ya Magufuli? anyway.
 
Mtu akiangalia kwa makini atagungua kuwa Uchaguzi huu CCM imeshindwa ila Magufuli (personal) ameshinda. Hata upinzani mtu waliye msimamisha (Lowasa na wengine) wameshindwa ila makusudio yao yameshinda. Maana yale yote waliyokuwa wanataka yameanza kufanyiwa kazi.
Ki ukweli CCM kama chama wameshindwa na kubaki na mshangao thats why wako kimya huku wakipigwa huku na kule.
Kauli ya jana ya JPM kuhusu Coco beach na kurudia tena kuwa hii ni serikali ya Magufuli (sio ya ccm) ni ishara kuwa HAWATAKI TENA CCM

Definitely!!!
 
Tunajenga nchi hatumjengi mtu individual, hata Mgwira angeshinda na kufanya yale Watz wanataka tungemuunga mkono.Wewe uchaguzi umeisha bado una ndoto za kichama? Hata JPM Akikosea bado atapewa za uso tuu
Kama mlikuwa mnajua hayo kwanini mlishupalia uozo kwanini hamkupenda kuhoji uhalali wa lowassa na cdm, kwanini hamkutaka ajenda ya ufisadi kuzungumzwa tena, mkubari lichama lenu limevamiwa na mnaongozwa na umimi na umungumtu
 
Sijui katiba yasema je but nauhakika 2020 ccm hawatampitisha huyu.jamaaa
 
hata iwaje JPM hamuwezi kumtenga na Ccm! MTU anasema mbona hajaongea mazur ya Ccm! hiv Magufuli bado anafanya kampeni? kinacho endelea in reforms ndan ya chama hayo mambo yako planed.
Chagua Magufuli mwingine anasema Mabadiliko Lowassa mbona hamkuona anajitenga na chadema?
siasa in sayansi soma upepo na akili za watu! watu wanataka mabadiliko, chama makin hubadilika kama walivyo Fanya Ccm
Niujinga kuendesha propaganda za kumtenga JPM na Ccm
 
ccm hawana jeuri ya kumkata magufuli 2020, katiba inasema lazima mara mbili, yaani wamekoma siyo kidogo sana.
 
naona sasa hivi mmeanza kumpotezea Lowasa hahaha

Hata uchaguzi ukirudiwa kesho nitampigia lowassa. Kwani huyu magufuli si ni kawaida yake akiingia wizara yoyote anaingia kwa mikwara. Baadae watu wanapiga kawaida tu. Mwaka huu huu watu wa wizara yake ya ujenzi walipiga billion 262 na yeye akiwepo
 
hata iwaje JPM hamuwezi kumtenga na Ccm! MTU anasema mbona hajaongea mazur ya Ccm! hiv Magufuli bado anafanya kampeni? kinacho endelea in reforms ndan ya chama hayo mambo yako planed.
Chagua Magufuli mwingine anasema Mabadiliko Lowassa mbona hamkuona anajitenga na chadema?
siasa in sayansi soma upepo na akili za watu! watu wanataka mabadiliko, chama makin hubadilika kama walivyo Fanya Ccm
Niujinga kuendesha propaganda za kumtenga JPM na Ccm
SASA utake usitake JPM anatekeleza Sera za Wananchi ambao ndiyo wapinzani wa ccm, nyerere alisema ndani ya ccm wapo,watu wanaoipenda nchi hii, wapo wapo wazuri wanaochukia Rushwa kwa dhati toka moyoni,"Sasa ndiyo Magufuli Mungu asante" Mkapa Kikwete kaa chonjo saa mbaya hii, hasa ZILE NYUMBA MLIZOUZA KWA BEI YA KUTUPA. HUYU JOM HANA CHAMA ILA ANA UTAIFA
 
Back
Top Bottom