makundubhyali
JF-Expert Member
- May 26, 2013
- 2,389
- 882
Ameahidi atakapoingia madarakani, atahakikisha kuwa mafisadi wote wanashughulikiwa bila woga.
Mgombea Urais wa CCM, Dk. John Pombe Magufulu akizumgumza katika mkutano wa kampeni
Mgombea urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. John Magufuli, amesema mafisadi wamo hadi ndani ya chama chake na ndiyo maana baada ya kuteuliwa kuwa mgombea urais wengi wao wameanza kuweweseka kutokana na hofu kubwa waliyo nayo dhidi yake.
Akizungumza kwa nyakati tofauti katika mikutano ya kampeni ya chama chake mjini Kisarawe, Pwani na baadaye Ukonga, jijini Dar es Salaam jana, Magufuli alikiri kuwa chama chake kiliwalea walarushwa na mafisadi kwa muda mrefu na ndiyo maana baadhi ya watu walianza kukichukia.
Hata hivyo, alisema tatizo hilo halitakuwapo tena kwani atakapoingia madarakani baada ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25, atahakikisha kuwa mafisadi wote wanashughulikiwa bila woga.
Ndugu zangu, nasema kweli mafisadi hawako upinzani tu... ni ngumu sana mtu aliye ndani ya CCM kuyasema haya, lakini lazima niseme ukweli maana msemaukweli ni mpenzi wa Mungu. Haya mafisadi ndiyo yametufikisha hapa na (sasa), lazima tuyashughulikie, alisema Magufuli na kushangiliwa na wananchi waliojitokeza kwenye mkutano wake wa Ukonga.
Magufuli aliwataja kwa sifa za jumla mafisadi waliopo kuwa ni pamoja na baadhi ya viongozi wa serikali, ambao hujihusisha na vitendo vya rushwa na dhuluma dhidi ya wananchi kiasi cha kuifanya serikali ichukiwe na baadhi ya wananchi wake.
Akitolea mfano, Magufuli alisema ni aibu kuona serikali ikikimbizana na mamalishe na wafanyabiashara ndogondogo (Wamachinga) ili kupata kodi wakati kuna baadhi ya nchi ambazo zinaendeshwa kwa mapato ya bandari tu.
Magufuli aliongeza kuwa anatambua wananchi wamekuwa wakinyanyaswa katika maeneo mbalimbali ikiwamo kutozwa kodi zisizosaidia kuinua pato la taifa bali kuwafaidisha baadhi ya viongozi na kwamba, kwa sababu hiyo, haoni sababu ya kuendelea kwa hali hiyo hasa kwa kujua kuwa kuna nchi zinajiendesha kwa mapato ya bandari.
Alisema yote hayo ni baadhi ya mambo anayoamini kuwa ni sababu ya yeye kuchaguliwa kuwa rais ili kudhibiti uonevu kwa wanyonge na pia kupambana na mafisadi serikalini, ambao wamezoea kuishi kwa rushwa na ulaghai.
Kwa mfano, alisema anajua namna ambavyo baadhi ya watumishi bandarini huruhusu makontena kupita bila kulipiwa ushuru na kuikosesha serikali mapato yake ili kuwahudumia wananchi.
Wapo watu wanaikosesha serikali mapato. Hawa nataka nikapambane nao... na nitapambana nao kweli kweli. Na hawatanikwepa najua wananiogopa na wameanza kumwaga hela ili nishindwe. Nyinyi hela zao kuleni maana ni kodi zenu, lakini kura ni kwa Magufuli, alisema.
K/K
Sasa wanaCCM wanaokuwa wanabwabwaja humu kuwa mafisadi wamekimbia CCM hebu tuelezeni ninyi na magufuri nani mwongo