Uchaguzi 2020 Magufuli asifia utendaji wa Anna Mghwira

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,007
9,873
DKT. MAGUFULI AMSIFIA UTENDAJI WA ANNA MGHWIRA

Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM ambaye pia ni Rais wa Tanzania amesifu utendaji wa Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Anna Mghwira

Dkt. Magufuli amesema Mama Anna Mghwira alikuwa mgombea Urais wa upinzani katika Uchaguzi Mkuu wa 2015 lakini alifanya siasa safi kwa kunadi sera za chama alichokuwa bila kutukana mtu, hali iliyopelekea kumteua kuwa Mkuu wa Mkoa

Amesema tangu amemteua kuwa Mkuu wa Mkoa, Anna Mghwira amekuwa mmoja kati ya wakuu wa mikoa wanaofanya kazi vizuri

Aidha amesisitiza kuna maisha baada ya Uchaguzi hivyo hakuna haja ya kuwa na matusi kwa vyama vingine kwa kipindi hiki cha kampeni
Magu.JPG
 
Mkuu Rekebisha hapo huyo ni mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro alikua na guts ya kumsema yule dogo mwenye mihemko Ole Sabaya.
 
Kwahiyo zawadi ya kutotukanwa ni kuwatunuku ugavana!?
Bora tu tuendelee na SPANA zetu munazoziita "Matusi"
 
Lissu alishasema hataki kazi ya mkuu wa mkoa! Sasa mafumbo kama haya hayasaidii chochote Magu ataondoka tu baada ya muda? Kuna tofauti sana Lissu anapigia kelele haki sio kuajiriwa
 
Huyu mama katuwekea mkosi Act saivi kila tunayemzamini urais lazima akimbie

😁😁😁😁 mugah di mathew shida sio huyu mama. Shida ni mmiliki wa wa chama chenu. Membe hajakimbia ila zito ndio kamkimbia membe

Fikiria kilichomfanya amchague membe ni nini na kilichomfanya ampotezee ni nini
 
Ni mkosi wa huyu mama ninae mjua toka kipindi hicho 90's years ihanja singida sio mtu wa kumuamini kihivyo ila juu ya membe ni usaliti kama walikubaliana wapime upepo waone ni nani anakubalika yeye hajaonaa?
 
Unajua was wanasema walikuabaliana wapime upepo ila mimi na wewe hatuwezi kuthibitisha kama kweli kulikua na hayo makubaliano.
Siasa ni mambo mengi mno.
 
Unajua was wanasema walikuabaliana wapime upepo ila mimi na wewe hatuwezi kuthibitisha kama kweli kulikua na hayo makubaliano.
Siasa ni mambo mengi mnooo
Ila hata sisi wanachama tupo nyuma ya Lissu hatumwamini Ccm yeyote hata kama amevaa shati la purple
 
Tangu lini mwanadamu muungwana akachukua ushauri toka kwa shetani.

Magufuli ameteka, ameuwa, ametukana na kufokea watu kwa miaka 5 halafu leo anajitia kutoa nushauri? Nani atamsikiliza?
 
Ila hata sisi wanachama tupo nyuma ya Lissu hatumwamini Ccm yeyote hata kama amevaa shati la purple

Tatizo na tofauti zetu ndio ziko hapo kwenye imani😁

CHADEMA mnamuona na kumuamini Tundu ila sisi tunawaona kina Amstadamz wakiwa nyuma ya Tundu tena wakiangalia rasilimali zetu kwa uchu wa ajabu

CCM wanamuona na kumuanini John Pombe Magufuli huku nyuma yake wakiona umeme vijiji, barabara, reli, elimu, mahospitali, kilimo bora, viwanda na mengine mema
 
Nyuma ya Ccm na magufuli kuna China akiangalia pembe za ndovu,gesi na tenda za vivuko vya barabara. Pia kuna Egypt akipalilia tenda ya rufiji dam construction huku akiuhujumu mradi wa lake Victoria water supply.

Pia kuna uturuki na reli yao huku wakiwaza kutuweka kuwa chini ya upcoming ottoman empire. Mwisho kuna USA na Canada hawa wanafurahia mikataba minono ya accacia iliosainiwa white house na vile vile jiwe ndiye bwege pekee dunia yote anaepigwa pesa ndefu na Boeing katika ununuzi wa dreamliner
 
Nyuma ya Ccm na magufuli kuna China akiangalia pembe za ndovu,gesi na tenda za vivuko vya barabara. Pia kuna Egypt akipalilia tenda ya rufiji dam construction huku akiuhujumu mradi wa lake Victoria water supply...

Hizo ni biashara sio sawa na kuweka madini dhamana eti ili chadema wapate pesa ya kuendesha nchi
 
Back
Top Bottom