Magufuli ashindwa kuhutubia Misungwi

General Mangi

JF-Expert Member
Joined
Dec 21, 2013
Posts
15,316
Reaction score
23,187
Leo mgombea wa ccm Dr Magufuli hakuhutubia jukwaan katika jimbo la misungwi zaidi ya kelele za wasanii.

Magufuli alifika na kupanda jukwaani lakini alipokuwa anatumbuiza fid Q tulishangaa kasimama na kuondoka bila hata kusalimia.

Jambo hili lilisababisha watu wazomee, na hata alipokuwa anaimba fid Q alizomewa pia na kundi la watu nyuma.

Sababu nilisikia kwa mbali kwani nilikuwa nyuma kwamba sijui anawahi kwenda wapi hukoo
 
Fafanua zaidi mkuu, nini kilisababisha pombe asihutubie?
 
Kwani lazima use me uwongo? UKAWA MMEKUWA UKIWA
 
Hakuna kapicha kidogo katuburudishe?
 
Sawasawa
 

Siku nyingine mkipewa vimemo, someni vizuri kabla ya kubandika hapa. Mkutano wa Misungwi ulioneshwa LIVE! Hayo uliyoandika ni madharau kwa wanajukwaa hili.
 
Fafanua zaidi mkuu, nini kilisababisha pombe asihutubie?

mkuu siwezi jua, kwani mm nilishangaa anaondoka, bila kuhutubia, sijui tatizo lilikuwa nn kwani walisema anawahi sijui wapi hukoo
 
Wewe ni muongo mkubwa missungwi magufuli amehutubia na kuwanadi madiwani na mbunge wao maarufu kama mawe matatu, pia alimkaribisha mbunge mstaafu shibiriti na mikutanoni palijaa maelfu ya watu Acha kupotosha umma
 
Siku nyingine mkipewa vimemo, someni vizuri kabla ya kubandika hapa. Mkutano wa Misungwi ulioneshwa LIVE! Hayo uliyoandika ni madharau kwa wanajukwaa hili.

nilimwona live mida ya 17:30 hivi japo sikufuatilia. na pale ndo kwao na mke wake
 
Mbona tulikuwa tunaona live Star TV na Magufuli alinanidiwa na mtu aliyemdhamini kwa mara ya kwanza kuingia mjengoni
 
Magufuli yuko katika wakati mgumu sana kutokana na ahadi lukuki ambazo hqzikutekelezwa zilizotolewa na mtangulizi wake!
 
Sasa yule tuliyekuwa tukimuona Star TV akihutubia alikuwa ni nani?
 
Duh! Hii hatari sasa, kama watu wako tayari kusema uongo mchana kweupe. Mkutano wa magufuli ulioneshwa live Star TV. Kila aliyeangalia ameona magufuli akihutubia ikiwa pamoja na kuwanadi Wagombea ubunge wa kuchaguliwa (Kitwanga) na viti maalum. Kisha akamwita somebody Shibiriti (kama jina nimelipata vizuri). Sasa hizi habari hakuhutubia misungwi mnatoa wapi ndugu zangu ukiwa, mbona mnaleta siasa za uongo kwa kiwango kikubwa hivi. Mna lengo gani kama si kuchochea uovu?
 
Wewe ni muongo mkubwa missungwi magufuli amehutubia na kuwanadi madiwani na mbunge wao maarufu kama mawe matatu, pia alimkaribisha mbunge mstaafu shibiriti na mikutanoni palijaa maelfu ya watu Acha kupotosha umma


acha uongo mbona wanasema hata startv ilikata matangazoo?? uliza kwa waliokuwa karibu na Tv
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…