Magufuli apiga STOP Safari za nje ya Nchi; Elimu Bure kuanza Januari 2016...

Ndivyo inavyokuwaga mwanzo, mwishoe ataisoma namba mwenyewe.

Yap. Anapenda sana publicity huyu Ngosha. Nchi haiendeshwi kama wizara kwa kukurupuka, kupigwa picha na kupigiwa makofi kwa kudhalilisha watendaji hadharani kama ilivyotokea jana wizara ya Fedha.Very soon ataisoma namba yeye mwenyewe. Tunataka mikakati siyo misifa ya kufoka mbele ya kamera.
 
UKAWA maswali yenu ya ajabu jibu ni hili rais mpya alipoapishwa baraza la mawaziri la Kikwete nalo lilimaliza muda wake.

wanaposema kuvunjwa kwa baraza la mawaziri usifikiri wanavunja kwa kutumia nyundo.

Wewe kweli kitulo, ni kule kitulo ambako huwa hamlioni jua mara kwa mara? Lazima akili igande, baraza la mawaziri lililopita lilikoma pale iliposhushwa bendera ya Rais
 
Watu kama wewe ni jamii ya mashetani, kwani shetani ndie asiyependa zuri lolote kwa mwanadamu.

Rais ndio kwanza ameanza kazi ,nyie mshaanza kumuombea ashindwe. Akifanikiwa matunda ni ya watanzania wote, sioni sababu ya kwanza fitina.

Waache hao hawa amini bado wana weweseka
 
Mungu akutangulia Rais wetu ktk utendaji wako, akuzidishie akili na maarifa, afya njema na maono mapana kwa taifa letu, ujasiri na uchapakazi. endelea na speed yako hiyo na mungu akutangulie nasi watanzania wenye nia njema na taifa letu tuko nyuma yako tunakuombea kila siku. God be with you our presidend
 
Yap. Anapenda sana publicity huyu Ngosha. Nchi haiendeshwi kama wizara kwa kukurupuka, kupigwa picha na kupigiwa makofi kwa kudhalilisha watendaji hadharani kama ilivyotokea jana wizara ya Fedha.Very soon ataisoma namba yeye mwenyewe. Tunataka mikakati siyo misifa ya kufoka mbele ya kamera.

Inaonekana ww Jana yamekukuta pale wizara ya fedha kwa taarifa nilizonazo umeachishwa kazi , nyodo zote peleka kishimundu

Hapa kazi tu
 
Kama anataka kufufua viwanda athibiti kodi inayokwepwa bandarini. Hiyo itafanya bei ya bidhaa zinazoshindana na zinazalishwa nchini kuwa kubwa hivyo walaji watanunua za nchini. Mfano halisi ni kanga na kitenge. Aweke sera za makusudi za kuzuia bidhaa zenye uwezo wa kuzalishwa nchini kuingizwa ovyo ovyo. Vinginevyo ufufuaji wa viwanda utakuwa ndoto.
 
Inaonekana ww Jana yamekukuta pale wizara ya fedha kwa taarifa nilizonazo umeachishwa kazi , nyodo zote peleka kishimundu

Hapa kazi tu
Mtumishi wa umma haachishwi kazi kihivyo. Rais mwenyewe ni mtumishi wa umma
 
Ni vyema kukutana nao so that you share your strategies and way forward na wajue what are your plans and actions.
 
Kama mikutano ndo kasi na viwango waliomtangulia mbona wangetisha?? Mikutano si tija, aelekeze anachokitaka kifanyike tu. Walikaa mahoteli makuubwa ya Ngurdoto lakini mwisho wa siku tuliona kilichotokea. Akumbuke maneno yake mujarab; HAPA KAZI TU sio vikao na kutembeleana ofisini. Hiyo ni kazi ya tarishi tuuuu

Punguza mahaba ya kijinga, utafanya kazi bila kikao
 
Kila mtu anataka kuwa rais, si mngegombea basi? John Pombe Magufuli ana mkakati wake ndio sababu ya kugombea, mnataka kumchagulia kila kitu, mwacheni aongoze nchi pambaf kabisa.
 
sasa Makatibu Wakuu ndio watendaji wakubwa kabisa serikalini, kama watanzania ni maskini hawa jamaa ndio wakuwahoji, mtu yeyote mwenye cheo juu ya makatibu ni msimamia sera wa chama tawala.

ni vizuri Raisi aongee nao, ili waelewe hilo, sio kunywa chai na kuwasubiri mawaziri atapangiwa wizarani kwao ili walumbane naye/nao.

Watanzania wako hapa waliko baada ya miaka 54 ni kwasababu ya Makatibu Wakuu sio sera za CCM, NCCR wala CUF.
 
Magufuli jembe na kiongozi kweli kweli, anaenda kujionea mwenyewe siyo kusubiri kuletewa taarifa
 
Back
Top Bottom