Magufuli apiga STOP Safari za nje ya Nchi; Elimu Bure kuanza Januari 2016...

UKAWA maswali yenu ya ajabu jibu ni hili rais mpya alipoapishwa baraza la mawaziri la Kikwete nalo lilimaliza muda wake.

wanaposema kuvunjwa kwa baraza la mawaziri usifikiri wanavunja kwa kutumia nyundo.

Mkuu, Kidogo kidogo wataelewa . Kumwelimisha nyumbu shughuli yake pevu. Hivi kweli mtu anaulizia kuvunja baraza la mawaziri wakati JK yupo Msoga?
 
Kwani hao makatibu wakuu wapo mpaka lini? Au hao wa awamu ya 4 ndio haohao wataendelea? kama sivyo......
 
ingekua mm ningeanza na kushughulikia Zanzibar ili seif apewe haki yake mapema
 
Kwani hao makatibu wakuu wapo mpaka lini? Au hao wa awamu ya 4 ndio haohao wataendelea? kama sivyo......

makatibu wakuu in watumishi/waajiriwa wa serekali ni kama watumishi wengine vyeo vyao vinaendelea labda abatilishe Kwa sababu maalum. na sikwamba wa jk katoka nao!
 
Ana kasi ya ajabu!

Ni mapema mno kumjaji kwa sasa hivi mimi nasubiri mambo manne toka kwake ili niweze kumpima na kuona dira na mwelekeo wa utawala wake;-

1. Uteuzi wa Waziri Mkuu.
2. Uteuzi wa Baraza la Mawaziri.
3. Hotuba yake ya uzinduzi wa Bunge jipya ambayo itaelezea kwa kina dira yake ya maendeleo na mikakati kwa kipindi cha miaka mitano ijayo.
4. Siku mia moja za utawala wake tangu aingie madarakani.

Haya mambo manne yanatosha kabisa kujua nini mwelekeo wa utawala wake na matarajio ya wananchi toka kwake.
 
Back
Top Bottom