Magufuli aomba wananchi wamuombee

Magufuli aomba wananchi wamuombee

Mwiba

JF-Expert Member
Joined
Oct 23, 2007
Posts
7,607
Reaction score
1,760
Namshangaa sana Raisi mteule wa Tanganyika (Zanzibar uchaguzi umefutwa)anapowambia wananchi kuwa sasa anaona zile ahadi zake ni nyingi sana na kuzitekeleza itakuwa mtihani ,hivyo anaomba wananchi wote bila ya kujali itikadi zao wamuombee ili azikamilishe.

Nimefurahi kuona Magufuli ameshinda ili nione ni kwa jinsi gani atakamilisha ahadi lukuki vinginevyo wale waliompa kura milioni sita baada ya miaka mitano nao wataelewa kuwa ndani ya CCM huwezi kufanya kitu. :hand:
 
yeah!time will tell.baada ya mwaka mmoja tu kila mmoja ataanza kulalamika,na safari hii wasitegeme misaada kutoka US na kama maalim akishinda kuna uwezekano mkubwa sana uchaguzi ukarudiwa ili kumpata rais mpya wa tanganyika
 
Wamwombee kafanya nini? Yeye eti ni mlokole siajiombee? Wanasema ni chaguo la Mungu kwani Yesu aliombewa? Kwa kuwa kakubali kuibeba dhambi ya chama chake Na kafurahia kuwa Rais hatuna haja ya kumwombea wafu watazika wafu wenzao
 
Nyambafu.... makufuli aombewe yeye kama nani muhimu sana hapa nchinii???? Shezy taipu......
 
Mbona mnalialia? Rais ni Magufuli, acha afanye kazi yake. Wewe sasa ni kutii mamlaka yake tu. Kelele za nini. Wengi mlijilisha upepo kuwa mabadiliko mabadiliko, mara kuzungusha mikono, tukawaambia huyu JPM huwezi mshindanisha na mtu anayelazimisha kwenda Ikulu, mkakataa, yako wapi?
 
Hivi magufuli hana mtoto aliye humu jamii forum amwambie baba yake hapendwi
 
Mungu yupi anayesema wa herufi ndogo ama kubwa,, laana ya wananchi itamtafuna anakubali kupewa uongozi kupitia nyota ya mtu, robo tatu ya wapiga kura hawajamchagua,,
 
Hayo maombi yatapokelewa na nani?

Akalie kiti cha wizi atulie.
 
yeah!time will tell.baada ya mwaka mmoja tu kila mmoja ataanza kulalamika,na safari hii wasitegeme misaada kutoka US na kama maalim akishinda kuna uwezekano mkubwa sana uchaguzi ukarudiwa ili kumpata rais mpya wa tanganyika
Mkuu umewahi kusoma taarifa za CIA zilizo vuja kupitia WikiLeaks, basi kwa taarifa yako kiongozi wenu wa UKAWA Serikali ya Merikani inamjua vizuri kuliko unavyo fikiria, vile vile na maalim Seif wakijifanya kwenda kulalamika, Merikani watawasikiliza lakini watawapuuzia,kama maalim Seif na wafuasi wake walifikiri watapata ushindi kwa kuwatumia mamuluki wa IT kutoka Korea kusini basi hiyo imekula kwao.

Msijifariji, uchaguzi hauwezi kurudiwa Tanzania bara
 
It has not been phrased correctly. Analosema ni kwamba siyo kwamba yeye ameahidi vitu na watu wasubiri kuvipata . Ni kwamba maendeleo ya nchi ni kazi ya Watanzania wote. Everyone must do what he does best kwa maendeleo ya nchi. Kila mtu kufuatana na ujuzi wake,kipaji chake,na Rais ndie coordinator.Na swami la kwanza linalotakiwa kuulizwa na kila mtu na kujibiwa ni:saa nzuri ya kuamka asubuhi ni saa ngapi? Saa ya kwenda kulala ni saa ngapi?
 
Kwa hali hii Ijumaa, Jumamosi na Jumapili watu wanavaa kanzu na ma_suite makubwa huku mikononi wamebeba misaafu mikubwa wanaingia nyumba za ibada kwa kumshukuru Mungu, eti wameshinda, naona kejeli kwa Muumba wa mbingu na nchi.

Nilijifunza siyo kila kiongozi analetwa na Mungu wa mbinguni bali hata shetani anahusika kuwaweka baadhi ya viongozi.
 
It has not been phrased correctly. Analosema ni kwamba siyo kwamba yeye ameahidi vitu na watu wasubiri kuvipata . Ni kwamba maendeleo ya nchi ni kazi ya Watanzania wote. Everyone must do what he does best kwa maendeleo ya nchi. Kila mtu kufuatana na ujuzi wake,kipaji chake,na Rais ndie coordinator.Na swami la kwanza linalotakiwa kuulizwa na kila mtu na kujibiwa ni:saa nzuri ya kuamka asubuhi ni saa ngapi? Saa ya kwenda kulala ni saa ngapi?

Watanzania hata wakifanya kazi kwa bidii yote, kama serikali ya Magufuli itaendelea na mfumo huu unaoabudu mikataba mibovu ya wawekezaji, ufisadi, rushwa kwenye vyombo vya dola (polisi, mahakama, n.k), hakuna maendeleo yoyote yatakayokuja.
Magufuli anapaswa kujiuliza:-
Adui wa Tanzania ni nini ??
Akipata jibu, basi atumie nguvu zake zote kupambana na adui huyo..
Kikwete yeye alishajiamulia kuwa adui wake ni vyama vya upinzani...!!! Hivyo akapambana navyo badala ya kupambana na ufisadi.
 
Back
Top Bottom