Magufuli angejiuzulu ili kuweka sawa ushindani kwenye uwanja wa uchaguzi

mweongo

Member
Aug 23, 2010
62
228
Hakika Katiba na sheria zetu za uchaguzi haziweki uwiano kwenye chaguzi zitu. Ingefaa serikali ( Raisi na baraza lake la Mawazili) wajiuzuru pindi tu bunge linapovunjwa na nchi iwe chini ya uangalizi wa uongozi wa mpito kama vileJaji Mkuu na Wizara ziwe chini ya Makatibu wakuu.

Hali ilivyo sasa inasikitisha na inashangaza. Raisi ni Mgombea lakini ndio anaamrisha Tume ya Uchaguzi jinsi ya kuendesha uchaguzi, kama ilivyotokea wakati Magufuli akifungua jengo la Tume hiyo. Pia Magufuli alivielekeza vyombo vya usalama jinsi ya kusimamia uchaguzi. Mbaya zaidi Maguli aliwaonya na kuwaelekeza wagombea wenzake jinsi ya kuendesha kampeni zao la sivyo wakienda kinyume vyombo vyake vya usalama vitawashunghulikia.

Mgombea huyo wa Uraisi kwa tiketi ya CCM alitoa amri ya kuruhusu shughuli za kisisa kuanza kwa wanasisa wa vyama vingine. Maana yeye na wanachama wenzake hawakusitisha shughuli hizo. Ikumbukwe kuwa Magufuli alitoa amri ya kusitisha shughuli hizo pale tu alipochaguliwa mwaka 2015. Zaidi ya hapo Magulifuli alisema amri hiyo itarejelewa mara baada ya uchaguzi wa mwaka huu.

Upande mwingine, kwa mujibu wa sheria zetu Waziri mkuu na Mawaziri wote ni Wabunge na Bunge limeshavunjwa, inakuwaje wao bado wanaendelea na kazi za uwaziri?

Watanzania wenzangu, kwa sheria, taratibu na amri hizi tunaenda kwenye uchaguzi unaoitwa wa vyama vingi kama maigizo au kubahatisha tu. Maana wapinzani kushinda ni kwa hisani tu ya msimazi wa uchaguzi, ambae pia ni mteule wa mgombea wa CCM.

Ifike mahali watanzania tupaze sauti tubadilishe sheria hizi baguzi na kandamizi kwa ustawi wa Taifa letu.
 
Kwa hiyo tusiwe na Rais? Acha utoto wewe, toa mifano ya nchi inayofanya vile
 
Back
Top Bottom