simplemind
JF-Expert Member
- Apr 10, 2009
- 16,695
- 9,580
DK. JOHN Magufuli, mgombea urais kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM) siku hizi anabeba vikapu vingi vilivyojaa ahadi.
Hizi ni ahadi anazozitoa kwa taifa kwa atayoyafanya katika nyanja mbalimbali endapo atachaguliwa Rais pamoja na zile anazowapa wakereketwa wa CCM walioangushwa katika kura za maoni.
Akiwaomba wasikihame chama chao, Magufuli aliwaahidi ajira viongozi hao wa CCM walioangushwa katika kura za maoni za kuwachagua wagombea ubunge na uwakilishi (kwa upande wa Zanzibar).
Ahadi hizo, kwa kweli, ni kama ahadi za hongo na zinadhihirisha jinsi hali isivyo shwari ndani ya CCM. Kuna viongozi kadhaa katika ngazi za juu za CCM (majina tunayahifadhi) ambao wameahidiwa mengi ikiwa watastahamili wasijitoea kutoka chama hicho.
Habari tunazozipata ni kwamba kunafukuta chini kwa chini, ndani kwa ndani, na kwamba viongozi wanazidi kutoaminiana.
Uongozi wa juu kabisa unalaumiwa sana kwa namna kura za maoni zilivyoendeshwa na kwa uamuzi wa waziri mkuu wa zamani, Edward Lowassa, kukisusa chama hicho, chama kilichomlea na alichokitumikia tangu 1977.
Kuna wakereketwa wengi wenye kunungunika kwamba walionewa na vigogo wakati wa kura za maoni. Magufuli aliwabembeleza walioangushwa katika kura za maoni na aliwaahidi ajira alipokuwa akihutubia mikutano ya hadhara, Mkoa wa Songwe Agosti 26, mwaka huu.
Lakini Raia Mwema limeelezwa kwamba ahadi hizo za Magufuli zilikwishatolewa Unguja kama wiki moja na nusu kabla ya hapo katika vikao vya ndani vya CCM/Zanzibar.
Wakereketwa kadhaa wa CCM/Zanzibar walitulizwa kwa kuahidiwa mambo fulani fulani, kwa mujibu wa aliyetupasha habari hizi.
Badala ya ujeuri na kuwachukulia hatua kali wakereketwa hao, viongozi wa juu wa CCM sasa wamekuja kwa matao ya chini na wanawapigia magoti.
Manunguniko mengi ya wakereketwa hao yanahusika na shutuma za wizi wa kura wakati wa kupigwa kura za maoni. Uongozi wa juu umewapelekea salamu za kuwatuliza na kuwaomba waache kulalamika chini kwa chini.
Wao wamekuwa sana wakimshutumu kigogo mmoja wa CCM/Zanzibar (jina tunalihifadhi) wakisema kwamba amedhulumu kwa kulazimisha ushindi wake.
Shutuma pia zimeenea kwamba mke wa kigogo mwengine wa Zanzibar aliiba kura. Shutuma hizi zinashangaza na zinatisha.
Watu wanaulizana, ikiwa CCM/Zanzibar wanaibiana kura wenyewe kwa wenyewe nini utakuwa mustakabali wa vyama vya upinzani wakati wa uchaguzi wa Oktoba 25?.
Mpashaji habari wetu anatueleza kwamba kuna wakereketwa kadhaa ndani ya CCM/Zanzibar wenye kutaka kukihama chama chao lakini hawajiamini na wanaogopana.
Inawezekana kwamba wakereketwa hao wasishiriki kikamilifu katika harakati za kukipigia kampeni chama chao. Kuna dalili nyingine yenye kuashiria kwamba CCM imepata mshtuko:
Vyombo vya habari vya Tanzania (Bara na Visiwani) vilivyo chini ya udhibiti wa dola vimekuwa vikitumiwa kuzipotosha habari kuhusu Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), muungano wa vyama vinne vya upinzani ulioamua kushirikiana katika uchaguzi ujao kwa lengo la kuingoa CCM madarakani.
Kwa jumla, chama kinachotawala na wasaidizi wake na kwa bahati mbaya hawa wako wengi katika vyombo vya dola kimekuwa kikijaribu kumfanya Edward Lowassa, mgombea urais kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kuwa kama ni alama ya ufisadi.
Lowassa anaungwa mkono pia na vyama vingine vitatu vilivyo katika Ukawa Chama cha Wananchi (CUF), NCR-Mageuzi na National League for Democracy (NLD).
CCM kimekuwa kikijaribu kumbomoa kwa kumfanya aonekane kuwa ni kitisho kwa uadilifu wa kisiasa wa taifa la Tanzania. Fani ya kuendesha kampeni za uchaguzi, na uwe wa udiwani, wa ubunge, au wa urais inahitaji weledi wa usanii na ubunifu.
Nchini Tanzania macho na masikio ya wananchi yanategea zaidi kuwasikiliza wanaochuana kuingia Ikulu za Dar es Salaam na Zanzibar.
Wananchi wanatambua kwamba tatizo sio nani wa CCM anayeongoza serikali ya chama hicho bali ni mfumo wa utawala wa chama chenyewe.
Madhali hakuna mabadiliko katika mfumo wa utawala hapawezekani pakapatikana mabadiliko ya maana yatayoweza kuyafanya maisha ya Mtanzania wa kawaida yawe bora.
Kwa namna kilivyo, CCM kinaonesha dalili za kuchoka kutawala. Hakionekani kuwa ni chama chenye mbinu mpya za kimaendeleo zitazoweza kuyageuza maisha ya wananchi.
Tukiliangalia, kwa mfano, suala la ufisadi, ambao sote tunakubali kwamba umekithiri katika takriban ngazi zote serikalini, hakuna hatua thabiti zilizochukuliwa na Serikali ya CCM au na Rais wake kupambana nao.
Hatua aina hizo hazikuweza kuchukuliwa kwa sababu zingegongana na mfumo wa utawala wa CCM. Umasikini nao umekuwa ukiongezeka katika jamii huku serikali ikiwa imeshindwa kuchukua hatua madhubuti za kuufyeka umasikini unaozidi kuwatesa wananchi wa Tanzania, licha ya utajiri wake mkubwa wa maliasili na malighafi.
Tunaweza kuandika orodha ndefu ya mambo ambayo Serikali ya CCM imeshindwa kuyatekeleza na ambayo sasa Magufuli, ambaye ni waziri wake, anasema akichaguliwa Rais atayatekeleza na ambayo hatoweza kamwe kuyatekeleza kwa sababu ya mfumo utaoifunga mikono yake.
Magufuli atahitaji miujiza ili aweze kuyatekeleza mambo hayo katika mfumo ambao unamtega Rais asiweze kufurukuta, akitaka asitake.
Itakuwa ni taabu kwake kuleta mabadiliko ya sera katika mazingira yatayomfunga asiweze kuchukua hatua zitazokwenda kinyume cha utamaduni wa utawala uliozoewa na chama chake.
Tangu aanze kampeni yake ya kuuwania urais, Magufuli amekuwa akiahidi kwamba ataleta mabadiliko, hasa katika mambo ya kupambana na ufisadi na ya kuinyanyua hali ya uchumi. Kwa kutoa ahadi hizo amekuwa wakati huo huo, pengine bila ya mwenyewe kutambua, akikiri kwamba serikali ya chama chake imeshindwa.
Alichokosa kufanya ni kusema wazi tu kwamba hali hii ya uchumi uliozorota ni matokeo ya sera za serikali ya chama chake. Athari moja ya sera hizo ni kuanguka kwa thamani ya sarafu ya shilingi ya Tanzania ikilinganishwa na thamani ya dola ya Marekani.
Bila ya shaka kuna mambo mengine, nje ya Tanzania, ambayo pia yamechangia katika kuporomoka kwa thamani ya sarafu ya nchi hiyo.
Lililo kubwa ni kupungua kasi kwa uchumi wa China, tukio ambalo limeathiri chumi za nchi nyingine zenye ushawishi katika ukuaji wa uchumi wa Tanzania.
Kile ambacho Magufuli na wenzake hawawezi kukataa ni kwamba serikali yao imeshindwa kuwa na mipango kabambe ya kuuimarisha uchumi wa Tanzania unaoonyesha kila dalili za kuzorota, licha ya kuwa kwa mujibu wa takwimu uchumi unakua.
Takwimu zinaweza zikaonyesha kwamba uchumi unakua lakini hali za wananchi zikaendelea kuwa duni kutokana na sera za serikali yenye kutawala.
Kuna mabaya mengi serikalini ambayo Magufuli ameyataja na ameahidi kuyarekebisha lau atachaguliwa awe Rais wa Awamu ya Tano.
Katika mikutano yote ya hadhara aliyoihutubia katika kampeni yake, Magufuli amekuwa akiikosoa na kuilaumu serikali kwa utendaji mbovu wa kazi na ahadi zisizotimizwa.
Amekuwa akiilaumu serikali lakini amekuwa akisahau kusema kwamba serikali anayoilaumu ni ile iliyoundwa na chama chake na yenye kuongozwa na Rais Jakaya Kikwete ambaye ndiye mwenyekiti wa chama hicho kinachotawala.
Hata hivyo, wapiga kura si wajinga na wanalitambua hilo. Viongozi wenzake ndani ya CCM wameona kuwa bora wajaribu kujitoa kimasomaso kwa kukilaumu moja kwa moja chama chao.
Kwa mfano, siku chache baada ya Magufuli kutoa kauli ya kushangaza kwamba CCM haina makosa, Katibu Mkuu wa chama hicho Abdulrahman Kinana alitoa maoni tofauti kabisa Septemba 5, akiwa Moshi wakati wa uzinduzi wa kampeni za ubunge wa jimbo hilo.
Kinyume na Magufuli, Kinana alinukuliwa akisema: CCM tumejaribu kuleta maendeleo lakini lazima nikiri kwamba ndani ya CCM kuna kasoro.
Tuna mijitu hovyo, tuna wezi, tuna majambazi humo na kuna watu wanafiki ndani ya CCM. Bila ya shaka wapiga kura watajiuliza kwa nini waendelee kuwaamini au kuitegemea mijitu hiyo kwa kumpigia kura Magufuli?.
Alichofanya Kinana kama alivyokuwa akifanya Magufuli ni kumpigia kampeni hasimu wao, Lowassa na Ukawa, kwa jumla. Kinana aliongeza kuahidi kwamba Magufuli atakisafisha chama akiwa mwenyekiti, CCM kuna majungu na ulaji, lakini Magufuli atayamaliza Kinana hakusema, lakini, Magufuli atayamaliza kwa kuchukua hatua gani.
Yote aliyoyasema Kinana yanauweka bayana udhaifu wa uongozi wa sasa wa CCM na yanazusha swali la iwapo wenyeviti waliopita wa CCM walishindwa kukisafisha chama hicho, Magufuli atakuwa na uwezo gani wa kufanya hivyo?.
Kinana naye alishangaza alipowatisha wanaotaka mabadiliko ya uongozi wa nchi kwa kutoa mifano ya yaliyotokea Libya, Misri na Zambia. Alisahau kutaja yaliyotokea kwingineko, kwa mfano, Tunisia na Kenya au Burkina Faso.
Hadi sasa ni taabu kutabiri upepo wa kampeni za uchaguzi wa urais unavumia upande gani. Mchuano ni mkali na ndio maana CCM imeshtuka, kinyume na ilivyokuwa katika chaguzi zilizopita.
Lililo wazi ni kwamba mara nyingi katika mikutano yake ya kampeni Magufuli amekuwa akimsaidia Lowassa kila alipokuwa akiikosoa Serikali ya CCM.
Chanzo: Raia Mwema