mgt software
JF-Expert Member
- Nov 1, 2010
- 13,767
- 7,115
Wana JF,
Kwenye mwanga usilete giza, hata kama ukinuna mashavu yakaota sugu lakini kusema ukweli, Rais Magufuri ni Nyota ingaayo kwa mbali kwani mwanga wake unaweza usione kama unakusaidia usiku wa giza totolo. Mheshimiwa Rais tangia aingie madarakani nchi imebadilika sana, ameweza kututoa kwenye dhuruma, utapeli na wizi, ngoja nifafanue kwa yale niliyoyaweka kwenye kichwa cha habari.
DHURUMA
Rais wetu alikuta watu wengi wananyasika kwa kudhurumiwa mali kama mashamba, nyumba hata fedha. Aina ya dhuruma alizozikuta ni kunyanganywa mali kwa wajane, kurudisha mashamba kwa wanakijiji yaliyotolewa kwa majanja na wakayatumia kukopea wakati hawayaendelezi. Kurudisha viwanda vilivyotelekezwa n.k
UTAPELI.
katika awamu zote , utapeli ulikuwa umetamalaki kila kona, kuna aina nyingi za utapeli, kuna utapeli wa madini, mashamba, magari, fedha. Katika kundi la utapeli wa madini kundi la akina Ndama ambalo linapendelea kukaa viti virefu maeneo ya Ambrosia, The billionear club , kundi hili lilikubuhu kutapeli wazungu, watu binafsi, vile vile kwa upande wa nyumba, lakini leo hii wengi wao wanaishi kwa duku duku milija yote imekatwa kwani madini yoote yatakuwa yanaratibiwa na benk kuu.
WIZI
Hili lilikuwa lishakuwa jambo la kawaida kwa kuwa baadhi ya waliopewa dhamana walikuwa wanawalinda sana majambazi ya kwenye mabenki, taasisi za fedha, tangu aingie madarakani kesi za ujambazi wa kuvamia benki zimeisha, Wezi wa kutumia pikipiki wamepungua. Vibaka ambao wengi walipatikana vituo vya mabasi wamepungua.
USAWA NA HAKI
Awamu zilizopita huko maofisini, ulikuwa ukienda mkurugenzi anakuangalia kama kinyago, unaweza kusoteshwa muda mrefu ukifatilia kitu wakati kitu hicho ni cha kumalizwa dakika kumi. Tumeona kunyoosha kwa wahudumua wa kada mbalimbali kama mahospitali, Jeshi la polisi bandarini, machimbo ya Madini.
Kwa nini hapendi siasa, Rais yeye ni mwanasayansi mbobezi kwani alishaona kuwa siasa ni mchezo mchafu ambao una ulaghai ndani yake, tumeshuhudia wanasiasa wengi wakibadilika kama shale wa saa. Angalia kinachoendelea baada ya Zitto kubadilika, angalia Mbowe alivyomkaribisha Lowasa, angalia Mwapachu malamiko yake alipokuwa anarudi CCM, angalia njaa ya Mpendazoe mzee wa kuhama vyama CCK, CCJ CDM CCM maneno yake ya sasa.
Angalia mwenendo wa Nape baada ya kutoka kwenye gamu. hapo ndipo utajua kuwa maana ya siasa ni si-asaaa. yaani sio kitu cha ukweli.