Tunkamanini
JF-Expert Member
- Jul 18, 2014
- 377
- 93
Yako mengi Mhe. Rais anayofanya na kutufanya wengine tubaki midomo wazi na hivyo kushindwa kuelewa whether ni yeye au wasaidizi wake wanampotosha.
Binafsi mpaka leo huwa najiuliza nikikumbuka siku Mhe. Rais alipomnanga DPP Feleshi siku akiongea na waendesha mashitaka pamoja na wapelelezi kisa kesi ya wale samaki wa Magufuli, nilijiuliza maswali mengi sana, kwa sisi tunavyoielewa tasnia ya sheria nchini ilivyo, ukambedha mtu kama mhe. Feleshi utafanya kazi na nani? yule gwiji wa sheria za jinai, kaongoza kitengo kile nyeti kwa miaka mingi kuliko DPP yeyote yule katika historia ya nchi tena akiwa kijana, uadilifu wa Feleshi uliliza mastate attorneys siku JPM alivyozungumza yale maneno.
Kila napohusanisha hili swala na haya yanayoendelea mitandaoni najiuliza, je ni kweli JPM anakuwa hajui hivyo ANAPOTOSHWA na wasaidizi wake au ni vinginevyo?