Rais Magufuli azindua Kiwanda cha Ngozi cha Rostam; Fursa na Changamoto kwenye kujenga Tanzania Economic Miracle

Freddie Matuja

JF-Expert Member
Jul 21, 2018
1,097
2,000
Hii makala nimeandika kama sehemu ya mchango wangu kumshauri Mkulu baada ya kusoma makala nyingine mbayo imeandikwa na mwana JF.

Naomba kuwashirikisha makala hiyo hapo chini; pia ntakupeni nini nafikiri kinaweza kufanyika ili tufike kwenye Tanzania economic miracle au Tanzania industrial economic miracle.


Kuna namna kama nchi inataka kuja na Tanzania economic miracle ikawezekana ndani ya muda mfupi, muda wa kati na muda mrefu kuja na mapinduzi ya kiuchumi.

Rais Magufuli kuja na Tanzania ya viwanda is such a perfect move kama Japan au Tigers countries; isipokuwa il tufike hapo Serikali lazima itengeneze projects financial leverage kwa ajili ya miradi ya serikali hata miradi ya private sector.

Nitagusia kwa kifupi tu kwenye private sector na kwa mfano halisia.

Hyundai ni kampuni binafsi ya magari nchini Korea ya Kusini iliyopata dhamana ya serikali kukopa toka banks za Germany kununua technology, equipment, expertise (hands on experience training kwa Wakorea) ili raia wa Korea wasinunue magari kwa bei kubwa nje ya nchi yao na fedha za zikatoka.

Either ajira badala ya kwenda nje zikabaki ndani kwa kutengeneza vitu ndani.

Tax base ikakua in the course of operating the Motor Vehicle investment.

Kuzaliwa kwa kiwanda kikubwa cha magari, kilizaa viwanda vidogo na vya kati kwenye sekta kama uzalishaji wa

Matairi,
Taa za gari
Wiring and electrical systems
Electronics chip
Cushion za viti,
Side mirrors
Ream za magari...the list goes on.

Why financial leverage, local demand which was substitute by creating a factory which produced products worth of satisfying customers demand.

Leo wakati JPM anafungua kiwanda cha ngozi kinachomilikiwa na Rostam Aziz; Katibu Mkuu wizara ya Mifigo amesema Tanzania ina uhitaji wa jozi 38 mil za viatu.

Local production ni jozi 1.2mil

38mil less say 2mil (maana yake local demand ni viatu jozi (36mil)

Jumuisha mikanda
Mikoba ya kike/
mikoba ya mikutano
Wallet za kiume na kike
Mipira
Cover za magari

Kama kwa miaka 5 hamna Watanzania wenye hela za kuwekeza, it goes without saying kwa miaka 5 ijayo watu kupata fedha kuwekeza kwenye kuzalisha viatu tu; yaweza kuwa ngumu sana.

Ila kama wizara ya uwekezaji ofisi ya Rais na BoT/Hazina ikaja na financial leverage; in less that 36months kuna makubwa yatafanyika kama tutakuja na Project investment financing models kukidhi uhitaji wa soko la ndani, soko la SADC, Africa na nje ya Africa.

Mwisho wa siku every one wins.

Serikali itapanua tax base na hii ndio economic miracle ya mataifa mengi.

The way I view kwanini Serikali ya JPM lazima ije na project investment financing model. Ulazima wake ni kutumia fedha uwekezaji za mikopo kwa kampuni binafsi za Watanzania ili kampuni hizo ziweze kununua

Technology, equipment and Machineries
Knowhow (ili ku-train watu wetu kuwa na hands on experience)

Utegenezaji wa bidhaa zenye ubora utavutia
Soko lililopo ndani na nje ya nchi
Watu wapo wa kununua. Prof. Ole Gabriel ameonesha uhitaji wa soko la ndani kwa viatu ni zaidi ya mil 36.
Tafsiri yake kama tukiwa na viwanda vya viatu kikidhi soko la ndani kwa bei ya sh 20,000 tu. Maana yake kwenye mzunguko wa fedha ndani ni 720,000,000,000. Kama vikilipiwa VAT serikali itavuna 129,600,000,000 toka kwenye viatu made in Tanzania

Ardhi ipo ya kutosha kwa ajili ya uwekezaji

Viatu ni mfano mdogo sana. Nchi hii na nchi 8 jirani ya Tanzania ni soko la bidhaa na huduma chungu mzima. Jumuisha Afrika Mashariki, jumuisha Afrika yote; jumuisha GCC walio jangwani.

Mzee wangu JPM, kwa uhitaji wa SADC wa mafuta ya kula tu; ukulima wa alizeti kutegemea mvua haitoshi.

Lazima twende kwenye commercial farming projects.

Kuna Watanzania wapo wanaweza kukopesheka kabisa na foreign financiers. Nini wanahitaji ni hati ya ardhi, TIC Certification na utambulisho wa serikali kutambua kampuni zao.

Basically serikali yako inaweza kuchukua hisa say 20% in exchange kwa ardhi na TIC Certification.

In the course uwekezaji ufanyike kuzalisha
Mafuta ya kula
Vitambaa vya nguo
Maziwa
Viwatilifu vya kilimo na mbolea
Sukari
Kahawa
korosho... orodha ni ndefu

Mhe. Rais anatakiwa kufahamu sio watendaji/wasaidizi wake wote wana utayari wa kufanya mambo kwa kasi pasi kufuata "michakato ya business as usual."

Nini chahitajika, deliberate effort kujenga ubia kati ya sekta ya umma na sekta binafsi.

Kama tunakubaliana ilitakiwa tuanzs jana mambo haya na kwa kasi zaidi.

Wasalaam

Freddie
 

Star 2

Member
Nov 24, 2020
13
45
Marehemu mzee mengi nakukumbuka.leo mafisadi papa wamekuwa mashujaa.ama kweli dunia hii ni mapito
 

Freddie Matuja

JF-Expert Member
Jul 21, 2018
1,097
2,000
Marehemu mzee mengi nakukumbuka.leo mafisadi papa wamekuwa mashujaa.ama kweli dunia hii ni mapito
Hata wakoloni wetu wa zamani walikwiba sana.
Ujerumani 1885-1919 (miaka 34)
Muingereza nae akakwiba miaka 42; walichukua dhahabu, kahawa, pamba, chai, katani, almasi, kodi na hawajawahi kuomba radhi kwa hilo na kuna wakati "wanatusadia" kwa masharti na masimango.

Rostam bila shaka.

Ila kwa kuwekeza ili azalishe, inapanua wigo wa mauzo ya ngozi zitokazo kwenye machinjio yetu.
Kuna 30% corporate tax atalipa, kuna wafanyakazi 1000 watapata mishahara.

Changamoro ambayo Mkulu katoa angalizo kwa Rostam, management ilipe mishahara inayokidhi huduma ya muda na akili wanazotumia Watanzania kuzalisha kiwandani kwake.

Pia mazingira ya kiafya kwa staff yawepo.

Working gears kama mask, safety boots, overalls na safety boots ili usalama wa afya za staffs uwepo.

Na sisi tunaomba access ya viwanda vilivyorejeshwa hazina ili tutumie hizo kukopa na kuendeleza uwekezaji.

Tusiwe kama Abood aliegeuza assets hizo kufanya biashara tofauti.

Tanzania ya viwanda chini ya JPM inawezekana pale tutakapotengeneza working team spirit ya Public Private Partnership.
 

Tate Mkuu

JF-Expert Member
Jan 24, 2019
7,275
2,000
Natamani kuona hili wazo lako likifanyiwa kazi kwa haraka na msukumo mkubwa. Ila kwa namna ninavyo ifahamu hii serikali na Rais wake, watapuuzia haya maoni yako mazuri na yaliyokwenda shule.


Hongera sana kwa kuwa Mzalendo wa kweli.
 

sysafiri

JF-Expert Member
Sep 19, 2019
638
500
Naona Magu amwemwagiza Prof.Ndalichako tena kwa vitisho vya kutumbuliwa kuhakikisha somo la Historia ya Tanzania linafundishwa mashuleni! Sasa sijui tutatoka lini hapa?
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom