Magufuli 'anajihujumu' mwenyewe...

Magufuli 'anajihujumu' mwenyewe...

Karanja, Ruttashobolwa has never made a sensible statement! Huyu ni pro CCM and therefore he is blind of the truth as long as he has a position in the government! Out of CCM, senses of truth may be will come!
Asante Mkuu kwa muda wako,any way kila mtu anatumia haki yake ya kikatiba.
 
Chadema mnatapatapa sana.

Kila saa Magufuli Magufuli hakauki midomoni mwenu.

Shem to you
Hivi kila anayetoa mawazo yake yanayokwenda kinyume na mtazamo wa CCM tayari anakuwa wa CHADEMA automatically? WanaCCM hawana uwezo wa kutoa mitazamo tofauti?

Shame (not shem) on you.
 
Huyu Magufuli mimi simwelewi kabisa siku hizi.

Alipoanza kuna baadhi ya mambo nilimuunga mkono.

Lakini sasa hivi naona haeleweki kabisa.

Bada ya kupiga kazi tu anaishia kukimbizana na CHADEMA.

Tatizo lake ni nini?

Hana ustahmilizu wa kukosolewa?

Mkuu, huyu mheshimiwa alianza vizuri sana, lakini akafanya kosa kubwa mno alipoamua kunyan'ganya haki za msingi za kikatiba na kisheria za watu wake. Kuanzia hapo, mambo yameendelea kwenda kombo. Shamra shamra za mwanzo alizokuwa akishangiliwa siku hizi zimekuwa adimu, na lugha za hofu toka kwenye mkono wa serikali ndizo zilizotawala. Kila kukicha ni hofu tupu.
 
Mkuu, huyu mheshimiwa alianza vizuri sana, lakini akafanya kosa kubwa mno alipoamua kunyan'ganya haki za msingi za kikatiba na kisheria za watu wake. Kuanzia hapo, mambo yameendelea kwenda kombo. Shamra shamra za mwanzo alizokuwa akishangiliwa siku hizi zimekuwa adimu, na lugha za hofu toka kwenye mkono wa serikali ndizo zilizotawala. Kila kukicha ni hofu tupu.

Hajui labda tofauti ya haki na hisani
 
Samwel Doe alikuwa mbabe sana tena akijivunia utiifu wa jeshi lake la polisi.

Yaliyojiri yako kwenye historia.

Kwanza waliomzunguka ndio hatari kuliko upinzani
anapaswa kujiuliza je wanamuunga mkono kweli au wanamlia timing?
 
Kipindi aliteuliwa kugombea uraisi na chama chake,Kuna mwana CCM (mwandosya sina uhakika sana) alilaumu sana jamaa hana leadership experience yyte.Kinachooneka
leo ndicho hicho hicho.

Mwandosya angekuwa way better than huyu
 
Nafikiri kitakachofuata ni kuzuwiwa kutumia mitandao. Maana naona kila kamanda anapokwenda kwenye vyombo vya habari anatuonya watumia mitandao, sijui tumekosea nini! Sisi kazi yetu ni kutoa maoni tu... huko tunakokwenda itafika siku tutaambiwa tusilale hata na wake zetu!
 
UKUTA, UKUTA! Sasa wanapotosha hata malengo ya UKUTA, wameanza kusema UKUTA unaleta machafuko. Nani kawaambia UKUTA umekuja kwa ajili ya kuleta machafuko? Mbona Operesheni Sangara haikuleta machafuko??? Hawa majamaa wamechanganyikiwa.
 
Kuna vitu Rais yoyote akifanya ni rahisi mno kutengeneza maadui wapya weengi mno

La kwanza ni kuongeza kodi

La pili ni kupiga marufuku 'watu wasiongee'

Kiongozi yoyote akifanya hayo ni dhahiri upepo utabadilika na 'atachukiwa'
haraka mno.

Huhitaji hata vyama vya siasa kubadili huo upepo.

Sasa kama kuna watu wa kumshauri Magufuli, basi wamueleze tu ukweli.

Kwanza awe makini na kupandisha kodi.

Kodi na tozo za biashara mbalimbali zimepandishwa kiholela.

Na sasa watu hawaruhusiwi hata kufanya mikutano, wala makongamano
wala kukosoa kwenye media, hivi vitu viwili vinaweza kufanya Serikali
kutumia 'Jeshi la Polisi' kila siku na kila wakati.

Kuna gharama kubwa mno Serikali itaingia ili kuimarisha Jeshi la Polisi
na kuliweka ready kila siku kwa mambo ambayo busara kidogo ingetumika
kusingekuwa na ulazima.

Yaani wewe nimeshakwambia. Miaka hii mitano tu imalizike na hukupata kiharusi kwa chuki yako dhidi ya Magufuli basi malaika wako mlinzi anafanya kazi.
 
Mimi nafsi yangu ina Amani kweli kwa haya yanayojiri. Maana najua mpaka wajinga waliolala wataamka wajionee.
 
Back
Top Bottom