Magufuli anacheza, akifungwa anashangilia(JAAA)

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2015
Posts
14,242
Reaction score
34,917
Hadi leo ni takribani siku 940 tangu JPM alipoapishwa na kuendelea kuitumikia nafasi ya juu kabisa Kimamlaka katika nchi, nafasi ya URAIS. Hata hivyo, pamoja na matarajio mengi ya baadhi ya watu ambao walidhani JPM ni Lulu ndani ya CCM na anaweza kuwa mwarobaini wa utatuzi wa masuala kadhaa ya kiuchumi na haki katika taifa hili, binafsi ninamuona JPM anayecheza akifungwa anashangilia

Juzi hapa, kaka yangu Tundu Lissu alitumia phrase moja kwamba kuna watu wana kitu kinaitwa "Attention Deficiency Syndrome" bila shaka nikubaliane naye kwa hatua za sasa kwamba tunao watu wa namna hii katika jamii yetu na wengi wao ni wenye mamlaka, tena wanaoamini kwamba mamlaka kwao ni UKUU wenye kujua kila kitu na wala hawawezi kukosea; hivyo kwao "SIFA" hata kwa kazi hasi ni kipimo cha matokeo hayo na si vinginevyo!

Kwa wale wenye maono kama Kaka yangu TUNDU LISSU na wengineo wachache bila kuwataja, tangu mwanzo mara JPM alipokalia kiti kile walimuona na wanaendelea kumuona anatumia NGUVU nyingi za mwili wake kuliko kutengeneza Msingi wa UIMARA wa nchi na Serikali yake kwa kutumia FIKRA na WELEDI Kuna tatizo kubwa mahali fulani!

Kwa wale tuliosoma masomo kama vile International Management na International Economics tunaamini kabisa kwamba uwezo wa kitaasisi(institutional capacity) ukiambatana na uwezo wa rasilimali watu(human resource capacity) na uwezo wa miundombinu(infrastructure capacity both physical and services) ni jambo muhimu katika kufikia matokeo bora ya uzalishaji(productive capacity) na uongozi/utawala bora(Good governance) katika taifa lolote. Bado sijaona kama JPM anatembea katika "a right trajectory" kufikia huko. Ninadhani sisi wakosoaji wake tunatembea ardhini na yeye anajenga baharini. JPM anacheza; anafungwa kisha anashangilia!

Mkwamo wa JPM upo katika mambo mengi lakini tunaweza kuyaweka katika makundi makubwa mawili: HAKI NA UCHUMI

Kwa JPM, HAKI si jambo lenye maana sana. Haki kwake si kitu cha thamani sana ndiyo maana maamuzi yake mengi anafanya nje ya utaratibu wa kisheria na kikatiba lakini zaidi ya hapo si mtu mwenye kuhangaika sana hata kukemea masuala ya utekaji, mashambulizi ya kutumia silaha za moto na mambo kadhaa ya hovyo yanayofanywa na vyombo vyake vya ulinzi na usalama.

JPM ametengeneza "UKABILA" wa kisiasa aliouona kama utamuokoa. Aliamini na bado anaamini kwamba kuua Nguvu ya Upinzani wa vyama vya siasa ingekuwa ni agenda muhimu sana kwake. Waliomshauri katika hili hasa wakati fulani alipoendesha kikao cha chama chake pale kwenye jumba lake jeupe kwamba wadhoofishe upinzani kwa kutumia mfumo wa Rwanda na au tumia aina ya mfumo wa siasa ya China, walimkaanga! Walimkaanga kwa sababu nauona upinzani unaoimarika zaidi na kupata ujasiri na uungwaji mkono mkubwa toka kwa umma wa watanzania. Wamemkaanga kwa sababu ndani ya chama chake pia kuna ukinzani mkubwa wa kimawazo wa namna JPM anavyoendesha chama na serikali. Anapoambiwa mambo kama haya JPM anajiona yupo sahihi. Anacheza, anafungwa kisha anashangilia!

Unapoona Kiongozi wa nchi anatoka hadharani kujibu hoja ambazo hazina uzito wa kujibiwa na yeye jua kuna tatizo mahali fulani. JPM ni mtu wa namna hiyo, ni mtu wa kujitetea, kutishia na hata kauli zake nyingi zina ishara ya kuamrisha "sijaribiwi, watakiona, watakwenda kusimulia, nitashughulika nao huku nje, ningelikuwa IGP na kauli nyingine kama hizo. Pengine JPM anaziona kama zinamuimarisha lakini kwa nafasi kubwa zimemtengenezea ufa katika jamii. Zinammaliza taratibu bila kujua. Yumkini mpaka sasa haongozi kwa amani tena na ni mtu wa hofu kila ukicha!

Uchumi kwa JPM, ni kukusanya bila kuwa na mazingira rafiki ya uzalishaji kwa wafanyabiashara na wawekezaji. Uchumi kwa JPM ni kutokuwa na Sera nzuri ya mapato, uchumi na biashara! Kwake ni kukamua kodi tu! Kwake hataki kusikia Uchumi umesinyaa, ni dhambi!

Mfumo wake(Austerity measures) wa kuamini katika ubanaji matumizi na ukusanyaji wa kodi pasipo kuweka mazingira rafiki umenyausha biashara, umefunga biashara na sasa TRA tunaanza kuwasikia wakiwaomba wafanyibiashara kufungua biashara zao na kukaa kwenye meza ya mazungumzo! It's too late. Bado JPM anacheza; akifungwa anashangilia! Ni rahisi sana kumuondoa mfabiashara katika Cycle, lakini ni vigumu sana kumrudisha tena.

Huko nyuma tulishauri sana jambo la "unnecessary harassment" kwa wafanyabiashara kwamba uchumi ni foreseeable future ya maisha ya biashara na watu. Serikali ikimuumiza mzalishaji leo bila shaka mzalishaji huyo ataondoka(phase out) kwenye pool ya kibiashara. What's the result in the longrun? Biashara zimefungwa, maana yake, taxbase itasinyaa, taxbase ikisinyaa, makusanyo ya serikali yatapungua, sambamba na hilo household income or multiplier effect itasinyaa pia JPM anacheza; akifungwa anashangilia!

Mkaguzi wa Hesabu za Serikali ni Kioo cha kuangalia na kidhibiti matumizi na mwenendo mzima wa fedha za umma; Leo hii JPM anajibu hoja za CAG hadharani. Kwa mfano anasema: "Shilingi 1.5 TRILLION hazijaibiwa" Well! Lakini CAG kwenye Uhasibu wake ameonesha fedha hizo hazijawa Accounted for kwa mwaka wa fedha 2016/17; JPM anatetea bila kuacha na hata kuziagiza mamlaka husika zifanye uhakiki wa jambo hilo. JPM anacheza; akifungwa anashangilia!

Tumeambiwa pia fedha zilizokusanywa kwenye balozi zetu ughaibuni hazijawasilishwa kwenye Mfuko wa Mkuu wa Hazina(Consolidated Account); JPM anacheza; anafungwa kisha anashangilia!

Diplomasia ya uchumi wa dunia pamoja na mambo mengine inaongozwa na Mpango wa dunia (World Order). Kwa JPM hili silioni kama linafanyika katika ustawi. Kwake Mawaziri na Viongozi waandamizi wa Serikali kwenda nje ya nchi kwa ajili ya majadiliano ya fursa za kiuchumi na kibiashara linaonekana ni jambo la ANASA Hata yeye mwenyewe kusafiri nje ya nchi kwa ajili Mikutano ya Kimataifa na kupitia hapo angalau angeweza hata kuwa na Bilateral talk na Wakuu wenzake wa nchi nalo ni Kitendawili! Katika mazingira ambayo tuna mabalozi ambao ni wachache kutuwakilisha katika nchi za dunia, sioni kama economic diplomacy na mission nyingine ya nchi yetu zinaweza kufanikiwa, JPM yupo baharini, sie wakosoaji tupo nchi kavu na wote tunataka tufike CHATO. Challenge! JPM anacheza; anafungwa kisha anashangilia!

Je, huko kwenye balozi zetu tuna Human resource capacity and quality? Je, tuna business acumen? Je, tuna good negotiators? He, tuna Institution capacity? JPM anacheza; anafungwa kisha anashangilia!

ANGUKO LA JPM

Anguko la JPM limetengenezwa na yeye mwenyewe kwa kuamini kwamba matumizi ya NGUVU, UBABE na VITISHO ndiyo njia sahihi ya kuwanyamazisha wakosoaji wa mwenendo usio sahihi katika utawala wake!

Katika siku 940 namuona JPM aliyetengeneza maadui wengi kuliko marafiki na anayeendelea kupunguza marafiki huku akiongeza maadui ndani ya chama na serikali yake, nje ya chama na serikali yake lakini pia Kikanda na Kimataifa. Bado JPM anaona sawa, simuoni kama anawaza hata kufanya "harmonization" ya masuala haya. JPM anacheza; anafungwa kisha anashangilia!

Kiongozi bora ni yule anayeamini kukosea ni sehemu ya maisha ya mwanadamu na anayekubali na kukiri kukosea na hata kukosolewa. Kiongozi yeyote anayeamini kwamba yeye hakosei na kwamba kuwa Kiongozi kumemuweka juu ya uelewa wa mambo yote, huko ni KUKENGEUKA! Kamwe uwezo wa mtu kiakili na Kifikra hauwezi kubadilika au kuwa ni mkubwa na kuwazidi watu wote kwa sababu tu umekuwa RAIS, MBUNGE au KIRANJA wa watu wengine.

JPM anacheza; anafungwa kisha anashangilia! Je, haelewi kwamba kuna anguko? Je, anaona yupo sahihi? Je, ni kiburi tu cha kwamba siwezi kuelekezwa kwa sababu ya ukubwa wa kiti?
 
Utaitwa mchochezi subir uone!.

Mi napita ntarudi baada kupitia maoni ya wadau
 
Hadi leo ni takribani siku 940 tangu JPM alipoapishwa na kuendelea kuitumikia nafasi ya juu kabisa Kimamlaka katika nchi, nafasi ya URAIS. Hata hivyo, pamoja na matarajio mengi ya baadhi ya watu ambao walidhani JPM ni Lulu ndani ya CCM na anaweza kuwa mwarobaini wa utatuzi wa masuala kadhaa ya kiuchumi na haki katika taifa hili, binafsi ninamuona JPM anayecheza akifungwa anashangilia

Juzi hapa, kaka yangu *Tundu Lissu* alitumia *phrase* moja kwamba kuna watu wana kitu kinaitwa *"Attention Deficiency Syndrome"* bila shaka nikubaliane naye kwa hatua za sasa kwamba tunao watu wa namna hii katika jamii yetu na wengi wao ni wenye mamlaka, tena wanaoamini kwamba mamlaka kwao ni *UKUU* wenye kujua kila kitu na wala hawawezi kukosea; hivyo kwao "SIFA" hata kwa kazi hasi ni kipimo cha matokeo hayo na si vinginevyo!

Kwa wale wenye maono kama Kaka yangu TUNDU LISSU na wengineo wachache bila kuwataja, tangu mwanzo mara JPM alipokalia kiti kile walimuona na wanaendelea kumuona anatumia NGUVU nyingi za mwili wake kuliko kutengeneza Msingi wa UIMARA wa nchi na Serikali yake kwa kutumia *FIKRA*na *WELEDI* Kuna tatizo kubwa mahali fulani!

Kwa wale tuliosoma masomo kama vile *International Management na International Economics* tunaamini kabisa kwamba uwezo wa kitaasisi(institutional capacity) ukiambatana na uwezo wa rasilimali watu(human resource capacity) na uwezo wa miundombinu(infrastructure capacity both physical and services) ni jambo muhimu katika kufikia matokeo bora ya uzalishaji(productive capacity) na uongozi/utawala bora(Good governance) katika taifa lolote. Bado sijaona kama JPM anatembea katika "a right trajectory" kufikia huko. Ninadhani sisi wakosoaji wake tunatembea ardhini na yeye anajenga baharini. *JPM anacheza; anafungwa kisha anashangilia!*

Mkwamo wa JPM upo katika mambo mengi lakini tunaweza kuyaweka katika makundi makubwa mawili: *HAKI NA UCHUMI*

Kwa JPM, [HASHTAG]#haki[/HASHTAG] si jambo lenye maana sana. *Haki* kwake si kitu cha thamani sana ndiyo maana maamuzi yake mengi anafanya nje ya utaratibu wa kisheria na kikatiba lakini zaidi ya hapo si mtu mwenye kuhangaika sana hata kukemea masuala ya utekaji, mashambulizi ya kutumia silaha za moto na mambo kadhaa ya hovyo yanayofanywa na vyombo vyake vya ulinzi na usalama.

JPM ametengeneza "UKABILA" wa kisiasa aliouona kama utamuokoa. Aliamini na bado anaamini kwamba kuua Nguvu ya Upinzani wa vyama vya siasa ingekuwa ni agenda muhimu sana kwake. Waliomshauri katika hili hasa wakati fulani alipoendesha kikao cha chama chake pale kwenye jumba lake jeupe kwamba wadhoofishe upinzani kwa kutumia mfumo wa Rwanda na au tumia aina ya mfumo wa siasa ya China, walimkaanga! Walimkaanga kwa sababu nauona upinzani unaoimarika zaidi na kupata ujasiri na uungwaji mkono mkubwa toka kwa umma wa watanzania. Wamemkaanga kwa sababu ndani ya chama chake pia kuna ukinzani mkubwa wa kimawazo wa namna JPM anavyoendesha chama na serikali. Anapoambiwa mambo kama haya JPM anajiona yupo sahihi. *Anacheza, anafungwa kisha anashangilia*!

Unapoona Kiongozi wa nchi anatoka hadharani kujibu hoja ambazo hazina uzito wa kujibiwa na yeye jua kuna tatizo mahali fulani. JPM ni mtu wa namna hiyo, ni mtu wa kujitetea, kutishia na hata kauli zake nyingi zina ishara ya kuamrisha "sijaribiwi, watakiona, watakwenda kusimulia, nitashughulika nao huku nje, ningelikuwa IGP na kauli nyingine kama hizo. Pengine JPM anaziona kama zinamuimarisha lakini kwa nafasi kubwa zimemtengenezea ufa katika jamii. Zinammaliza taratibu bila kujua. Yumkini mpaka sasa haongozi kwa amani tena na ni mtu wa hofu kila ukicha!

[HASHTAG]#Uchumi[/HASHTAG] kwa JPM, ni kukusanya bila kuwa na mazingira rafiki ya uzalishaji kwa wafanyabiashara na wawekezaji. Uchumi kwa JPM ni kutokuwa na Sera nzuri ya mapato, uchumi na biashara! Kwake ni kukamua kodi tu! Kwake hataki kusikia Uchumi umesinyaa, ni dhambi!

Mfumo wake(Austerity measures) wa kuamini katika ubanaji matumizi na ukusanyaji wa kodi pasipo kuweka mazingira rafiki umenyausha biashara, umefunga biashara na sasa TRA tunaanza kuwasikia wakiwaomba wafanyibiashara kufungua biashara zao na kukaa kwenye meza ya mazungumzo! It's too late. Bado JPM *anacheza; akifungwa anashangilia!*Ni rahisi sana kumuondoa mfabiashara katika Cycle, lakini ni vigumu sana kumrudisha tena.

Huko nyuma tulishauri sana jambo la "unnecessary harassment" kwa wafanyabiashara kwamba uchumi ni foreseeable future ya maisha ya biashara na watu. Serikali ikimuumiza mzalishaji leo bila shaka mzalishaji huyo ataondoka(phase out) kwenye pool ya kibiashara. What's the result in the longrun? Biashara zimefungwa, maana yake, taxbase itasinyaa, taxbase ikisinyaa, makusanyo ya serikali yatapungua, sambamba na hilo household income or multiplier effect itasinyaa pia *JPM anacheza; akifungwa anashangilia!*

Mkaguzi wa Hesabu za Serikali ni Kioo cha kuangalia na kidhibiti matumizi na mwenendo mzima wa fedha za umma; Leo hii JPM anajibu hoja za CAG hadharani. Kwa mfano anasema: "Shilingi 1.5 TRILLION hazijaibiwa" Well! Lakini CAG kwenye Uhasibu wake ameonesha fedha hizo hazijawa Accounted for kwa mwaka wa fedha 2016/17; JPM anatetea bila kuacha na hata kuziagiza mamlaka husika zifanye uhakiki wa jambo hilo. *JPM anacheza; akifungwa anashangilia!*

Tumeambiwa pia fedha zilizokusanywa kwenye balozi zetu ughaibuni hazijawasilishwa kwenye Mfuko wa Mkuu wa Hazina(Consolidated Account); *JPM anacheza; anafungwa kisha anashangilia!*

Diplomasia ya uchumi wa dunia pamoja na mambo mengine inaongozwa na Mpango wa dunia (World Order). Kwa JPM hili silioni kama linafanyika katika ustawi. Kwake Mawaziri na Viongozi waandamizi wa Serikali kwenda nje ya nchi kwa ajili ya majadiliano ya fursa za kiuchumi na kibiashara linaonekana ni jambo la *ANASA* Hata yeye mwenyewe kusafiri nje ya nchi kwa ajili Mikutano ya Kimataifa na kupitia hapo angalau angeweza hata kuwa na Bilateral talk na Wakuu wenzake wa nchi nalo ni Kitendawili! Katika mazingira ambayo tuna mabalozi ambao ni wachache kutuwakilisha katika nchi za dunia, sioni kama economic diplomacy na mission nyingine ya nchi yetu zinaweza kufanikiwa, JPM yupo baharini, sie wakosoaji tupo nchi kavu na wote tunataka tufike CHATO. Challenge! *JPM anacheza; anafungwa kisha anashangilia!*

Je, huko kwenye balozi zetu tuna Human resource capacity and quality? Je, tuna business acumen? Je, tuna good negotiators? He, tuna Institution capacity? *JPM anacheza; anafungwa kisha anashangilia!*

*ANGUKO LA JPM*

Anguko la JPM limetengenezwa na yeye mwenyewe kwa kuamini kwamba matumizi ya NGUVU, UBABE na VITISHO ndiyo njia sahihi ya kuwanyamazisha wakosoaji wa mwenendo usio sahihi katika utawala wake!

Katika siku *940* namuona JPM aliyetengeneza maadui wengi kuliko marafiki na anayeendelea kupunguza marafiki huku akiongeza maadui ndani ya chama na serikali yake, nje ya chama na serikali yake lakini pia Kikanda na Kimataifa. Bado JPM anaona sawa, simuoni kama anawaza hata kufanya "harmonization" ya masuala haya. *JPM anacheza; anafungwa kisha anashangilia!*

Kiongozi bora ni yule anayeamini kukosea ni sehemu ya maisha ya mwanadamu na anayekubali na kukiri kukosea na hata kukosolewa. Kiongozi yeyote anayeamini kwamba yeye hakosei na kwamba kuwa Kiongozi kumemuweka juu ya uelewa wa mambo yote, huko ni KUKENGEUKA! Kamwe uwezo wa mtu kiakili na Kifikra hauwezi kubadilika au kuwa ni mkubwa na kuwazidi watu wote kwa sababu tu umekuwa RAIS, MBUNGE au KIRANJA wa watu wengine.

*JPM anacheza; anafungwa kisha anashangilia! Je, haelewi kwamba kuna anguko? Je, anaona yupo sahihi? Je, ni kiburi tu cha kwamba siwezi kuelekezwa kwa sababu ya ukubwa wa kiti?*
Kweli kabisa,ikiwa washauri wake wanaogopa kushauri au wanapuuzwa basi anguko lake halipo mbali inaweza kuwa 2020,kama tukijaaliwa kushikamana kiukweli.
 
Mkuu una mwandikia Autobiography JPM?
Kuna sehemu anapatia na kama binadamu kuna sehemu anakosea.
Tumpe sapoti pale anapopatia basi!
 
Falsafa ya uongozi nyepesi kabisa: kiongozi anayefikiria nguvu ni suluhisho la kuleta ufanisi ni dhaifu. Kiongozi mzuri ni yule anayeunganisha watu kumfanyia kazi.

Mkulu kweli katengeneza maadui wengi na kwa wazi kabisa angalia ulinzi wake kwa sasa. Tulikuwa tunayaona huko nje ambako nchi hizo zinazo ongozwa kiimla lakini sasa tunayaona hapa. Akihutubu hadhara nusu ya watu hao ni walinzi wake! Najua sasa anaanza kubadilika kujaribu kutafuta marafiki, lakini kama ilivyo kwa mteja ukishampoteza ni ngumu kumrejesha.

Kitu kingine kinachoiangusha serikali yangu ni uongo. Wengine wanauita propoganda. Nakubali Serikali zote duniani zina propoganda ya aina fulani lakini inapogeuka kuwa uongo wa wazi unatengeneza kutoaminika. Mambo ya wazi unapoyatetea kuyafanya yawe 'kweli' wakati watu wanajua ni kinyume chake unawajengea usugu wa kukuamini.

Rais wangu waache wataalamu wafanye kazi bila wewe kuwalalamikia hadharani kila wakati. Hawa watakugeuka na utakosa support. Tanzania hatujafika mahali kuwa kama mtaalamu huyu anakosea fukuza uweke mwingine. Hawako wengi kiasi hicho.

Mwisho ni vizuri Rais ukapunguza hotuba zako ili watu wawe na hamu ya kukusikiliza utakapotoa hotuba. Bahati mbaya hotuba zako zinarudia yale yale na zina maudhui ya kulalamika, kutisha, kujisifu na kukejeli. Badilisha hili na uwe Rais wa kuunganisha, kumotisha na kuonesha maono ya maendeleo.
 
Pia Mhe JPM anaangalia maisha katika mitazamo ya ukinzani badala ya ukamilishano. Huu nao ni mtazamo hasi unaoweza kuwa kikwazo katika kuleta maendeleo.

Kwa mfano, katika ziara yake ya juzi mikoani Iringa na Morogoro amedhihirisha udhaifu huu kwa kutoa kauli zinazohimiza ukinzani badala ya ukamilishano: Kiswahili vs. Kiingereza (badala ya Kiswahili na Kiingereza), shule za binafsi vs. shule za umma (badala ya shule za binafsi na shule za umma), mikopo ya elimu ya juu kwa wanafunzi waliosoma shule za binafsi vs. waliosoma shule za umma (badala ya waliosoma za binafsi na waliosoma za umma), maendeleo ya ukanda wa kusini vs. maendeleo ya ukanda wa kaskazini (badala ya maendeleo ya ukanda wa kaskazi na maendeleo ya ukanda wa kusi).

Mtazamo huu ndio unaomsukuma kuangalia chama tawala vs vyama vya upinzani (badala ya chama tawala na vyama vya upinzani). Maendeleo kwa kasi ya JPM hayawezi kuja kwa mitazamo ya ukinzani bali ya ukamilishano.
 
SGR, Stieglers Gorge, Bomba la Mafuta na mengine, ni kati ya mambo yakimalizika tutamkumbuka Magufuli.
 
Maso! siasa za kiafrica zimejaa ghirba na unafiki! Mimi si mnafiki the guy is out of tune! I doubt if he knows what he is doing!

I started doubting him the day he utterer something odd! " Saddam was a Libyan president oooh no a quwait president! wasingekuwa akina sisi he would have been out Tayari!
 
Back
Top Bottom